Tamko la CCM juu ya kumwagiwa tindikali katibu wa mufti Zanzibar

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Chama Cha Mapinduzi kinasikitishwa na kitendo cha kinyama alichofanyiwa Sheikh Fadhili Soraga cha kumwagiwa tindikali sehemu ya uso na kifuani. Sheikh Soraga ni mtu maarufu hapa Zanzibar kwani huwa anashiriki katika shughuli mbali mbali za kidini hapa nchini, yeye ni Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar. Sheikh Soraga amefanyiwa unyama huo na watu wasiojuulikana wakati akitoka kwenye mazoezi ya viungo asubuhi ya leo.

Sheikh Soraga ni miongoni mwa masheikh wachache hapa zanzibar wenye kuheshimika na kueleweka. Hivi karibuni Sheikh Soraga alitoa hutuba nzuri na fasaha kwenye sala ya Eid-Haji juu ya kuimarisha amani na utulivu katika visiwa vyetu vya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Khutba hiyo aliitoa mbele ya viongozi wakubwa wakitaifa waliohudhuria katika sala hio, miongoni mwa viongozi hao ni pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dk. Ali Mohamed Shein, Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharifu Hamadi, Rais Mstaafu wa awamu ya sita wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume na viongozi wengine kadhaa.

Siku hiyo hiyo katika Baraza la Iddi lililofanyika katika Ukumbi wa Salama Bwawani Sheikh Soraga wakati akitoa khutba ya utangulizi aliwaasa tena wazanzibari na watanzania kwa ujumla juu ya umuhimu wa amani, lakini katika hafla hiyo Sheikh Soraga alikwenda mbali zaidi kwani alitoa takwimu za hasara iliyoipata Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano, mashirika ya watu binafsi na ya Umma, taasisi za Kidini pamoja na vyama vya Siasa hasa Chama Cha Mapinduzi kufuatia vurugu mbali mbali zilizokuwa zikifanywa na Uamsho.

Vitendo vya kumwagiwa watu tindikali hapa Zanzubar vimeanza siku nyingi. Kama tutakumbuka mnamo mwaka 1995 Kada wa Chama Cha Mapinduzi ndugu Ali Mwinyi Msuko alimwagiwa tindikali na watu wasiojuulikana huko Wete Pemba, mwaka 2007 wakati zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura huko Pemba Sheha mmoja alimwagiwa tindi kali, na mwaka uliopita Ndugu. Rashid Ali Juma Mkurugenzi wa Baraza la Mji wa Zanzibar nae alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana na leo hii Sheikh Fadhil Soraga Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar nae amemwagiwa tindikali pia na watu wasiojulikana.

Chama Cha Mapinduzi kinasema kimechoka kusikia vitendo hivi vya kinyama vya kumwagiwa watu tindikali na watu wasiojulikana. Tunaviomba vyombo vya Dola kuwatafuta watu hawa waovu wasio na huruma na wenzao ili wakamatwe waweze kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria.

Mwisho Chama Cha Mapinduzi kinawaomba wananchi wote wapenda amani na utulivu kumuombea dua Mwalimu wetu Sheikh Fadhil Soraga, Mwenyezi Mungu ampe moyo wa subira yeye na familia yake na amjaalie wepesi ili apone haraka. Sheikh Soraga hivi sasa amesafirishwa kupelekwa Muhimbili kwa Matibabu zaidi.

“KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI’
MAPINDUZI DAIMA

Issa Haji Usssi Gavu
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC
Idara ya Itikadi na Uenezi
ZANZIBAR.
 
Soraga hana umaarufu wwte wacha kumwaga sifa za kipuuzi.

Soraga amevuna alichopanda, wacha aonje utamu wa fitna zake kwa waislam wa znz.

Any way Allah ampe afya njema huenda akajifunza.
 
Inasemekana sheikh alikua anatoka nyumba ndogo alivofuymwa akaona aue soo akajimwagia tindi kali asa akabugi stepu akajimwagia sana
 
Inawezekana hili tamko liliandaliwa jana kabla ya tukio!hongereni CCM kwa maandalizi mazuri!
 
taarifa kwa vyombo vya habari

chama cha mapinduzi kinasikitishwa na kitendo cha kinyama alichofanyiwa sheikh fadhili soraga cha kumwagiwa tindikali sehemu ya uso na kifuani. Sheikh soraga ni mtu maarufu hapa zanzibar kwani huwa anashiriki katika shughuli mbali mbali za kidini hapa nchini, yeye ni katibu wa mufti mkuu wa zanzibar. Sheikh soraga amefanyiwa unyama huo na watu wasiojuulikana wakati akitoka kwenye mazoezi ya viungo asubuhi ya leo.

