Tangu nilipojua jinsi Watanzania walivyo nimepunguza sana kuwalaumu viongozi

El Roi

JF-Expert Member
May 29, 2020
263
502
Kuna wakati nilitembea nchi fulani nje ya hapa. Kulikuwa na shughuli iliyohusisha watu kutoka nchi mbalimbali . Tukiwa pale wenzetu wakenya na waganda waliokuwepo walionekana kutokuwa karibu na sisi mpaka tulipokuja wasikia mahali fulani wakisema hawa watanzania wape maneno mengi tu na kiswahili kirefu lakini hawajui lolote.

Nakumbuka mtanzania mwenzangu niliyekuwa nae jinsi alivyong'aka na kugombana nao sana, mpaka ikatishia amani.

Mimi pia pamoja na kuwapinga nilienda hatua moja zaidi na kujiuliza Kwa nini jamaa walituona vile. Katikati ya kongamano lile nikaanza kugundua kiasi Kwa Nini jamaa walikuwa wakitudharau.

Watanzania ndo walikuwa hawajali muda, hawajui kujenga hoja zenye kina wakati wa majadiliano. Hawaongei kiingereza grammatical, hawajui kutumia vifaa vya technologia ya kisasa na hawajui hata kudai na kukumbushia tu haki zilizokuwa zinatuhusu kwenye workshop hiyo. Bafuni wanaenda kuoga wawili wawili wakati mabafu yako tele na ni haki kuoga mtu mmoja.

Baada ya utafiti wangu huo nikaanza kuamini kiasi maneno ya wale jamaa.

Tuliporudi, ndo hasa nikaona uhalisia wa mambo waziwazi.

Nilitembelea ofisi ya mbunge ambayo iko kwenye majengo ya serikali, ilikuwa imefungwa siku zote wananchi wakienda na kurudi lakini hakuna aliyeuliza hata tu kugomba kwamba mbunge wao Kwa Nini alikuwa hapatikana ofisini na hata katibu wake?

Kwa sababu ya ujasiri nilioupata baada ya dharau za ughaibuni, nilienda ofisi ya mkuu wa wilaya kitengo Cha malalamiko nikatoa madai Kwa nini mbunge wala katibu wake hawako ofisini, kesho yake tu ofisi ikawa wazi na katibu wa mbunge akaanza kukutana na wananchi.

Najiuliza, watu wengine wote hapo mwanzo hawakuona adha hiyo? Na Kwa Nini walikuwa kimya muda wote? Nakumbuka mmoja wao akinambia siku ya pili niliyokuwa nataka huduma za ofisi hiyo" Baba tunazunguka hapa Sasa karibu wiki ofisini imefungwa tu". Imagine!!

Wakati naamia eneo lingine la makazi , mtaa huo ulikosa umeme kabisa kwa muda wa kama miaka mitatu hivi, achilia mbali kwamba mitaa yote ilikuwa tayari na umeme. Tanesco waliliacha eneo makusudi kabisa kwa sababu walizojua wenyewe

Wakati natoa wazo la kufuatilia umeme mtaani kwenye mamlaka husika, wakazi wa eneo hilo nakumbuka wakiniambia" achana na Tanesco huwawezi".

Wengine walionesha mpaka namba za malipo yaliyokuwa wameshafanya tanesco maarufu control number lakini hawakuwa bado na huduma hiyo achilia mbali rushwa kubwa waliyokwisha toa.

Tulipata huduma ya umeme baada tu ya kuufuatilia mie mwenyewe kimkakati kwa kumuona na kudai kwa kila aliyehusika. Nakumbuka jinsi wengine walivyorudishiwa pesa walizokuwa wameshawaonga vishoka na wafanyakazi wa chini kabisa wa Tanesco walowapa control namba fake . Najiuliza watu wote kwenye mtaa pamoja na wingi wao walishindwa kudai haki yao hiyo?

Ndugai wakati anamfukuza mtu aliyepigwa risasi bungeni akiwa kwenye matibabu, wananchi wake wa kongwa walishindwaje kumpinga hata tu kwa mkutano wa chama chake kwamba hiyo tu siyo kukiuka haki za mtu bali siyo ubinadamu? Nchi nayo tulikuwa wapi hata kupiga kelele tu?

Leo nimeshangazwa na wabunge wetu. Wakati waziri mkuu anakuja kueleza hatua za serikali ilizochukua juu ya uzimaji moto mlima. Kilimanjaro na kusisitisha operation ya kusajiri mifugo kiektronik, nilishangaa kuona makofi makubwa yakipigwa na wabunge kwa waziri mkuu kana kwamba ameshatoa maelezo yaliyowaridhisha.

Ajabu baada ya maelezo ya waziri mkuu waliuliza maswali ya ukosoaji kana kwamba siyo wao waliokuwa wanapiga hayo makofi. Hivi mtu anayepigiwa makofi kiwango kile hata hajajibu hoja maana yake ni nini?

Sasa, watu wamesema mengi. Ooh mara hatuna elimu ya kutosha, sisi ni waoga, tunapenda amani, nk. Sikatai haya yote yanaweza Kuwa majibu ya matatizo yetu.

Na kama ni hivyo, basi lawama zisiende kwa viongozi TU kama tunavyofanya. Tujilaumu wenyewe.

