Tanganyika Mbona Mnajikanyaga?

Status
Not open for further replies.

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,432
3,006
Membe-564x272.jpg

Membe nimemsikia akitoa msimamo wa Tanzania juu ya taifa la Sahara magharibi ambayo inatawaliwa na Morocco ambao wameomba kujitenga na kuwa nchi huru kuwa wanapendekeza wana Sahara Magharibi wapige kura ya maoni kuamua kama wanataka kutawaliwa au wajitawale wenyewe.
Na amezidi kusema Tz ni nchi huru inapenda kila nchi na wananchi wake waamue jinsi gani ya kuishi na kuamua juu ya nchi zao

Muono wangu mbona Zanzibar wanagoma kuwaruhusu kupiga kura ya maoni juu ya nchi yao?
 
Huu ndio undumilakuwili wenyewe,

Ila sio mara ya kwanza hata Nyerere alishafanya Nigeria!
 
Ni sawa na kujigeuza mbuni kutia kichwa kwenye mchanga haliyakuwa kuna kiuno kimebaki nje eti tumejificha,hawa ndio viongozi wetu.

Viongozi wa Serikalia ya muungano wanajidai kujifanya watu wa democracy ila sio kweli,kwa wao wanao uwo udemocracy basi watupe kura ya maoni zanzibar juu ya muungano,kama tunautaka au hatuutaki ? Kwa maneno tushasema na kwa hisia tumeshatoa,na kwa vitendo tayari tumefika hadi baraza la wakilishi,kilichopo viongozi wa ccm kutumia nguvu za dola kuwanyamazisha wazanzibari ,na baadhi ya jumuia za kiraia kutotoa elimu juu ya muungano.

Na jengine zaidi kutumia nguvu ya dola kuwazibiti wale wote ambao wanatahadharisha kuvunja muungano kwa nini ? Huu muungano sio bibilia wala msahafu,tunaweza kuujadili kwa njia yoyote ile.

Naamini iko siku utafika mwisho,lakini watambue viongozi kuwa muungano wanaulamisha hasara yake itafika kwa wananchi,itafika wakati tutahamisiana baina ya wazanzibari na watanganyika,tutachukiana na tutauwana,hisia za wananchi tayari ziko wazi kabisa.

ELEWA hilo viongozi .
 
watumieni wawakilishi wenu na serikali yenu ya znz kudai huo uhuru wenu. Ila T. LISSU aliwawakilisha bungeni mkamgeuka kwa kumtusi na dharau nyingi. Kuweni na msimamo mmoja kwanza afu muamue mkitakacho.
 
Tatizo lenu mnataka kusafiria nyota za wengine! Agenda ya kuandika katiba mpya mnataka kuibebesha na kura ya moni kuukataa muungano juu yake! Haiko hivyo, tumieni mamlaka zenu kuufikisha ujumbe katika ngazi ya serikali ya muungano. Wawakilishi watoe tamko,na kwa kuwa kuna wabunge wanaoliwakilisha baraza la wawikilishi, basi wafikishe katika bunge
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom