TAMKO LA UVCCM na Mwelekeo wa Kisiasa Nchini

Nashindwa kuwaelewa ma-strategists wa chama kikongwe CCM, inakuwaje wameacha chama chao kuwa kwenye defensive for this long? Who is running that party as of now? Na hii yote ni kutokana na ile dhambi ya kutokuukubali ukweli!
 
Mbona wana matusi hivo?
Huyo shigela Dr.Slaa alimchukulia mamake au?
Ndo umoja wa vijana walio "rukwa" akili wa ccm hao kutukana watu ambao ni sawa na wazazi wao?
Au ndo malezi ndani ya chama chao cha mauaji?

...Wao na tamko lao lote wapuuzi tu
Mtu mnafiki ni mbaya kuliko unayejua kuwa ni adui yako. Ni aheri Rostam kuliko kuliko hawa UVCCM maana huyu tunajua ni adui wa kila mtanzania mnyonge. Viongozi wote wa UVCCM wapo TISS, na hii TISS ndiyo iliyoharibu uchaguzi mkuu wa 2010. UVCCM inaendeshwa kwa ufadhili wa mafisaidi, halafu leo wapinge ufisadi?

Nia yao kubwa ilikuwa ni kumshambulia DR Slaa, CHADEMA, Sita na Mwakyembe, na maaskofu. Mengine wameyaongezea ili kuokota watu wenye akili nyepesi waamini kuwa UVCCM sasa imebadilika, na inapigania maslahi ya Taifa. UVCCM miaka yote imekuwa ni taasisi ya kufifisha akili za vijana (brain wash), kuandaa watu ambao watakubali kila jambo la CCM ikiwa pamoja na wizi na dhuluma ya CCM kwa wananchi, ndiyo maana hata hapa wanazungumzia uwajibikaji wa pamoja wa Mawaziri licha ya kwamba maamuzi ya kuilipa Dowans hayakupitishwa na Baraza la mawaziri.
Tujihadhari sana na UVCCM na jumuia nyingine zote za CCM, hawa hawana tofauti yoyote na CCM. Mtu yeyote mwadilifu kabisa kabisa, shujaa, asiye mnafiki, asiye mchumia tumbo, anayelipenda Taifa lake na watu wake, kamwe hawezi kabisa kuwepo kwenye CCM ya leo maana yanayofanyika huko hayawezi kuvumiliwa kabisa na mtu mwadilifu. Ni vigumu sana kumwona mtu mzalendo ndani ya CCM au jumuia zake, hawa ni watu ambao huangalia maslahi ya chama chao na siyo Taifa, na maslahi yao makubwa ni kufanya chochote wanachoweza ili kuendelea kutawala. Tutumie tamko lao kuongeza nguvu ya kudai mabadiliko na kuondoa ugandamizaji na mauaji ya CCM dhidi ya watu wasio na makosa maeneo mbalimbali ya Tanzania.
 
statement ya uvccm kisiasa sio mbaya ni nzuri ila wamekosea sana kutumia jazba kwenye suala la chadema.....kama institution hawakutakiwa kutumia lugha ya mitaani,kihuni na matusi ...dhidi ya chadema na slaa wao......maana watasababisha watu wahame kujadili katiba na dowans waingie kujibu tuhuma personal za dr slaa especially kama chadema nao wataamua kumshambulia rais kikwete kwenye mambo yake binafsi...tutahama kabisa kwenye mijadala ya kitaifa!

Na nilikuwa nasoma kuhusu mtu fulani anashauri Chadema vijana(BAVICHA) Lijibu tamko hili.

Ila ushauri wangu ni kuwa watakapo jibu wakae kwenye mstari wa mambo ya msingi kwa sasa,waachane na hizi shutuma za Dr. Slaa kuhusu mambo binafsi kana kufukuzwa kanisani,ndoa n.k. maana ni mbinu ya kisiasa kubadili topic na focus ya watu .

Ni bora tuka focus na kujadili mambo ya msingi kama Dowans na mengineo...watanzania wengi kwa sasa they dont care kuhusu kashfa binafsi ya mtu iwe kweli au uongo..wako concern kupanda kwa gharama za umeme zinazosababishwa na Dowans ,wako concern na kupanda kwa gharama za maisha wakati mishahara haitosholezi still tunataka kulipa watu haraka haraka ...wanafunzi hawapewi mikopo kwa wakati ,bajeti ya mbolea inapotelea kwao wenyewe bils.
Watu wanataka katiba mpya itakayoweza kumwezesha kufanya viongozi kutawala kwa mujibu ya mahitaji ya watanzania.

So tusihame kujadili mambo muhimu ya nchi tushauri na viongozi wetu...
 
