Tamko la Mbowe mwenyekiti Chadema Taifa la kulitafakari

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898
images

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Freemaan Mbowe
amesema kamwe haongozi kundi au genge la wasaka vyeo na madaraka
ndani ya chama chake bali anaongoza kundi la watu wanaopenda mabadiliko.

Kiongozi huyo amesema binafsi hawezi kwa sasa kusema atagombea
Urais au Ubunge kwa sababu huu si muda wake hata kidogo.

Mbowe amesema mwanachama yeyote makini wa CDM kwa sasa
ni muda wa kuwaunganisha wanachama na watanzania kwa ujumla
na wala si muda wa kuwagawa kukimbilia madaraka.

Kiongozi huyo amesema ndiyo maana makamanda wote
wakiongozwa na Dr Slaa wamejichimbia vijijini
kwa kazi moja tu ya kueneza vuguvugu la mabadiliko-M4C
 
...Mkuu candidscope hii si JF where we dare to talk openly!? au siku hizi imebadilishwa!?
A%20S-coffee.gif

Kuna wakati tujadili kama wanataaluma ambao hujikita katika kujadili mada badala ya watu. Tukiendekeza kujadili zaidi nafsi hoja hukosa uzito stahiki na kukuta tunaelekeza nguvu kumjadili zaidi mtu. Hii ni kasoro ambayo JF tunahitaji kukua na kupanda ngazi ya juu zaidi katika kujadili mada.
 
...Nimekuelewa Mkuu.

Sijawahi kumsikia Mbowe akiongea ujinga hata siku moja. huyu ni Mwenyekiti kweli na anajuwa ni nini maana ya uongozi.

Nakubaliana nawe, huyu mwenyekiti wa Chadema taifa ana hulka ya uongozi na busara pengine kupita wanaomtangulia kwa umri. Kauli kama hiyo inatakiwa kutamkwa na kiogozi ili kutoa picha ya kinachotakiwa kufanyika na chama katika harakati za kuongoza mabadiliko nchini.

Njia mbili zaweza kumpasua mtu msamba (samahani kwa nililotamka), kwa sababu mshika mawili moja humponyoka.

Wazungu wanasema, fanya kitu kimoja kwa wakati, kikishakamilika anza kinachofuata. Waafrika tuna hulka ya kufanya karibu yote yatujiayo kichwani kwa wakati moja na kwa pupa, matokeo yake ni hakuna linalokamilika. Bora moja likamilike kuliko yote kutokamilika. Nafikiri Mwenyekiti anamaanisha hivyo kwamba nguvu zielekezwe kukijenga chama kwa sasa badala ya kulegeza nguvu kukijenga chama na kuanza mambo mengine ambayo si muda mwafaka kwa sasa.
 
...Mie naunga mkono kauli ya Mbowe na imetolewa wakati muafaka. Mambo muhimu ya kukikuza chama yapewe kipaumbele kwa sasa ambapo bado kuna miaka mitatu kabla ya uchaguzi Mkuu.

Wale wote wanaotaka kugombea nafasi zozote za uongozi kupitia CDM basi wafanye hivyo kupitia vikao maalum vya chama badala ya kuropokaropoka bila mpangilio na hivyo kuharibu mshikamano uliopo ndani ya CDM.
 
images

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Freemaan Mbowe
amesema kamwe haongozi kundi au genge la wasaka vyeo na madaraka
ndani ya chama chake bali anaongoza kundi la watu wanaopenda mabadiliko.

Kiongozi huyo amesema binafsi hawezi kwa sasa kusema atagombea
Urais au Ubunge kwa sababu huu si muda wake hata kidogo.

Mbowe amesema mwanachama yeyote makini wa CDM kwa sasa
ni muda wa kuwaunganisha wanachama na watanzania kwa ujumla
na wala si muda wa kuwagawa kukimbilia madaraka.

Kiongozi huyo amesema ndiyo maana makamanda wote
wakiongozwa na Dr Slaa wamejichimbia vijijini
kwa kazi moja tu ya kueneza vuguvugu la mabadiliko-M4C

Candid indeed! Hakuna ubaya kupasua haka kajipu mapema.
 
Nakuunga mkono hoja yako, kwani kauli ya Mwenyekiti isipotiliwa maanani, tutakuwa watu tunahangaikia zaidi kufanya kampeni za urais, ubunge na mengineyo wakati muda haujawadia na hivyo kudhoofisha nguvu ya kukijenga chama matawili kwa nguvu moja, ambako ndiko kwenye chimbuko kubwa la wapiga kura. Tunajua wazi kwenye miji mingi Chadema imeshashika usukani, lakini nguvu ya mijini haimtoi nyoka pangoni. Vijijini ndiko kwenye asilimia kubwa ya wapiga kura, kwani mijini wapo mashabiki ambayo hawajiandikishi kupiga kura. Ukiona umati kijijini wamekukubali, ujue nusu au robotatu yao watakupa kura, lakini mijini umati wote ule utakachoambulia pengine ni chini ya robo tu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Candid indeed! Hakuna ubaya kupasua haka kajipu mapema.

Highlander shukrani kwama utajaribu kutufafanulia, lakini tunachoomba hapa tujitahidi sana kuijadili mada yenyewe zaisi ili kuitafakari na kuufikisha ujumbe wa Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa jamii ya wapenda mabadiliko.
 
Mkuu Candid Scope sisi ambao tumeijua CDM tangu inazaliwa tunazo sababu za kukubali kuwa kuna watu wengi wameweka mchango mkubwa kukikuza chama. Tatizo ambalo nadhani Kamanda Mbowe anajaribu kuliaddress kwa ujasiri ni kukemea ambition ambazo pengine zinapingana na strategy za chama.

Nimetumia neno ujasiri kwa sababu huenda anakemea watu au mtu ambaye anao mchango mkubwa katika kujenga na kukuza chama.

Unahitaji ujasiri kukemea mtoto ambaye ukweli unampenda.
 
Nakubaliana nawe kuwa tamko hilo linaweza kutafsiriwa kwa namna mbalimbali ambayo kila mmoja navyofikiria. Lakini kwa upande wangu naliona kama ni tamko linalowaasa wanachama na viongozi kwa sasa kushikamana katika jambo moja la kukiimarisha chama, maana mambo mawili kwa wakati mmoja ni vigumu na pengine ni kitu kinachoweza kusababisha ufa katika utendaji wao wa kila siku.

Wakati wengine wanahaha kukifikicha chama vijiji na kukazana kuwaelimisha wananchi wafunguke kuhusu kuifahamu maana ya demokrasia na wajibu wa viongozi kwa wananchi, ni kitu kitakacholeta mgongano kama baadhi wakianza shughuli ambazo ni za ratiba ya mwaka 2015, ambazo kwa sasa hazina msingi kwa maana ya kwamba zikiendekezwa, basi kila mmoja ataanza kuhangaikia uchaguzi na kile kilichokusudia kueneza vuguvugu la mabadiliko kukosa msukumo na nguvu ya pamoja kwa sababu ya kutofautiana malengo wawapo katika uwanja wa mapambano.

Hatuna maana waasisi wa chama kuwaweka kando au kutojali mchango wao, ila tunachotazamia kwamba pamoja na juhudi kubwa walizofanya, bado kazi ipo kwao kuongeza ushirikiano na mshikamano katika kueneza vuguvugu la mabadiliko nchini.

Kwa wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali baadaye, utendaji wao wa kila siku chamani na katika uwanja wa kuendesha vuguvugu la mabadiliko ni mwango utakaowasaidia katika kujitangaza kuliko kuelekeza nguvu sasa hivi ni mapema mno.
 
Maeneo yenye red yanaonesha dhahiri tunawaza sawa mkuu. Labda tu niongeze kuwa anapotokea mwanachama, ama wanachama wakaanzisha agenda mpya, nje ya agenda iliyopo mbele kwa utekelezaji, hili linaweza kutafsiriwa mkakati wa detraction na tafsiri hii ikawa na mashiko. Tatizo ni kwamba detraction hiyo ikikemewa inaweza kuleta ugomvi, na ni hapo ambapo sasa unahitaji ujasiri kuendelea na ukemeaji anyway! Which is what Mbowe has done rightly.
 
Uko juu katika uchambuzi na mwono, ndio maana napenda mtu kama wewe tunaweza kujadili mada kama zilivyo na kuangalia kwa upana na urefu wake advantages & disadvantages kwa chama na wananchi.

Copy kwa dudus, Lunyungu, Lukansola, Magesi, DIALLO,
 
images

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Freemaan Mbowe
amesema kamwe haongozi kundi au genge la wasaka vyeo na madaraka
ndani ya chama chake bali anaongoza kundi la watu wanaopenda mabadiliko.

Kiongozi huyo amesema binafsi hawezi kwa sasa kusema atagombea
Urais au Ubunge kwa sababu huu si muda wake hata kidogo.

Mbowe amesema mwanachama yeyote makini wa CDM kwa sasa
ni muda wa kuwaunganisha wanachama na watanzania kwa ujumla
na wala si muda wa kuwagawa kukimbilia madaraka.

Kiongozi huyo amesema ndiyo maana makamanda wote
wakiongozwa na Dr Slaa wamejichimbia vijijini
kwa kazi moja tu ya kueneza vuguvugu la mabadiliko-M4C

Mwenyekiti asiishie hapo.Kuna haja ya kurejea Katiba ya chama Ibara ya 9.2 KANUNI NA MAADILI YA CHAMA hasa kipengele cha
9.2.5
''Kamati Kuu itatunga Maadili ya kuongoza Nidhamu,Utii na uwajibikaji na dhamira ya watendaji Viongozi wa Chama na wanachama kwa ujumla. Hii ni pamoja na maadili ya Mwenendo katika Vikao vya Chama''

Hivyo basi kama Kamati Kuu haijafanya kazi hiyo nashauri ianze mara moja na ipanue wigo wa Kanuni hii hata kwa masuala ya huko mbeleni kama haya ya Ugombeaji nafasi mbali mbali ya uongozi nje ya Muda unaotambulikana kwa mgombea kutangaza kushiriki pamoja na madai ya uhuru binafsi masuala mengine lazima yaweze kulindwa kwa ajili ya ustawi wa chama na si masilahi binafsi kwanza.
 
Mbowe akalipe deni lake msajili kwa ajili ya disco lake lile la kupotosha vijana . BILICANAS. duh ikija kutokea ndio mbowe akawa rais . Yaani rais anamiliki dangulo.
 
its a spin

waweza kuta zitto anatumwa vilevile kudilute siasa za NEC ya ccm

Please, tujadili mada ilivyo yenyewe bila majina, nashukuru kwa mchango wako, ila ningependa mada hii tuijadili kwa uzito stahiki kuangalia advantage na disadvantage kwa Chadema.

Watu tumeshawajadili sana, siona kama itasaidia kwani kama kusikia na kusoma wamefanya. Kwa sasa tuijadili falsafa hii ya Mwenyekiti Mbowe.
 
Back
Top Bottom