TANESCO, tangazeni rasmi kuwa mgao wa umeme umeanza

mansoorsaid

JF-Expert Member
May 31, 2014
1,498
284
Nipo karibu siku kumi hapa Dodoma, naona umeme unakatika maeneo kwa maeneo masaa 24. Hebu mtueleze, kuna mgao? Ili tujue tuweze kupanga mambo yetu.

1. HALI YA UZALISHAJI UMEME

Tunatoa taarifa hii ili kuufahamisha umma hali halisi ya umeme ilivyo, changamoto zilizopo na matarajio ya hali itakavyokuwa katika siku za karibuni. Tunafanya hivyo ili kuondoa minong'ono, uzushi na taarifa nyingi za kubuni ambazo zimekuwa zikizunguka katika vyombo mbali mbali na hasa katika mitandao ya kijamii.

a) Umeme wa Maji

Hadi tarehe 4/10/2015 Mabwawa karibu yote hayana maji ya kutosha na baadhi yanaelekea kukauka kabisa. Ifuatayo ndiyo hali halisi ya Uzalishaji umeme kwenye Mabwawa yetu kwa sasa:

Mtera: Uwezo wake wa juu – 80 MW
Uzalishaji kwa sasa – 0

Kidatu: Uwezo wake wa juu - 204 MW
Uzalishaji kwa sasa - 27 MW

Kihansi: Uwezo wake wa Juu - 180 MW
Uzalishaji kwa sasa – 51.5 MW

New Pangani Falls: Uwezo wake wa Juu – 68 MW
Uzalishaji kwa sasa – 17 MW

Hale: Uwezo wake wa Juu – 21 MW
Uzalishaji kwa sasa – 4 MW

Nyumba ya Mungu: Uwezo wake wa Juu – 8MW
Uzalishaji kwa sasa – 5.5MW


Uwezo wa juu wa Mitambo yote ya Maji – 561 MW
Uzalishaji wote wa Umeme wa Maji kwa sasa – 105 MW sawa na 18.7% tu ya uwezo wake

Kwa lugha sahihi uzalishaji umeme katika mabwawa ya maji umeshuka kwa 81.3%!

b) Uzalishaji Umeme kwa Gesi ya SongoSongo

Kwa sasa Kampuni ya Pan Africa inatekeleza mradi wa kuviboresha visima vyake ambavyo uwezo wake wa kuzalisha gesi ulikuwa umeshuka sana hadi kufikia Megawati 260 tu kutoka Megawati 340 tulizokuwa tunapata mwanzoni.

Kwa taarifa walizotoa, wamekamilisha ukarabati wa Kisima no. SS9 na sasa wanaaza ukarabati wa SS5. Japo ukarabati huo utatuhakikishia gesi zaidi baadaye lakini wakati huu wa matengenezo panakuwa na uhaba wa gesi kutoka Songosongo.

c) Uzalishaji umeme kwa Mitambo ya Mafuta

Mitambo ya mafuta yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 230 inazalisha Megawati 190 kwa sasa.

d) Uzalishaji wa Umeme kwa Gesi – Bomba Jipya.

Mitambo ya kuzalisha umeme kwa Gesi ya Bomba jipya iliyokwishawashwa ni ya Megawati 90 na leo tunatarajia kuongeza mwingine wa Megawati 35.

Pamoja na Megawati hizo 90 zilizoungwa kwenye bomba jipya tarehe 21 Septemba 2015 tuliwasha mtambo mwingine wa Megawati 20 ukitumia gesi ya bomba la Songosongo na kufikisha kiasi cha umeme ulioongezeka kufikia 110 MW.

Mitambo mingine inayotarajiwa kuongezeka ndani ya wiki moja hadi mbili zijazo ni Symbion 20 MW, Ubungo II – 35 MW na Songas – 20 MW na Kinyerezi 70 MW. Mtambo wa mwisho wa Symbion 20 MW unatarajiwa kuwashwa mwishoni mwa mwezi Oktoba 2015.

KWA NINI BOMBA JIPYA LA GESI LIMEKAMILIKA LAKINI TATIZO LA UMEME HALIKWISHA MARA MOJA?

Baada ya Bomba la Gesi kukamilika, visima viwili kati ya vine vya M&P vilianza kuingiza gesi kwenye bomba kule Mtwara tarehe 22/8/2015 na Gesi hiyo kufika Dar es Salaam tarehe 5/9/2015 yaani wiki mbili baadaye. Hata hivyo gesi hiyo ilifika Dar es Salaam ikiwa na Pressure ya 2 Bars.

Ilichukua wiki mbili hadi Pressure kufika 37 Bars na kuwezesha kuwasha mitambo ya 90 MW pale Ubungo. Hata hivyo mitambo mikubwa iliyokuwa imebaki ikiwemo ule wa Kinyerezi ulihitaji pressure ya 55 Bars ili iweze kuwashwa au kuanza majaribio ya kuwashwa.