Sheikh soraga ni miongoni mwa masheikh wachache hapa zanzibar wenye kuheshimika na kueleweka. Hivi karibuni sheikh soraga alitoa hutuba nzuri na fasaha kwenye sala ya eid-haji juu ya kuimarisha amani na utulivu katika visiwa vyetu vya zanzibar na tanzania kwa ujumla. Khutba hiyo aliitoa mbele ya viongozi wakubwa wakitaifa waliohudhuria katika sala hio, miongoni mwa viongozi hao ni pamoja na rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi mh. Dk. Ali mohamed shein, makamo wa kwanza wa rais wa zanzibar maalim seif sharifu hamadi, rais mstaafu wa awamu ya sita wa zanzibar dk. Amani abeid karume na viongozi wengine kadhaa.

Siku hiyo hiyo katika baraza la iddi lililofanyika katika ukumbi wa salama bwawani sheikh soraga wakati akitoa khutba ya utangulizi aliwaasa tena wazanzibari na watanzania kwa ujumla juu ya umuhimu wa amani, lakini katika hafla hiyo sheikh soraga alikwenda mbali zaidi kwani alitoa takwimu za hasara iliyoipata serikali ya mapinduzi ya zanzibar na jamhuri ya muungano, mashirika ya watu binafsi na ya umma, taasisi za kidini pamoja na vyama vya siasa hasa chama cha mapinduzi kufuatia vurugu mbali mbali zilizokuwa zikifanywa na uamsho.

Vitendo vya kumwagiwa watu tindikali hapa zanzubar vimeanza siku nyingi. Kama tutakumbuka mnamo mwaka 1995 kada wa chama cha mapinduzi ndugu ali mwinyi msuko alimwagiwa tindikali na watu wasiojuulikana huko wete pemba, mwaka 2007 wakati zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura huko pemba sheha mmoja alimwagiwa tindi kali, na mwaka uliopita ndugu. Rashid ali juma mkurugenzi wa baraza la mji wa zanzibar nae alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana na leo hii sheikh fadhil soraga katibu wa mufti mkuu wa zanzibar nae amemwagiwa tindikali pia na watu wasiojulikana.

Chama cha mapinduzi kinasema kimechoka kusikia vitendo hivi vya kinyama vya kumwagiwa watu tindikali na watu wasiojulikana. Tunaviomba vyombo vya dola kuwatafuta watu hawa waovu wasio na huruma na wenzao ili wakamatwe waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Mwisho chama cha mapinduzi kinawaomba wananchi wote wapenda amani na utulivu kumuombea dua mwalimu wetu sheikh fadhil soraga, mwenyezi mungu ampe moyo wa subira yeye na familia yake na amjaalie wepesi ili apone haraka. Sheikh soraga hivi sasa amesafirishwa kupelekwa muhimbili kwa matibabu zaidi.

"kidumu chama cha mapinduzi'
mapinduzi daima

issa haji usssi gavu
katibu wa kamati maalum ya nec
idara ya itikadi na uenezi
zanzibar.



itakua ni uamsho tuh haooo
hawa jamaa wana laana sana
 
Mtu ameumizwa halafu wewe unasema eti Kidumu Chama Cha Mapinduzi
 
Uamsho mnaanzisha wenyewe halafu mnalia, kamata hao magaidi wanyoe ndevu kwa chupa hadharani, mijitu imetoka Oman halafu ooh! Tunataka nchi yetu! Kamwe hamnafanikiwa!!
 
Walisahau kutoa tamko kipindi kile Mwakyembe alivyopewa sumu??
si wangeliunganishia humu humu tuu.
 
CCM ina uhusiano gani na Katibu Mufti wa Zanzibar mpaka iwe ya kwanza kutoa statement?
 
CCM wana viroja! Huyu mtu walikua wanamtumilia kwa masilahi yao, mbona alipotekwa Sheikh Farid hawakutoa tamko?
 
Kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi, tunatia pole pia kwa kumwagiwa kwa Tindikali kwa Kubenea wa gazeti lilofungiwa mwanahalisi, pole kwa Dr Mwakembe, mauaji ya Mwandhi wa chanel ten Mwangosi, bila kusahau Morogoro wakati wa maandamano ya kudai haki ya Chadema. Poleni sana wazanzibar kwa niaba ya CCM.

MAPINDUZI DAIMA.
 
dah jamaa yuko hoi anaumwa alafu watu wanasema kidumu chama chao....ccm will always b ccm utadhani wamezaliwa na baba/mama mmoja
 
Back
Top Bottom