Tamko la CUF kuhusu vurugu za Zanzibar

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Chama cha Wananchi CUF kinasikitishwa na matukio ambayo hayakutarajiwa kutokea hapa Zanzibar yaliyoanza kujitokeza jana tarehe 17/10/2012 ambayo yamesababisha vurugu kubwa katika Manispaa ya Zanzibar na vitongoji vyake.

Matukio hayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa mali za Umma, wananchi mmoja mmoja na hata vyama vya siasa. Miongoni mwa vitendo hivyo ni kuvunjwa Maduka, vyombo vya usafiri, kukatwa miti ovyo na nguzo za umeme, pamoja na kuchomwa moto maskani za CCM. Matukio mengine ya kusikitisha na kuhuzunisha kufuatia vurugu hizo ni kuwepo taarifa za kuuwawa kwa Askari Polisi.

Kutokana na vitendo hivyo, Chama Cha wananchi CUF kinaalaani kwa nguvu zote matukio hayo ambayo yamepelekea uvunjifu wa mkubwa wa amani ya nchi, na kusababisha hofu kubwa kwa raia pamoja na wageni wanaotembelea Zanzibar.

Sambamba na vurugu hizo, Chama Cha Wananchi CUF kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyotolewa na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mhe. Mohammed Aboud Mohammed iliyoeleza juu ya kutoweka kwa Sheikh Farid Hadi Ahmed katika mazingira ya kutatanisha.

Katika Taarifa hiyo, Serikali imethibitisha kuwa vyombo vyake vyote vya ulinzi havijamkamata Sheikh Farid, jambo ambalo limezidisha hofu na wasi wasi kwa wananchi juu ya mahali alipo na hali yake kiongozi huyo wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar.

Chama cha Wananchi CUF kinaiomba Serikali kuendeleza juhudi zote za kuhakikisha taarifa za ukweli na za uhakika zinapatikana juu ya kadhia ya kutoweka kwa Sheikh huyo kwani Sheikh Farid ni raia wa nchi hii, na Serikali hii ni kwajili ya wananchi wote, ili kuondoa hofu na wasi wasi ambao umesababisha baadhi ya wananchi kujengwa na dhana mbaya.

Aidha, Chama cha wananchi CUF kinawataka wanachama wake, wapenzi na wananchi wote kwa ujumla kutojiingiza na kutofanya vitendo vyovyote vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani ya nchi yetu.

Sote kwa pamoja tukatae kabisa kujihusisha na vitendo vya kuleta vurugu kwa vitendo na kauli zitakazopelekea kuiondolea sifa njema nchi hii ya Zanzibar ambayo imejijengea duniani kote.

Haki sawa kwa Wote

………………………..
Salim Biman
Kaimu Naibu katibu Mkuu Zanzibar
 
Kusikitika hakutoshi. Kwanini CUF hailaani kama haiko nyuma ya vurugu hizi hasa kipindi hiki Seif anaanza kujitafutia nafasi ya kugombea tena urais baada ya kuwekwa kinyumba na CCM na kunogewa?
 
ujinga mtupu, ni.ichokiona hapo Cuf wanataka serikali iseme alipo huyo sheikh mleta balaa
 
Mbona Maskani za CUF hazijachomwa? Hii inadhibitisha kuwa Uamsho ni Sehemu ya CUF.
 
AYA EPISODE NYINGINE TUONE MTU NA MUMEWE WAKIPEPESA MACHO NA KUUMAUMA MANENO EH PATAMU APO, SIE TNATAKA KUJUA FARID WETU YUKO WAPi?
 
Ikumbukwe kuwa vurugu hizi zilianza pale CUF ilipotamka kuwa haimtambui Mbunge aliyechaguliwa hivi karibuni (Jimbo la Bububu). CUF Mnajitoaje kwenye hili? Nionacho mimi mnajikosha ili muonekane na ninyi mnapinga jambo hili lakini ukweli mnaujua
 
Nchi ya Zanzibar??mnafiki hajifichi wanataka kuvunja muungono ili watamke ktk Nchi ya Pemba kuna......
 
AYA EPISODE NYINGINE TUONE MTU NA MUMEWE WAKIPEPESA MACHO NA KUUMAUMA MANENO EH PATAMU APO, SIE TNATAKA KUJUA FARID WETU YUKO WAPi?
Mbona mnajua wenyewe alipo huyo muuaji wenu si alienda na garı yake na dreva wake akabadili akapanda garı nyingine huyo kaenda zake huyo ndıo kutekwa?hebu acheni jana yenu yakutlar kuhalalisha hızı Fiko zenu
 
Aidha, Chama cha wananchi CUF kinawataka wanachama wake, wapenzi na wananchi wote kwa ujumla kutojiingiza na kutofanya vitendo vyovyote vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani ya nchi yetu.
Amani itavunjika mara ngapi? au mpaka sasa wanaona amani bado ipo?
 
Kusikitika hakutoshi. Kwanini CUF hailaani kama haiko nyuma ya vurugu hizi hasa kipindi hiki Seif anaanza kujitafutia nafasi ya kugombea tena urais baada ya kuwekwa kinyumba na CCM na kunogewa?

kwani chadema iko wapi hata ishindwe mpaka leo kusema kitu au inakula mtori Arusha
 
Mwana umleavyo ndivyo akuavyo ubaguzi ni kitu hatari sana leo hii watanganyika hawawataki znz, wakristo hawatakiwi, wakiona makanisa wanaweweseka, ccm wanaihujumu, serikali hawaitii, suk imeleta amani ya geresha wanatafunana visogo, cuf wanashindwa kulaani uchomaji wa makanisa, wamesahau manyanyasa ya waarabu?

Palipo na mwarabu mwisilamu mweusi ni kafiri,kuna misikiti ipo washwahili hawaruhusiwi kuingia wala kuswali, waeshimu watu waliokuletea elimu, waliokufundisha kusoma, bado hamjajua kitu kuna elimu bado hamjaifikia, wachache mliosoma waeloimisheni wenzenu.
 
CUF wanajua A TO Z ya kinachoendelea Zanzibar. wana mawasiliano ya karibu na FARID na ndio maana waliamua kumficha ili wawadanganye wazanzibar kama ametekwa nyara na kuhifadhiwa Tanzania bara ili waone kama ataungwa mkono na wazanzibar kwa kiasi gani kabla ya kutangaza uasi kamili.walikuwa wanapima upepo,bahati mbaya hawaja ungwa mkono kihivyo!! pole yenu CUF,POLE YENU UAMSHO.
 
Back
Top Bottom