Nimewahi kusema hapa kwamba siyo viongozi tu ndio wanatakiwa na jamii, bali viongozi nao huitaji jamii inayojielewa ili wawajibike zaidi. It isn't only leaders who shape the society, the leaders also need the society to shape them.

Nchi hii haifanyi vizuri sana siyo Kwa Sababu ya viongozi tu. Tatizo kubwa kuliko yote ni sisi waongozwa. Hatujielewi, ni waoga, tunajipendekeza, tunaishi kama nchi hii siyo yetu bali Iko nchi yetu nyingine na sisi ni wapangaji. Tuko kimya hata atukemei ubaya wa waziwazi, hatuwaoji viongozi mambo magumu, hatukatai viongozi au watumishi wasiotutendea haki.

Niambie katika mazingira hayo ni nani wa kulaumu? Style yetu ya maisha ndo inatupa viongozi Hawa tunaowalaumu. Haya ni matunda ya jinsi tulivyo, tuyale.
 
Safi sana kwa kuweka mawazo yako wazi hapa jukwaani ili yasomwe na wengi. Tatizo mawazo haya kila mtu anakuwa nayo akishakuwa mtu mzima, ukiwa katika ule umri wa primary au sekondari huwezi kuwa na mawazo mapana kama haya.

Ukishaanza kujitegemea na kujua mbivu na mbichi akili na yenyewe inatanuka na kujiuliza maswali mengi kuhusu Tanzania yetu.
 
Aliyelala chato alionyesha jitahada za dhati kurekebisha tabia. mwisho wa siku wengine wakaishia kumuombea afe sababu hawajazoea maisha hayo.

Watanzania wameridhika wanalia siku mbili then wanasahau na maisha yanaendelea.

Na hili furushi lililobaki hapa ndio kabisa.
 
Tatizo la watanzania wengi hasa hawa vijana waliozaliwa miaka ya 90 kuja juu wamekubali kuuza utu wao kwa sababu ya njaa zao.

Yan wenye elimu na wasiokuwa na elimu wote wamekubali kufanywa mitaji, ngazi au madaraja na hawa wanasiasa uchwara wa Tanzania.

Wakati wenzetu wako busy kupambana na changamoto za maisha huku wakichangamkia fursa mbali mbali. Watanzania wao wako busy na siasa, upinzani uchwara nk. So lazima wenye akili wawakimbie.

We fikiria unakuta mtu anakataa kwenda kwenye msiba wa kaka yake waliezaliwa nae tumbo moja, kisa kwa sababu wakati wa uhai wake kaka huyo hakumpigia Lisu au Zito kura.

Mungine anakataa kwenda mpiran kisa kule kuna watu wanavaa sare za yanga zinazofanana na sare za CCM.

Kizazi cha sasa cha Tanzania kimevurugwa zaidi na wanasiasa uchwara wanaofaidi maisha kupitia ujinga wa hawa vijana.
 
Viongozi take advantage of situation na hawapo kutaka kubadili. Japo ni lazima walaumiwe sababu wanalipwa kwa kodi za wananchi!
 
Shida hii ni kubwa sana na inahatarisha maendeleo ya taifa. Kwakuwa naungana nawe mtoa andiko.

Niwazi kwamba kunahitajika sasa kutoa Mawazo mbashara na mbada kutoka kwa washika dau hapa JF, Mitandao mingine ya kijamii ili kupata Mawazo na njia sahihi ya kuwa-shape watanzania hasa watoto na vijana.

Vyuoni, mashuleni,na ngazi za familia ni muhimu kuanza kubadili mienendo na utaratibu wa kuzipinda ,kuzijari Mila na desturi zetu , Utu wa watu ni muhimu Sana kuujari kwani huko ndiko kunako weza kuwafanya watu wajari maisha ya watu na amali zao zote.

Ni vigumu Sana mtu kuthamini Mali ya jamii/ nchi ikiwa haja fundishwa kujari Utu wa watu na umuhumu wake.
 
Aliyelala chato alionyesha jitahada za dhati kurekebisha tabia. mwisho wa siku wengine wakaishia kumuombea afe sababu hawajazoea maisha hayo.

Watanzania wameridhika wanalia siku mbili then wanasahau na maisha yanaendelea.

Na hili furushi lililobaki hapa ndio kabisa.
RReigns, kwani huioni jamii yenyewe ya watanzania kwamba ndo tatizo? Huyo mmoja unayemsema akiongoza jamii inayojielewa atabadirika lazima au ataacha hayo madaraka kwa sababu ya challenge kama hawezi.

Wananchi, wananchi, wananchi.
It is time to change.
 
RReigns, kwani huioni jamii yenyewe ya watanzania kwamba ndo tatizo? Huyo mmoja unayemsema akiongoza jamii inayojielewa atabadirika lazima au ataacha hayo madaraka kwa sababu ya challenge kama hawezi.

Wananchi, wananchi, wananchi.
It is time to change.
Basi huenda tuna shida kwenye mfumo wa elimu na malezi tunakuzwa kwa kuwa waoga.
 
Hii Nchi imejengwa kwa watu kuwa na hofu na wasio wadadisi Wala kuhoji..

Unaehoji unaonekana wa ajabu kuanzia mtaani hadi Taifani..

Sasa usijichoshe Sana kuwapigania Watzn komaa na mambo yako ndugu.
 
Hapo ndipo akili na consciousness ya raia wengi wa taifa hili vilipokomea, huenda evolution yetu iko katika hatua za awali
Tuupe muda nafasi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom