CHADEMA
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 488
- 2,469
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa masikitiko taarifa ya kusimamishwa kiholela kufanya kazi za uwakili iliyomkumba Wakili Mwandamizi Mheshimiwa Mpale Mpoki ambaye alikuwa akiongoza jopo la Mawakili wa utetezi katika shauri la kinidhamu linalomkabili Wakili Boniface Mwabukusi mbele ya Kamati ya Maadili ya Mawakili iliyoketi tarehe 20 Novemba, 2023 katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi, Dar –es- Salaam mbele ya Mheshimiwa Ntemi Kilekamajenga, Jaji- Mwenyekiti wa Kamati.
Aidha, Chama kimeshtushwa na kinalaani mikakati inayoashiria nia ovu ya Serikali kupitia kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na sasa imedhihirika kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Mawakili na kupitia baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu kwa nyakati tofauti kuendeleza vitisho dhidi ya mawakili wanaotumia haki yao ya kikatiba ya kutoa huduma ya uwakilishi Mahakamani na wakati mwingine kutoa maoni mbadala, kutishiwa kuondolewa katika orodha ya Mawakili Tanzania.
Kama Chama, Tunaamini hili sio tishio tu dhidi ya Wakili, Boniface Mwabukusi au Wakili Mpale Mpoki na Jopo lake lote, bali ni tishio dhidi ya taaluma ya Sheria na Mawakili wote nchini na tishio dhidi ya vyombo vya utoaji haki nchini. Tunafahamu kwamba njama hizi zilianza na kuondoa Uwakili wa Wakili Fatma Karume ambaye Mpaka sasa hajarudishiwa Uwakili wake, Wakili Edson Kilatu, Wakili Jebra Kambole na Mawakili Wengine ambao wameshitakiwa kwa nyakati tofauti ili kuwatisha Mawakili wawe wanaiabudu serikali hata pale ambapo inakiuka utawala wa Sheria. Ikumbukwe kwamba Tanzania imeridhia mikataba na matamko mbalimbali ya Kimataifa ikiwemo Tamko la Umoja wa Mataifa la tarehe 7 Septemba, 1990 Mjini Havana, Cuba ambalo liliweka sharti kwa mamlaka za Serikali kuwalinda Mawakili dhidi tishio lolote la kiusalama wanapotimiza wajibu wao.
Chama kinamtaka Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Mawakili Mheshimiwa Ntemi Kilekamajenga, Jaji kuwajibika kwa kujiondoa katika nafasi yake ya Uenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Mawakili ili kuruhusu Jaji mwingine kuendelea kusikiliza shauri husika. Pili, kinawashauri Mawakili wote Tanzania na Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) kutumia vikao vyake vya kikatiba na kama Maafisa wa Mahakama kwa mujibu wa Sheria ya Mawakili, kuchukua hatua za dharura kuhami wanachama wao wanaoonewa na Serikali na kuhakikisha kwamba uamuzi wa Jaji Ntemi Kilekamajenga unafutwa kwa mujibu wa Sheria za nchi yetu.
Tunasisitiza kwamba, Mahakama inatakiwa kuwa sehemu ya kutoa haki bila upendeleo wala kuonea watu ili jamii inapoonewa iwe na imani kuwa wakikimbilia Mahakamani watapata haki bila kujali aliyeonewa kaonewa na Mtu au taasisi gani.
Imetolewa leo Jumanne tarehe 21 Novemba, 2023
John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya NjeView attachment 2820990