Baada ya Mitambo hiyo ya 90 MW kuanza kufyonza gesi kutoka kwenye bomba kwa kiwango cha futi za ujazo milioni 21 kwa siku kasi ya pressure kuongezeka ilishuka sana kutoka 3 Bars per day hadi 1 Bar per day.

Hivyo ilichukua siku 12 hadi tarehe 29/9/2015 yaani siku tano zilizopita kwa pressure kufika 55 Bars na hivyo kuwezesha Mitambo mingine kuanza kutest ikiwemo ya Symbion na Kinyerezi. Sambamba na hilo, Kisima cha tatu cha Mnazi Bay kilikamilika na kuwa tayari kuingiza gesi kwenye Bomba tarehe 1 Oktoba 2015 yaani siku nne tu zilizopita.

MTAMBO WA KINYEREZI

Mtambo huu ni mpya na kazi za kuukamilisha zilikuwa zinategemea sana upatikanaji wa gesi katika msukumo sahihi wa 55 Bars uliofikiwa tarehe 29 September 2015 na kazi za kusafisha mabomba kwa kupitisha gesi yenye msukumo mkubwa ilipoanza.

Kazi hizo zitaendelea hadi pale wataalam wa Kampuni ya General Electric iliyotengeneza mtambo huo watakaporidhika kwamba mabomba yote ni masafi na Turbines zinaweza kuanza kuwashwa.

Kwa taarifa tulizopokea kutoka kwa Kampuni ya Lahmayer ya Ujerumani ambaye ndiye Msimamizi Mkuu wa Mradi (Supervising Consultant), inaonyesha kwamba kwa sababu ya kuchelewa kupata Gesi katika msukumo wa 55 Bars, Mitambo miwili ya Kinyerezi yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 70 inatarajiwa kuwa tayari kuwashwa ifikapo tarehe 14 Oktoba 2015.

Hii inatokana na kwamba kabla ya kuwasha ni lazima samples za gesi zitumwe GE kwa uhakiki kwanza.

Mitambo miwili ya mwisho ya Kinyerezi itaendelea kufanyiwa kazi hadi itakapokuwa tayari kabisa.

Kukamilika kwa mitambo hiyo kutatuhakikishia jumla ya Megawati 305 zaidi ya umeme unaopatikana sasa na ndipo tutakaposema kwa uhakika kwamba tatizo la umeme nchini limemalizika. Hata hivyo kila mtambo mpya utakapokuwa unawashwa makali ya upungufu wa umeme yataendelea kupungua.

Ni muhimu pia Watanzania watuelewe kwamba kila kitu hakiko katika uwezo wetu. Hii ni kwa sababu baadhi ya Mitambo ya kuzalisha umeme na pia mifumo ya Gesi sio ya kwetu na inamilikiwa na watu wengine.

Hivyo taarifa tulizokuwa tunazipokea kutoka kwa Makampuni haya ndizo tumekuwa tukiwapatia wateja wetu na bahati mbaya baadhi yake hazikuwa kama tulivyokuwa tumeelezwa. Mbali na Mitambo ya TANESCO umeme unaopatikana kwa sasa unatoka kwa Makampuni ya Songas, Symbion, Aggreko na IPTL wakati mfumo wa Gesi unahusisha Makampuni ya Pan Africa Energy, TPDC na M&P.

Kwa namna moja au nyingine makampuni haya yana mchango mkubwa katika kuwezesha umeme kupatikana kwa muda kama inavyokuwa imepangwa.

Naomba niendelee kuwaomba Watanzania wenzangu kwamba tuendelee kuwa na subira wakati kazi hizi zinakamilishwa. TANESCO haina nia yo yote ya kuwatesa kwa kuwanyima umeme.

Ukweli ni kwamba tunajitahidi kadiri iwezekanavyo kuhakikisha kwamba mitambo yote inawashwa haraka iwezekanavyo na umeme wa uhakika unapatikana mapema iwezekanavyo.

Hata hivyo tusisahau hizi ni mashine na baadhi yake hazijawahi kuwashwa kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa sababu kulikuwa hakuna gesi, hivyo wakati mwingine zinapchukua muda mrefu zaidi kuweza kuwaka na hata marekebisho ya hapa na pale hivyo kuathiri ratiba zinazokuwa zimetolewa.

UVUMI KWAMBA MTAMBO WA KINYEREZI NI MCHAKAVU

Ukweli ni kwamba Mtambo wa Kinyerezi ni mpya, umetengenezwa na Kampuni kubwa na maarufu zaidi ya kutengeneza mitambo ya Gesi na Engine za ndege ya General Electric (GE), Unajengwa na Mkandarasi maarufu duniani Kampuni ya Jacobsen Elektro ya Norway na kazi zinasimamiwa na Kampuni maarufu ya Ushauri ya Lahmayer International ya Ujerumani bila kusahau kwamba TANESCO inawakilishwa na Wahandisi wazoefu na waliobobea.

