Katika juhudi za kuboresha uchumi, upatikanaji wa nishati ni muhimu sana.
Ila kama pia usambazaji wa nishati utalega tunaweza tusipate matokeo tarajiwa.
Mimi ni mkazi wa Ukonga, Imepita miezi 6 tangu nimalize mchakato wote wa kupata umeme, yaani kufanya e/wiring kwangu, maombi, survey, wakatoa ripoti, inahitajika nguzo moja, wakanipa control number, nikalipia. Almost 600,000TSH. Tangia mwaka jana August nimekuwa nikifuatilia Gongo la Mboto mpaka kuonana na Meneja ili nijue tatizo kwa nini hawajaja kuunganisha umeme bila mafanikio, danadana nyingi, uongo uongo mwingi, mwisho nenda tutashughulikia na hawashughulikii.
Je, kwa hali hii, mtu kuunganishiwa umeme uliopita 105m kutoka kwake TANESCO inachukua zaidi ya miezi sita, uchumi wa kati tutatoboa kweli, hili kwa kweli ni swali kwa Waziri wa nishati.
Mimi nafikiri kuna umuhimu wa kulivunja hili shirika ili kuongeza ufanisi wa huduma za nishati au kuhusisha mashirika binafsi kwa kiwango kikubwa katika shughuli wanazoweza kufanya. Mfano: kwa sasa hatupati shida kwenye suala la kuunganishiwa mawasiliano ya simu kwa sababu TTCL wana washindani, ila kipindi wakiwa wenyewe walikuwa na ukiritimba mwingi kama huu wa TANESCO
Kuna harufu kubwa ya rushwa hapa, hasa hapa branch la TANESCO Gongo la Mboto, watu wanacheleweshewa huduma kwa makusudi ili waingie mfukoni kutoa rushwa, Nashauri PCCB wamulike eneo hili.
TANESCO wafanye kazi zao, kwa nini nilipe laki sita kuunganishiwa umeme na nisubiri zaidi ya miezi 6, hiyo fedha ningekuwa nimeitumia kwa biashara ningekuwa na bakaa fulani ya kunitoa mwaka 2021, kuna umuhimu wa kuwa na mkataba kwa wateja, yaani ndani ya muda gani mteja atakuwa ameunganishiwa umeme, iwapo watavuka muda huo kuwe na hatua madhubuti za kumlinda mteja kwa uonevu huo.