Tambwe hiza, ahusisha migomo ya tanzania na chadema

PayGod

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
1,259
57
Tambwe hiza kiongozi wa propaganda CCM, akihojiwa na chanel ten, amesema CDM , ndio kinausika na migomo yote ya hapa nchini inayotokea, kwa habari zaidi fatilia chanel ten sasa hivi
 
Yeye anasema eti ni sahii mary chitanda kupiga kura ya udiwani kwenye JIJI la Arusha, hakuna mbunge wa viti maalum wa mkoa fulani, unaweza kupiga kura mkoa wowote
 
Kipindi kimeisha ila watu wote waliopiga simu wamemshangaa tambwe hiza kwa kuhusisha migomo ya ttcl, udom na CHADEMA, kwa kumwambia migomo ilikuwepo hata kipindi cha Chama kimoja, kwa mfano SITTA alishawahi kuongoza mgomo wa UDSM , hezi hizo za chama kimoja tu, je hapo napo chadema ilihusika
 
Najua wapo baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasaambavyo vimepanga mikakati ya kuendeleza malumbano yauchaguzi na kutaka Watanzania waishi kama vile nchi ipokwenye kampeni za uchaguzi.Wamepanga wakati wotekutafuta jambo au hata kuzua jambo ili kuwachocheawananchi waichukie Serikali. Wamepanga kuchocheamigomo vyuoni na maandamano ya wananchi mara kwamara. Kwao wao huo ndiyo mkakati wa kujijenga kisiasa ilikujiandalia ushindi kwenye uchaguzi wa mwaka 2015. - JK salaam za mwaka mpya 2011.

Source: Bonyeza Hapa

Watanzania bana yaani mmesahau mara hii mwenyekiti wa chama cha akina Tambwe alichosema katika salaam zake za mwaka mpya. Tambwe amefanya nukuu tu. Najikuta nawashangaa wanaomshangaa Tambwe ila hawakumshangaa mwenye kiti wake.
 
Kwa hiyo hii itakuwa sera ya ccm kila wapopata muda wa kuongea na chombo cha habari

Najua wapo baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa ambavyo vimepanga mikakati ya kuendeleza malumbano ya uchaguzi na kutaka Watanzania waishi kama vile nchi ipo kwenye kampeni za uchaguzi.Wamepanga wakati wote kutafuta jambo au hata kuzua jambo ili kuwachochea wananchi waichukie Serikali. Wamepanga kuchochea migomo vyuoni na maandamano ya wananchi mara kwa mara. Kwao wao huo ndiyo mkakati wa kujijenga kisiasa ili kujiandalia ushindi kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.

[FONT=Palatino Linotype, serif]Nawatanabaisha ndugu zangu myajue hayo ili msipoteze muda wenu muhimu wa kujiendeleza na kugeuzwa kuwa mbuzi wa kafara kwa ajili ya kuendeleza maslahi ya kisiasa ya watu fulani. Kwa jinsi watu hao walivyokuwa wabinafsi na wasivyokuwa na huruma na wenzao, wako tayari kuchochea ghasia bila kujali madhara yatakayowakuta watu watakaoshiriki. Wao hasa wanachotaka ni ghasia kutokea na vyombo vya dola kuingilia ati waiambie jumuiya ya kimataifa jinsi Serikali yetu ilivyo katili. Nawasihi ndugu zangu msiwasikilize wala kuwafuata wanasiasa hawa[/FONT]
 
Tambwe hiza kiongozi wa propaganda CCM, akihojiwa na chanel ten, amesema CDM , ndio kinausika na migomo yote ya hapa nchini inayotokea, kwa habari zaidi fatilia chanel ten sasa hivi

Huyu ni puppet kama alivyo Makamba wanatumika kwa manufaa ya hao viongozi wa CCM wanakuwa remote controlled, soon wata-expire then watatupwa kama Big G.
 
Sikupoteza muda kumsikiliza kwa kuwa nilijua ataongea propaganda tu!
 
Hivi Wasambaa wote duniani akili zao ni kama za Tambwe na Makamba? Nauliza tu jamani msichukie watani zangu Wasambaa!
 
Wakuu huyu Tambwe ni mtu wa kupuuzwa hana jipya ambalo linaweza kulisaidia taifa letu changa!!
 
Tambwe hiza hastahili kujadiliwa na watu wenye fikra pevu, huyu ni kasuku wa chama cha majambazi.
 
Tambwe hiza kiongozi wa propaganda CCM, akihojiwa na chanel ten, amesema CDM , ndio kinausika na migomo yote ya hapa nchini inayotokea, kwa habari zaidi fatilia chanel ten sasa hivi


Hii ni kweli kabisa, maana CDM ndio inawapa watu elimu ya kutosha na kufichua jinsi wafanyakazi, wanafunzi na raia wa kawaida wanavyonyanyasika na utawala wa ubabe, uliojaa ufisadi na manyanyaso.

Just imagine wana hela ya kuilipa dowans kampuni hata serikali haijui mmiliki wake lakini hawana hela ya kuwapa wanachuo na kulipa madai ya wahadhiri. This is shame to Tambwe, JK, Makamba etc and CCM.

Ahsananteni waTZ kwa kuelewa haki zenu za msingi na muendelee kuzidai.

Hongera CDM na Viongozi wake kwa kuwafungua waTZ macho.

Tuko pamoja.
 
Uliposema tu Tambwe Hiza nilichomoa power cable ili watoto wasije wakaselect Ch 10 kwa bahati mbaya!
 
Cha msingi kama watu wanagoma kwa sababu zenye maana na ikiwa ni katika harakati za kupigania haki zao kosa liko wapi hata kama CDM ndio wanawaongoza kufanya hivyo.Naona kwa hilo wametoa pongezi kwa CDM kuwa wako mstari wa mbele kuwashawisha wananchi kudai haki zao.Pole kwa ujinga wao(CCM) kuisifia CDM bila kujua.
 
Badala ya kudeal na caose wao wanahangaika na repercussion, chanzo ni ccm wenyewe ambao wamekataa kuwapa watz haki zao msingi . Wasisingizie cdm!
 
Huyu jamaa kipindi akiwa upinzani aliwahi kusema kama atarudi chama tawala basi amlale mama yake.
Sasa amerudi chama tawala na tgena ni naibu kitengo cha umbea(propaganda)
hapa tumuulize ndg yetu tambwe,vipi ametekeleza ile ahadi yake?maana amerudi tayari chama tawala.
My take:tambwe ni wa kupuuzwa tena kwa hali ya juu kabisa
 
Back
Top Bottom