Si kweli kwamba mtambo hauwaki ila hatua ya kuuwasha bado. Leo ndio kwanza wanaanza kupitisha gesi kwenye mabomba ya mtambo kwa msukumo mkubwa. Mtambo huo ni mpya na unakidhi vigezo vyote vya kitaalam.
Imetolewa na

OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI – TANESCO
4/10/2015


Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) limesema kuwa mgao wa umeme unaoendelea nchini umesababishwa na kushuka kwa uzalishaji wa umeme katika mabwawa ya maji kwa asilimia 81.3.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema leo jijini dar es Salaam kuwa uwezo wa juu wa mitambo yote ya kuzalisha umeme wa maji ni megawati 561, lakini kwa sasa uzalishaji wote wa umeme wa maji ni megawati 105 ambazo ni sawa na asilimia 18.7.

Kuhusu umeme wa gesi, Tanesco walisema kuwa uwezo wa kuzalisha umeme kupitia Kampuni ya Pan Africa ulishuka kutoka megawati 340 hadi kufikia megawati 260. Shirika hilo limesema kuwa Pan Africa wanaendelea kuviboresha visima vyake ili kuhakikisha gesi zaidi inapatikana.

"Mitambo ya kuzalisha umeme kwa gesi ya bomba jipya iliyokwisha washwa ni ya megawati 190 na leo tunatarajia kuongeza mwingine wa megawati 35. Mwezi Septemba tuliwasha mtambo mwingine wa megawati 20 ya gesi ya bomba la Songosongo na kufikisha umeme ulioongezeka kufikia megawati 110," walisema Tanesco.

Shirika hilo la umeme limesema kuwa mitambo mingine ya Symbion (Megawati 20), Ubungo II (Megawati 35), Songas (Megawati 20) na Kinyerezi (Megawati 70)inatarajiwa kuwashwa ndani ya wiki moja hadi mbili tangu sasa ili kukabiliana na tatizo la mgao.

Alisema uwezo wa uzalishaji umeme kwa mitambo ya mafuta ni megawati 230, lakini kwa sasa inazalisha megawati 190 tu.

Chanzo:
Mwananchi[/QUOTE]

Hizi ni baadhi ya thread zilizozungumzia Tatizo la umeme tanzania

Dar es Salaam yaghubikwa na giza kwa umeme kukatika katika


TANESCO, mgao huu una sababu gani tena?


Tanesco yatangaza mgawo wa umeme nchi nzima


Uongo wa TANESCO mwisho leo - September 14, 2015


Shirika la Umeme (TANESCO) limetangaza Nchi kuwa gizani kwa siku 7
 
Juzi kati waligundua makaa ya mawe wakasema ifikapo 2015 mgao wa umeme utakuwa ni ndoto Tz ila sasa sielewi kinachoendelea.
makaa yamechotwa na hayazungumziwi tena
 
Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa tanesco alituambia kwamba mgao wa umeme haupo tena lakini kila siku umeme unakatika na kakaa kimya, Magufuli ingia madarakani utusaidie kuondoa huu uozo maana hata waziri wa nishati na madini ni walewale tu hakuna kitu
 
Juzi kati waligundua makaa ya mawe wakasema ifikapo 2015 mgao wa umeme utakuwa ni ndoto Tz ila sasa sielewi kinachoendelea.
makaa yamechotwa na hayazungumziwi tena

hiyo ndio ccm ni kama kuku anapomuahidi mwanae kunyonya. wana gita jipya sasa na wafuata upepo wameanza kufuata mkumbo. labda umeme utapatikana 2115
 
Huku Arusha mgao was 10hrs ulianza tangu Jumanne. Mji mzima wa Arusha unakosa umeme bila maelezo
 
Uhalisia ni kwamba Tanzania tuna rasilimali za kutosha ila viongozi wa serikali hawana dhamira ya dhati ya kutukomboa wananchi kutoka katika hali ngumu ya maisha. mbaya zaidi wananchi wameridhika na hali ngumu ya maisha hivyo viongozi wanazidi kutafuna tu pesa bila kujali.
 
Tanesco ni vema wakawa wakweli, toka nifike Dodoma nashuhudia kukatika kulikoratibiwa kwa umeme, kati ya masaa 8-10. Kuna wenzetu ambao ni wajasiriamali wadogo inawaumiza sana, ni bora ratiba ya mgao ikawekwa wazi, huo ndio uwazi na uwajibikaji tunaoutarajia kwenye shirika letu la umma.
 
wameshindwa hao mbinu mbadala za kupata umeme zipo na matangazo yataendelea kama kawa.

People's power.
 
Nenda katoe taarifa customer care Kituo cha karibu, halafu Kwani hayo matangazo ya Live hao Star Tv na Itv hapo ground wanategemea umeme wa Tanesco tu? si wana standby Generator? Tutaona huku kwa niaba yenu kama kuna marekebisho ya Njia kuu za umeme waache kisa CDM inafanya mikutano acheni hizo!
 
Back
Top Bottom