Tamko limejaa unafiki, halafu kwenye tamko mara wanamzungumzia Slaa na kuchukua mke wa mtu ukiona watu kuishiwa cha kuongea ndio hao sasa hawana lolote zaidi ya unafiki na kejeli
 
Hopelessness and misdirection...
Nahisi hawa UVCCM wanatumiwa na wanaume fulani.
Huu ni Uzabizabina...hawaako serious...Huwezi kuongea mambo serious na kisha ukayafunika yote na habari za kikekike na za udaku!
Dr Slaa alishitakiwa mahakamani kwa suala la mke, na kwa kawaida kama kesi iko mahakamani, hawa wapuuzi wataibukaje na kauli za kipuuzi kabla ya hukumu?...hii ni prejudice...nisawa na kuandaa chakula kizuri sana , LAKINI kukiandalia CHOONI!..wadda'Mess!
 
Na nilikuwa nasoma kuhusu mtu fulani anashauri Chadema vijana(BAVICHA) Lijibu tamko hili.

Ila ushauri wangu ni kuwa watakapo jibu wakae kwenye mstari wa mambo ya msingi kwa sasa,waachane na hizi shutuma za Dr. Slaa kuhusu mambo binafsi kana kufukuzwa kanisani,ndoa n.k. maana ni mbinu ya kisiasa kubadili topic na focus ya watu .

Ni bora tuka focus na kujadili mambo ya msingi kama Dowans na mengineo...watanzania wengi kwa sasa they dont care kuhusu kashfa binafsi ya mtu iwe kweli au uongo..wako concern kupanda kwa gharama za umeme zinazosababishwa na Dowans ,wako concern na kupanda kwa gharama za maisha wakati mishahara haitosholezi still tunataka kulipa watu haraka haraka ...wanafunzi hawapewi mikopo kwa wakati ,bajeti ya mbolea inapotelea kwao wenyewe bils.
Watu wanataka katiba mpya itakayoweza kumwezesha kufanya viongozi kutawala kwa mujibu ya mahitaji ya watanzania.

So tusihame kujadili mambo muhimu ya nchi tushauri na viongozi wetu...

Nakubali, pia nina wasiwasi EL ana mkono kwenye hili tamko, mbona hawa vijana wamekazania issue irudi mjengoni? nadhani wanataka Lowasa akasafishwe na akina mwakyembe wawe macho na itabidi hata yale ambayo hawakuyasema kwa hofu ya usalama wa taifa wayaseme tujue mbivu na mbichi.
 
Kwani walipokuwa wanapiga kampeni hawakujua hela zilizokopwa hazina zitarudishwaje?
 
Hapo DOWANS imetumiwa kama pazia kuficha jambo fulani. Kwa kuangalia kwa undani lengo ilikuwa kumtukana Dr. Slaa na CHADEMA kwa ujumla na kutaka akina Dr. Mwakyembe na wenzake ndani ya CCM wabanwe zaidi. Hata uandishi wake unaonekana kama uliofanywa na watu ambao sio makini na waliosoma nia kama wametumwa kufanya hilo kwa interest ya kikundi fulani na umoja huo.
 
Nini nafasi ya UVCCM katika uongozi wa Taifa - Kikatiba?

Sijui kama hawa vijana walikuwa hawajapata mvinyo kabla ya kukutana na waandishi? Walikuwa wanapayuka!
 
kama hao ndio viongozi wa UVCCM wametoa hilo tamko.... na wanasema walikaa kimya muda mrefu wakitafakari! kazi ipo!!!!
 
Itakuwaje na BAVICHA wakitoa tamko linalozungumzia zaidi maisha binafsi ya JK au viongozi wao wengine, Kuna atakayesalimika kweli?
 
hawa UVCCM wamefikia hatua hii,kumtukana Dr Slaa,ana kosa gani, leo hii walitakiwa wamsifie kwa kua wamegundua wanaibiwa mchana. hivi huyu mzee alikosea kuwafumbua macho, hivi hawa ni vijana gani ambao akili zao zimelala kiasi hiki,wana busara gani kutoa matusi kiasi hiki mbele ya jamii, baba zao na mama zao wawakemee na waliombe taifa radhi.
 
Hawa watu wapuuzi kweli.. sisi tumeyasema ya bodi ya mikopo miaka mitatu iliyopita wao walikuwa wapi? Hilo la Dowans kwanza inaonekana hata hawalielewi kabisa.

Wao na wakubwa wao ni fire fighter na siyo fire preventer!
Ndivyo walivyo
 
nyie UVCCM acheni kifuatilia maisha binafsi ya watu nyie ni vijana mnapaswa kufuatilia utendaji wa viongozi na si maisha ya familia zao hivi na vyama vingine vikiamua viwaseme baba zenu hivi watasalimika,mbona vijana wa CHADEMA,CUF etc hawafanyi hivyo,sitaki kuamini kama vijana kama nyie mnaweza kutoa tamko kama hili isipokua kuhusu Dowans kidogo mmeonyesha umakini
 
Back
Top Bottom