TANESCO umeme kukatika kila siku imekuaje? Yaani kazi zetu zinalala hatuingizi kipato kisa nyie kushindwa kusimamia majukuku yenu ipasavyo.

Nimevumilia sasa inatosha. Ni lisaa la tatu umeme haupo kazi zimesimama. Mnategemea tunaishije? Acheni mambo yenu turudishieni umeme.
 
Wakuu Kuna aliyewahi kuomba namba za cmu humu na tanesco akasaidiwa??
Eleza ululivyosaidiwa
 
Taarifa Kama hizi nimetuma inbox ZAIDI ya Mara tatu na Mara ya mwisho ilikuwa 14/10/2020 na hakuna mrejesho
 
Ningependa kujua kutoka kwenu TANESCO

Mnalichukuliaje suala la umeme kukatika masaa zaidi ya matano na mstakabali wa uchumi?
Hivi tukiwaita nyie ni wahujumu uchumi wa taifa hili na wanachi wake tutakua tunakosea?
Hivi najua ni hasara kiasi gani tunazipata kila mnapokata umeme?

Yaani imekua kama desturi kwa umeme kukatika maeneo haya Tabata. Ni kwamba hamna wataalamu wenye kutatua changamoto kwa muda mrefu au shida ni nini?

Hivi hamjui kama mnakwamisha maendeleo?
 
Hata huku mkuranga umeme unakatika siku nzima na sio mara moja ila hawaishi kujigamba kuzarisha umeme mwingi
 
Ningependa kujua kutoka kwenu TANESCO

Mnalichukuliaje suala la umeme kukatika masaa zaidi ya matano na mstakabali wa uchumi?
Hivi tukiwaita nyie ni wahujumu uchumi wa taifa hili na wanachi wake tutakua tunakosea?
Hivi najua ni hasara kiasi gani tunazipata kila mnapokata umeme?

Yaani imekua kama desturi kwa umeme kukatika maeneo haya Tabata. Ni kwamba hamna wataalamu wenye kutatua changamoto kwa muda mrefu au shida ni nini?

Hivi hamjui kama mnakwamisha maendeleo?
Je ni eneo gani?

Wilaya

Namba ya simu
 
Kero yangu watu wa kitengo cha survey Moshi mjini wamekua wanakwamisha juhudi za mh rais niliomba kuunganishiwa umeme sasa ni mwaka unakwenda nomesota sana kufungua malalamiko mwisho wa siku nimeaambiwa hawana usafiri siku ukiwepo watanistua kwaiyo nimekata tamaa baada ya kupoteza mda mwingi nafkiri mnahitaji washindani ili mfanye kazi kwa ueledi pia naomba msaada wenu kwa hili
 
Tunaomba kupata taarifa zako zaidi ikiweka
Jina
Eneo
Simu
 
Kwema, Umeme hamna huku Moshi giza tupu. Mimi nilidhani mgao wa umeme umeisha lakini naona hili jinamizi bado tunalo huku Moshi pamoja na juhudi zote hizo bado naona kautaratibu ambako siyo kazuri.

Hii imekuwa ni mtindo kujirudia. Kama kuna lo lite lile si tuambizane. Mbona tulikuwa pazuri tu. Au mpaka tupigiane makelele na kuumbuana. Tusirudishane katika kipindi cha enzi za ugima. Tupeane taarifa. Mishahara si mnalipwa tena mimono tu.
 
Tunaomba kupata taarifa zako zaidi ikiweka
Jina
Eneo
Simu
Huku Moshi kuna tatizo gani, umeme unakatwa mara kwa mara kea muda mrefu na utaratibu unajirudia bila hata taarifa kama kuna uwezekano.
Leo tangu saa kumi na mbili hakuna umeme hadi sasa saa 4.22
 
Nina malalamiko makubwa la kwanza na kuhusu uombaji wanguzo za umeme ,,,maana tume toa taarifa kuhusu kubadilishiwa kwa nguzo ya umeme maeneo ya hapa kwetu (Mbezi Mtoni ,fremu sita )nguzo imeoza mpaka basi tumetoa taatifa ta kubadilishiwa nguzo wanasema kuwa tutakuja kushughulikia mpaka sasa nguzo imeinamaa na inaweza kusababisha madhala makubwa kwa watu ..na waomba sana Tanesco mnisaidie...(Kinondon Kaskazin)
 
Back
Top Bottom