Tanga watatangatanga sana

mchafukuoga

Member
Apr 17, 2011
24
9
jamani wana jamvi mwenye habari kamili nasahihi atujuze,
kuna kampuni inaitwa athi riva imenunua eneo kubwa sana kwa ajili ya kuzalisha saruji tanga na kuna wafugaji wa n'gombe wa maziwa katika hilo eneo la kuanzia maweni hadi amboni:
nina wasisi kama inaweza watu wafukuzwe .
mwenye habari sahihi na za uhakika atujuze.
tunaogopa kutanga tanga :mod:

watu wafukuzwe coz of hao ng'ombe wa maziwa au? nway, kuna kiwanda kipya cha saruji (rhino cement) kinajengwa maweni karibu kabisaaaa
na kiwanda cha chokaa hapo maweni but cdhani kama kitasababisha hamahama kwani kiwanda cha simba cment ndo kipo
karibu kabisaa na makazi ya watu pamoja na hao ng'ombe wa maziwa na nyama pia.
 
eneo la ng'ombe wa maziwa linafahamika mipaka yake..tena kubwa sana ndani yake kuna chuo cha liti buhuri..rhino cement wao wamepewa pia eneo kubwa wanapakana na simba cement upande wa magharibi..rhino walianza na kutengeneza chokaa na sasa wanajenga ma sailos kwa ajili ya kuzalisha cementi
 
sawa je wanatoa wapi malighafi ( raw materials) kama mawe?
ili utengeneze saruji ni lazima uwe na mawe yakutosha.
nyuma ya hicho kiwanda kuna eneo kubwa sana lenye mawe
na ndio huko kuna wafugaji wadogo wadogo kwa uande unaopakana na amboni.
VUTA TASWIRA VIZURI NA PIA FIKIRIA KWA MAKINI.:mod:
 
Nilivyowahi sikia ni kwamba lile eneo la Amboni limenunuliwa na mwekezaji atatengeneza chokaa? pia kuna waturuki wamenunua mamia ya ekari kwa ajili ya kujenga shule/ chuo. Pia niliwahi sikia kuwa maeneo hayo kuambaa na bahari kutajengwa au limetengwa kwa ajili ya satelite town/city. Hivyo ni a long run wafugaji watabanwa wasiwe na mahali pa kufugia.
 
kama ni kweli kuhusu viwanda & shule ... safi sana! wafugaji watatufuta njia nyingine ya kufuga.. zero grazing etcl ...
 
Waliihasidi Tanga kwa muda mrefu sana, kisa, nyerere hakukubalika huko. Sasa twayaona maendeleo babu wee, barabara zajengwa. Viwanda vyarudi, mpaka wanja la mpira la FIFA wakachakuwa lisijengwe huko, wakastukiwa. Bandari yaja.

Haa, Kikwete wewe wanikooooosha mpaka ndani ya roho, Wallahi. Tanga hii Tanga yashamiri kila kukicha toka huyu bwana atwae madaraka.
 
Waliihasidi Tanga kwa muda mrefu sana, kisa, nyerere hakukubalika huko. Sasa twayaona maendeleo babu wee, barabara zajengwa. Viwanda vyarudi, mpaka wanja la mpira la FIFA wakachakuwa lisijengwe huko, wakastukiwa. Bandari yaja. Haa, Kikwete wewe wanikooooosha mpaka ndani ya roho, Wallahi. Tanga hii Tanga yashamiri kila kukicha toka huyu bwana atwae madaraka.
Nipo tanga lakini unayosema hayaendani ukweli halisi, tanga kiuchumi inashuka imebaki umaarufu tu.
 
Nipo tanga lakini unayosema hayaendani ukweli halisi, tanga kiuchumi inashuka imebaki umaarufu tu.

Upo sahihi kabisa nilisoma na kuanza kazi huko miaka ya mwisho ya sabini ukiangalia na sasa haviendani. Labda hiyo miradi mipya inaweza kuirudisha kama zamani.
 
Waliihasidi Tanga kwa muda mrefu sana, kisa, nyerere hakukubalika huko. Sasa twayaona maendeleo babu wee, barabara zajengwa. Viwanda vyarudi, mpaka wanja la mpira la FIFA wakachakuwa lisijengwe huko, wakastukiwa. Bandari yaja.

Haa, Kikwete wewe wanikooooosha mpaka ndani ya roho, Wallahi. Tanga hii Tanga yashamiri kila kukicha toka huyu bwana atwae madaraka.
Kweli Tanga ile siyo hii ya leo,miaka ile ukiamka alfajiri mji umechangamka....mabasi ya wafanya-kazi wa saruji yanapita ktk vituo kupitia wafanyakazi,watu wa mbolea wanajivuta taratibu kazini wachilia mbali chuma,foma upande wa michezo usiseme ukisikia leo Coastal wanacheza na Bandari ya Tanga unahamu ya kwenda mpirani,kila kiwanda kilikuwa sehemu ya michezo,kawaida kusikia wkend maskani fulani wameandaa picnic,iwe Kigombe,Pangani or somewhere else...pengine haya yanayokuja yatarejesha hadhi ya mji wa Tanga..wenyewe wanaliiita jiji..
 
cementi raw material kubwa ni redsoil,mawe na pozolana wanayotoa moshi..redsoil ndio inatumika zaidi material zipo za kutosha mfano machimbo ya tanga cement hayajaenda mbali sn tangu kiwanda kimeanzishwa na wana material ya kutosha miaka 100 ijayo..rhino hawatafika huko amboni unaopajua wewe nao wanaeneo la kutosha..nimefanya field practical 3 times pia nilishi saruji kotaz kwa miaka 7 hivyo naelewa sn haya maeneo unaezungumzia..mpaka kule pande(karibu na kambi ya jeshi) bado mawe mengi tu watu sio wajinga kufungua kiwanda kipya!
 
Nipo tanga lakini unayosema hayaendani ukweli halisi, tanga kiuchumi inashuka imebaki umaarufu tu.

Hujaenda barabara ya horohoro ukaiona inavyotengenezwa? Hujaona Tanga Fresh inavyovutia ukiingia Tanga? Hujaona jiwanda la Saruji linavyopendeza usiku ukiingia? hujaona jiwanda la unga (sijui laitwaje lile)? hujaona na hili linalosemwa hapa laja? hujaona wakilipwa kule itakapo jengwa bandari mpya? Taratibu lakini twayaona.
 
Waliihasidi Tanga kwa muda mrefu sana, kisa, nyerere hakukubalika huko. Sasa twayaona maendeleo babu wee, barabara zajengwa. Viwanda vyarudi, mpaka wanja la mpira la FIFA wakachakuwa lisijengwe huko, wakastukiwa. Bandari yaja.

Haa, Kikwete wewe wanikooooosha mpaka ndani ya roho, Wallahi. Tanga hii Tanga yashamiri kila kukicha toka huyu bwana atwae madaraka.

ushabiki maandazi tu. Hivyo viwanda vilivyokuwepo zamani alijenga babuyo?
 
Back
Top Bottom