Tamko la Kamati Kuu ya Chadema: Jan 31 Jan, 2011

Wametoa tamko kuhusu matokeo ya form four pia. Wataunda kamati ya / tume ambayo. Itatoa report kufikia mwezi wa tano.
Katiba mpya mchakato uanzie bungeni .

Nimeipenda hii kwa kweli jamani. Yaani ni kama vile Chadema wanaongoza nchi vile. Waliosababisha hili janga la kitaifa (Matokeo ya Form IV) wako kimya kabisa kwenye viyoyozi as if haliwahusu. Tuliwaeleza kuhusu tatizo la shule za kata wakatuona wapuuzi na kutuita photocopy sasa matokeo yamewaumbua kwa kuwaonesha kuwa wao ndio photocopy.

Nakumbuka mgombea wao wa "urahisi" alikariri mpaka figure ya wanafunzi wa sekondari kwenye lile igizo la mdahalo ikulu. Kwake yeye siku zote namba ni muhimu kuliko quality. Sasa hizi zero karibu laki moja na nusu anazipeleka wapi? Angalizo please msitupelekee Division 4 high school, ni heri hayo madarasa yabaki wazi na hao walimu wa high school wakafundishe O level.
 
CUF walikataa mwanzoni kuungana na CHADEMA,ikiamini kuwa kambi ndogo ya upinzani itakubalika kisheria.Ukiachilikia mbali sababu ya CUF kuwa kitu kimoja na CCM bado inaonekana wazi kwamba CUF na CHADEMA hawawezi kuungana kwanini interest zao ni tofauti,shida nyingine ni pale NCCR,TLP na UDP ilivyotekwa na CUF mwanzoni tu baada ya uchaguzi inawafanya CHADEMA isiwe na imani na hivyo vyama vingine.Hivyo maamuzi ya CHADEMA ni sawa.
 
Hili jambo linatumika vibaya na hawa watu CCM kudai kuwa kuna udini hasa wakati wa uchaguzi 2010.

Mbona mwaka 2005 wakati KIKWETE alipochaguliwa na CCM kugombea MASKOFU na baadhi ya Mapadre walisikika wakisema wazi wazi kuwa KIKWETE NI CHAGUO LA MUNGU,wala hakuna shehe hata mmoja aliyepinga kauli hizo au Mtu yeyote kati ya wale wagombea kuomba likemewe hilo maana ni la udini?

Imekuaje leo hao hao watu wa dini wanapotoa maoni yao wakati na baada ya uchaguzi wa 2010 inakuwa inatafsiriwa ni udini?

CCM semeni ukweli kuwa nchi inapelekwa ku-baya.Wacheni kelele za udini pigeni kelele za kujenga nchi.
 
Samahani wandugu,

Mi huwa nashangaa, hivi hawa watu wanaoamini (wanaosema) kuwa Slaa katumwa na kanisa/katoliki ina maana huwa wanaamini kweli au wanataka tu kuchafua hali ya hewa? Hebu tujifunze kuchagua maadui jamani.

Kwa haraka bila hata kufanya uchunguzi wa kina, shida yetu kubwa ni umasikini wa kujitakia, viongozi wasio na utu, (Bila kutujali wanyonge na dini zetu) maamuzi yasiyofaa ya viongozi, kudanganywa mara nyingi sana viongozi wetu, mifumo ya uongozi ambayo haisukumi kuwajibika viongozi. Watu wenye uchu jamani hawana dini, hata angekuwa shehe au padri, alhaji au askofu, wakishaanza tu uchu na wizi, basi sio mwenzenu tenaaaaa.

Kuna ile hadithi ya fisi wawili na sungura:
Hapo zamani fisi wawili waiokota pande la mkate mkubwa wakakubaliana wagawane. Basi mmoja wao akaumega ule mkate ila ukaonekana umezidi kidogo upande mmoja, ili kupata muafaka watatue vipi tatizo la kugawiana bila kuoneana wakamwita sungura aje awasaidie, basi sungura akawasikiliza weeeeeee, akavichukua vile vipande viwili akauliza kipi kikubwa? Wakajibu wote hicho mkono wa kushoto, Sungura akangata kile kipande kikubwa kikapungua, akauliza tena sasa je vimekuwa sawa au kipi kikubwa? Wakajibu kwa pamoja kabisa, hicho mkono wa kulia, Sungura akakingata kile kipande kikubwa kikapungua, basi ndo ikawa hivyo, kila kipande kikingatwa kinapungua zaidi, inabidi kungwatwe kingine ili kikaribie kile kidogo.

