Tamasha la filamu za bara asia kuanza kesho

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,320
33,125
pix.gif
TAMASHA kubwa la filamu za Bara la Asia linatarajiwa kuanza kesho katika Ukumbi wa World Cinema uliopo Mwenge jijini Dar na kumalizika Machi 25 mwaka huu.
Katika tamasha hilo nchi zilizohakikisha kushiriki ni pamoja na India, Iran, China, Korea na Indonesia.
Akizungumza na mtandao huu katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar, Balozi wa India hapa nchini, Ngulkham Gangte, alisema lengo la tamasha hilo hapa ni kutaka kuunganisha mahusiano ya kiutamaduni kati ya nchi za bara la Asia na Tanzania.

Balozi wa India hapa nchini, Ngulkham Gangte akiwajuza wanahabari tamasha hilo. Kulia ni Afisa Utamaduni wa Ubalozi wa Iran, Saeed Omidi na kulia ni mmoja wa wadau kutoka bara la Asia.


Baadhi ya washiriki wa hafla hiyo wakipata burudani ya vinywaji baridi.


Washiriki wengine wa hafla hiyo walionaswa na kamera yetu wakikata kiu.
 
Hivi sisi nasi tuna matamasha yetu ya filamu za kiafrika tunayoyafanya kwenye mabara mengine?
Kama hatuna maonyesho yetu nje, tutarajie nini??
Kufa kwa utamaduni kwa mwafrika ndio huku.
 
Back
Top Bottom