pia nadhani Synovate wanazo ripoti za tafiti za coverage ya radio na TV hapa Tz kwa hiyo ni muhimu pia kuzisoma na kuona ni maeneo gani kijiografia yanahitaji ukombozi zaidi
Wanafunzi wakimsikiliza kwa makini Kamanda Mbowe alipokuwa akiwahutubia.
Mh. Mbowe alizungumzia Maandamano ya Arusha na kusema yameamsha hamasa mpya katika Taifa kwa ujumla na kwamba Wananchi watulie wakati Chama kinapanga mikakakati mipya na kwamba hakuna kulala mpaka kieleweke.
Akijibu risala ya wanafunzi, alisema Hivi karibuni CDM itaanzisha operation kubwa kuliko ile Sangara ili kuhakikisha kwamba kila kijiji kinafikiwa nchi nzima na Makamanda wa CDM wakiwemo wabunge wote 48 na kuwataka wabunge kujiandaa kikamilifu kwa kazi hiyo.
Mh. Mbowe alisema, CCM katika uwanja wa mapambano ni laini kuliko embe Mbivu, na kwamba Chama hicho kinategemea zaidi vyombo vya dola, ikulu na usalama wa Taifa. Alisema kama kungekuwa na uwanja huru kwenye uwanja wa mapambano, CDM wanao uwezo wa kuishinda CCM kumi bila (kwa kutoa mfano wa Soka)
Pichani, Mheshimiwa Mbowe akiwa na Mwenyekiti wa CDM mkoa Arusha Bw. Samson Mwigamba Kushoto, Mwenyekiti wa Tawi la Chuo kikuu Makumira CDM M/s Rose na kulia kabisa ni Mwenyekiti wa CDM wilaya ya Meru.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.