Hatimaye vikabaki vitonge viwili ambavyo havilingani vilevile, ndio wale jamaa wakapata fahamu wakamuambia sungura awaache wajiamulie mambo yao wenyewe,


Jamani hawa wanaokuwa huko juu haijalishi ni wa dini gani, hawafai kuwaamini na mali yetu, tupange sisi, hata tukipunjana kidogo, si neno kama akishiba mmoja.

Alivyokuwa Mkapa na Nyerere tulilalamika sana, anapendelea wakristu, wakiwa Mwinyi na Kikwete wanapendelea waislamu, bora tuwafunge wote/yeyote anayekuja ashindwe kufanya nje ya tunayomtuma.
 
uamuzi wa chadema ni upo sawa kabisa. wanaharakati tunahitaji upinzani wa vyama zaidi kuliko muungano,kwani huu ndio utapelekea uwazi na ukweli kwenye kuendesha taifa letu bila kuoneana haya!

angalieni sana hao cuf sasa hivi huku zanzibar,nadhani mmeona wafanyabiashara wadogo walivovunjiwa viduka vyao bila kupewa mpango endelevu..yupo wapi mtetezi wa mwanachi? wizarani mishahara midogo,maisha magumu...mtetezi wenu ni nani? ni yule anayekubana uwahi kazini,usipite mtaa wa pili ukatafute centi 2 kwani mshahara wako haukutoshi?

huku bara ni kheri tuna wapinzani wa ukweli CHADEMA kwani bado wanaweza kuona kuwa umeme,gas vimepanda wakatetea na kuleta mabadiliko.

"ni afadhali kuwa baridi au moto na sio vuguvugu"
 
Tatizo la watu mnaotaka muungano wa kiinimacho wa wapinzani hamtaki kujibu maswali magumu! Liberal walipoungana na Conservative inafananaje na CHADEMA kuungana na CUF??? ktk muungano huo wa Waingereza Ccm ni ipi hapo?! Taja vyama vitatu Uingereza vyenye muungano wa ajabu kama mnaotaka uwepo hapa Tz... halafu wabunge wazalendo wa kweli wanatakiwa wawe kwenye baraza la mawaziri kivuli au wapiganie hoja zenye maslahi kwa raia wa Tanzania??! Hivi bunge lililopita kina Mwakyembe walikuwa mawaziri vivuli? Kumbukeni raia wengi hatuko kwenye vyama vyenu hivi vya siasa...

Natumaini hujanipata, muungano wa vyam vya upinzani si ule wa TANU na ASP = CCM, au serikali ya kitaifa CUF+CCM la! Kinachotakwa ni makubaliano ya ku-support miswada na misimamo ya kibunge. Tatizo watanzania wanadhani kufanyakazi pamoja kwa malengo fulani ni kukiuza chama. Haya ndio matokeo ya siasa za muda mrefu za CCM. The winner takes it all! Napozungumzia Conservatives na Liberal ninamaana ya mirengo miwili toufati ambayo kimtazamo ni vigumu kufanya siasa moja lakini kwa ajili ya malengo wamekubali kuunda serikali moja huko UK.
 
chama cha siasa kina imani, itikadi, falsafa, na uongozi yakinifu. Kila raia mwenye akili timamu anakuwa mwanachama wa chama husika baada ya kukubaliana na sera kanuni, katiba na mwongozo wa chama husika. Ni uhayawani kuamini lazima vyama viungane wakati vina taratibu malengo na nia tofauti kuleta utawala wa sheria haki na maendeleo. Ikumbukwe hata ccm ni chama cha siasa na kina wafuasi ambao wanakubaliana na yote yanayotokea na kutendwa chini ya katiba na uongozi wao. Ni vyema vyama vya siasa vikatekeleza wajibu zake badala ya kulazimisha kuungana kinafiki wakati kila kimoja kina mitazamo yake.

