Tanesco! Tanesco! Tanesco!

Mwanakili90

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,568
245
Salaam wanajF,

Neno tanesco limekua likitajwa sana Midomoni mwa watu kama lilivo neno "MAISHA MAGUMU''.

Ni vigumu kulifanya liondoke kwa mara moja,ila nashauri jambo moja,kama ilivokuwa kwa shirika la TTCL,lilikua na Nyodo na sumbufu kama Tanesco,lakini baada ya makampuni binafsi kuruhusiwa kutoa huduma iyo Leo hii TCCl ipo wapi?

My take:waruhusu makampuni binafsi yazalishe umeme ili Tuisahau Tanesco kama tulivyo isahau TCCL.
 
Mbona kuna IPTL,Symbion,Songas,Aggreko etc etc uzalishaji tayari umeruhusiwa...labda usambazaji... Walijaribu Artumas Mtwara na Lindi tena kwa kuuza beo ya TANESCO govt was giving them subsidy and it didn't work waliona ni hasara tu

Transmission pekee ndio inabaki mali ya serikali
 
Umemsikia ngeleje?????anasema wanasiasa wanajitafutia UMAARUFU kupitia suala la mgao.....anawaasa wananch wasiwasikilize wanasiasa.......mgao ni janga la KITAIFA
 
janga la kitaifa?? Mbna alisema ikifika mwez wa sita mwaka huu mgao utakua ni ndoto sasa amefuta kauli yake au ndo anazidisha siasa?
 
Mbona kuna IPTL,Symbion,Songas,Aggreko etc etc uzalishaji tayari umeruhusiwa...labda usambazaji... Walijaribu Artumas Mtwara na Lindi tena kwa kuuza beo ya TANESCO govt was giving them subsidy and it didn't work waliona ni hasara tu Transmission pekee ndio inabaki mali ya serikali
Wapewe uwezo wa kufanya kama makampuni ya simu,sasa IPTL hawana mamlaka ya kuuza moja kwa moja kw mtumiaji.
 
hivi hawa wasomi wa bongo walishindwa nini kuhimiza matumizi ya Solar energy mbadala wa Hydro energy? nadhani wangekuwa na uwezo wa kuona mbali wangehimiza watanzania wenye uwezo wa kuagiza mitambo hii wafanye hivyo. watuuzie kwa bei nzuri ambayo kwa matumizi ya nyumbani tungeweza. kuna watanzania wamejenga majumba yao ya bei mbaya wasingeshindwa kugharamia Solar Power. Huenda watanzania wasingekuwa wanategemea sana tanesco kuwasha taa, tv, pasi, redio, jiko, kama wangehimizwa kutumia Solar. Lakini ndio hivyo uwezo wetu wa kuona yajaya ni kama wa ile hadithi ya Kusadikika; kuwa kuna haja gani kujenga barabara ikiwa unyao wa mtu hauzidi inch sita?
 
Wapewe uwezo wa kufanya kama makampuni ya simu,sasa IPTL hawana mamlaka ya kuuza moja kwa moja kw mtumiaji.

Hahah..I can imagine the days of:
IPTL: Washa zote zote kwa bei nafuu kuanzia saa sita usiku mpaka majogoo!!!lol
Symbion nao waje na yao: Nunua umeme kwa robo shilingi kila utumiapo m-pesa...
damn...wat a future!!!
 
hivi hawa jamaa wanajua shida tunazozipata,mtu akisimama kusema ukweli utasikia anatafuata umaarufu wa kisiasa
hivi kwenye swala kama hili kuna umaarufu hapa hiki ni kitu ambacho hata kipofu lazima atakipinga haya za mwizi ni 40
 
Back
Top Bottom