TANESCO yasimamisha kuunganisha umeme tangu Mei

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
20,693
20,454
Kuna habari kwamba shirika la umeme nchini (TANESCO) limesimamisha kuunganishia wateja wake wapya huduma hiyo muhimu. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari hii toka ndani ya shirika hilo, sababu kubwa inayotolewa na shirika hilo ni kukosekana kwa nyaya za kuunganisha kutoka kwenye mlingoti kwenda katika jengo (service line) na kwamba mteja wa mwisho kupata huduma hiyo katika mkoa wa Ilala (wa TANESCO) aliwekewa mwezi wa Mei 2010. Kama kuna ukweli wa habari hii, maana yake ni kwamba iwapo ataonekana mteja ameunganishiwa umeme hivi karibuni, basi huyo atakuwa ametoa rushwa au amepita njia za 'panya' na anatakiwa aripotiwe TAKUKURU ili wachunguze ni nani amemuwekea umeme na ametoa wapi nyaya wakati inajulikana kwamba nchi nzima hakuna nyaya na huduma ilishasimamishwa. Naona MD mpya amekuja na mikosi. Karibuni jamvini ...

NB: Naombeni msaada wa kisheria kwani nataka niwashitaki TANESCO kwa kukiuka mkataba wa kuniwekea umeme ndani ya siku 60 baada ya kufanya malipo halali.
 
Inawezekana kabisa na mimi nipo mmojawapo nitatoa ushahidi hadi leo sijapata umeme tokea nilipiae Mwezi wa Sita.
 
Kuna habari kwamba shirika la umeme nchini (TANESCO) limesimamisha kuunganishia wateja wake wapya huduma hiyo muhimu. ........., sababu kubwa inayotolewa na shirika hilo ni kukosekana kwa nyaya za kuunganisha kutoka kwenye mlingoti kwenda katika jengo (service line) na kwamba mteja wa mwisho kupata huduma hiyo katika mkoa wa Ilala (wa TANESCO) aliwekewa mwezi wa Mei 2010.

Kwa mwendo tutayafikia lini maisha bora kwa kila Mtanzania?
 
Naendelea kukusanya maoni ili niwaburuze hawa jamaa mahakamani.
 
mimi nililipia mei wakahaidi kuja tarehe 30 june,lakini hiyo tarehe ikapita hawakuonekana.Nilipoona muda unazidi kwenda nikaenda kuwauliza mbona muda umepita waliohaidi,wakasema hawana mita za luku.Wiki iliyopita nilifuatilia tena, wanadai hadi baada ya uchaguzi.
 
Kuna habari kwamba shirika la umeme nchini (TANESCO) limesimamisha kuunganishia wateja wake wapya huduma hiyo muhimu. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari hii toka ndani ya shirika hilo, sababu kubwa inayotolewa na shirika hilo ni kukosekana kwa nyaya za kuunganisha kutoka kwenye mlingoti kwenda katika jengo (service line) na kwamba mteja wa mwisho kupata huduma hiyo katika mkoa wa Ilala (wa TANESCO) aliwekewa mwezi wa Mei 2010. Kama kuna ukweli wa habari hii, maana yake ni kwamba iwapo ataonekana mteja ameunganishiwa umeme hivi karibuni, basi huyo atakuwa ametoa rushwa au amepita njia za 'panya' na anatakiwa aripotiwe TAKUKURU ili wachunguze ni nani amemuwekea umeme na ametoa wapi nyaya wakati inajulikana kwamba nchi nzima hakuna nyaya na huduma ilishasimamishwa. Naona MD mpya amekuja na mikosi. Karibuni jamvini ...

NB: Naombeni msaada wa kisheria kwani nataka niwashitaki TANESCO kwa kukiuka mkataba wa kuniwekea umeme ndani ya siku 60 baada ya kufanya malipo halali.

Huko Iringa sasa hawapokei hata pesa ya kuunganishja umeme kwa madai hayohayo-hawana nyaya! Sasa kama huko Dar ni huku mikoani tumekwisha.

Kwa mujibu wa sheria wamefanya kosa kwa kushindwa kukuunganishia umeme baada ya kupokea malipo yako, nenda EWURA kawashitaki na kabla ya hayo anza kuwalima barua ya notisi kwanza kwa Meneja wao.
 
Duu ! Hii ni dhambi jamani. Sasa kama wameshindwa umeme , na maji ndio shida - hivi internet wataiweza kweli ?
 
Back
Top Bottom