Ni ukengemfu chadema kuungana na CUF wakati CUF tayari wameungana na CCM na katibu mkuu wa CUF ni makamo wa raisi ndani ya serikali ya CCM. Utaibana vipi CCM wakati mikakati yote ccm watakuwa wanaipata. Ni uwendawazimu kufikiri CUF ni chama cha upinzani. Nchi kama Israel ambao huwa vyama vinaungana kutengeneza serikali, vile vinavyoungana vinakuwa serikali. Kimsingi CUF inatakiwa ipewe lawama kwenye matatizo yanayoikumba nchi katika mipango inyoshindwa ya serikali kwani CUF ni insider.

Chadema kuungana na CUF bungeni utakuwa uhayawani na usaliti mkubwa kwa wapiga kura. kilio cha wengi ni kushindwa kwa miaka 50 kwa uongozi wa CCM. CUF wakafanya uhuni kukubali ushindi wa wizi wa CCM visiwani kisa Hamadi kaahidiwa umakamu wa raisi. Haya ni matatizo ya viongozi wazee wa kiafrika wanafikia mahali hawajali tena wananchi wanatafuta kufa kwa heshima kwa kuwasaliti wananchi. wanataka kuzikwa kwa mizinga wakiwaacha wengi hoi.

kwa yeyote mwenye akili timamu hawezi kutenganisha CCM zanzibar na Bara. mwenyekiti wa ccm taifa ni JK. wote Shein na Kikwete wanafuata maamuzi ya kamati kuu. sasa hiyo ndoa ya cuf na ccm maana yake nini......Usaliti.

Tunataka ushindani wa maendeleo ya kweli, check and balance isiyo na rushwa ya madaraka. nataka kuona vyama vya siasa amaivyo vitaachiana ofisi sio kuzitumia pamoja, hii itasaidia kila mmoja kumwogopa mwenzake na sio kufiachiana siri za wizi, ufisadi, rushwa, uhujumu, kulindana kwa kisingizio tulitengeneza serikali pamoja.

CUF wameamua kutumia tamaa ya madaraka badala ya kuwaletea wananchi na wapiga kura wao maendeleo ya kweli.

Mwaka 2000 walikufa wapemba katika mapambano ya kupigania haki, haki ambayo hamadi kaiuza ili kuwa kibaraka wa ccm. kaiuza na haki ya msingi ya kuwakumbuka mashujaa wale kwamba walitoa damu yao kupigania haki. Hawakumbukwi wala hakuna siku yao. Kwani siku ya mashujaa ni ya nini, ni watu kama wao. CUF imeamua kula njama na ccm na kuwapotezea mbali wahanga wa mapinduzi ya kiuchumi na demokrasia ya kweli kwa ndoa ya kinafiki ya ccm.

Chadema wana haki ya msingi kukataa upuuzi wowote wa muunguano na cuf. na siku kwa njia au hila yeyote ile chadema watatengeneza serikali ya mseto na ccm watakuwa wamepoteza sifa ya kuwa chama cha siasa kama cuf walivyopoteza sifa.

Nia moja kubwa ya chama cha siasa ni kushika madaraka na kutekeleza ilani zake na dira zake za maendeleo kwa wananchi wake.

serikali za umoja wa kitaifa ni uuwaji wa demokrasia na mwendelezo wa udikteka na mfumo wa chama kimoja kutawala nchi.
 
Kurunzi, points nzuri! Lakini mimi ni mpenzi wa Chadema ila kijaribu kufanya siasa kivingine. Ushirikiano na vyama vingine vya upinzani si muungano wa vyama. Wengi wa wachangiaji wanamtizamo wa TANU + ASP = CCM. la! Ni makubaliano ya ku-support misimamo. Hakuna siri zinazouzwa TLP, UDP, NCCR au hata CUF. Ni uhusiano wa kusupport misimamo huku bara. Nikupe mfano Ujerumani kuna vyama vinavyokinzana kwenye siasa za kitaifa lakini vikaungana kwenye siasa katika majimbo. Nadhani tunapaswa kujifunza demokrasia ya vyama vingi
 
CUF wake up, know where you are, Sisi CCM tunawahitaji huku bara, nyie ni Serikali eti. mlidhani mko upinzani.

Usawa wa Serikali, Mbeleeeeeeeee tembea.
 
wanaosema kuungana ili kuongeza nguvu kwenye kutetea hoja! ni nchi gani duniani chama kimoja kikaungana na vyma viwili kwa wakati mmoja upande mmoja kutengeneza serikali iliyoko madarakani na upande mwingine na upinzani unayoipinga serikali hiyo hiyo iliyoko madarakani. No spinning naitaka hiyo nchi. Hakuna kitu kama hicho hii katuni ipo Tanzania tu. Hili ni tatizo kubwa sana la watanzania kupaste bila kutafakari. unapoungana na CUF unampango wa kwenda kumbana nani? na nini kipo kwenye mkataba wa serikali ya umoja wa kitaifa baina ya cuf na ccm?

Wananchi tunawajibu wa kuwaambia viongozi wetu umangemeza umepitwa na wakati tunahitaji na maendeleo ya kweli sio uroho wa madaraka. Kwani cuf wakiwa bungeni wanakosa haki gani ya kuwa wabunge na kuwawakilisha wananchi wao ? kwanini walazimishe kuungana na chadema. mbona hoja za akina mwakyembe ziliungwa mkono na akina Slaa ? kama mtu atakuwa anatetea maslahi ya nchi si lazima aungane na mtu hata akiwa mwenyewe ataungwa mkono na wengi. Njaa ya madaraka inachanganya wananchi
 
Hii move ni counter-productive. Unajua unapokuwa huna hata nguvu ya kuzuia muswada au bajeti kupitishwa bungeni then unakuwa aunahitaji kila aina ya support kutoka kila mahali hata kama pamoja na support hiyo bado hutoweza kupiga kura yako ya turufu.

Nchi hii ina matatizo mengi na ni vyema wale wasiokuwa sehemu ya CCM (chanzo cha matatizo) au hata wa ndani ya CCM ila wenye chembe ya uzalendo, wakaungana na kuzungumza lugha moja. Kitakachotokea ni Chadema kupigana vita on two fronts which serves no real purpose in practice.
 
Hii hoja...hivi aliyeinzisha kwenye majukwaa ya siasa wakati ule wa kampeni alijua athari zake, kuwa ni za muda mrefu si muda mfupi
 
CHADEMA wanaisoma sana JamiiForums. Maazimio yao yote yamo humu. Ni kama vile walioko humu ndio wanaounda CC ya CHADEMA. Jambo jema sana hili kwani vichwa na uhuru wa kuandika ulioko humu haupatikani kungine kokote Tanzania hii ya leo.
 
wametoa tamko kuhusu matokeo ya form four pia. Wataunda kamati ya / tume ambayo. Itatoa report kufikia mwezi wa tano.
Katiba mpya mchakato uanzie bungeni .
chadema bwana wanafanya mambo ambayo ccm hawakufikilia kabisaa kuyafanya.
 
wewe ni yule Mwera wa Tarime lazima. Punguza hasira! Hizi ni mbio za vijiti mkuu. Pole... Chadema hayo ndo maamuzi ambayo sisi tulikuwa tunayangoja
 
Cuf wanachohitaji hapa ni huruma ya chadema kwani kwa sheria za bunge chadema ndio wanaostahili kuunda kambi ya upinzani.:thinking:
 
Hurusiwi kuvaa nguo za chama chengine zaidi ya zile za cuf. Kama unashida ya maandamano njoo la kama unashida ya kuvaa magwanda ya wafungwa subiri maandamano ya chadema keshatangaza padri slaa mda si mrefu.

sio maalim seif
 
Cuf ina viti 2 bara(tanganyika) ie lindi mjini na kilwa kusini na pia cuf ina madiwani karibu 200 huku tanganyika,
jee chadema wana viti vingapi zanzibar? Chadema Wana madiwani wangapi zanzibar?

Wingi sio jambo kiivyo. Angalia jongoo ana miguu mingi lkn hana mbio. Ni sawa na wingi wa watanganyika hauna maana yeyote ktk mambo ya muungano iko sawa na zanzibar iliyo na watu milion moja? Upo mlevi?

mlevi jk au? acha matusi,mod wapi siku izi
 
Back
Top Bottom