TAKUKURU wachunguzwe na CAG, wabadhirifu wa mamilioni wanyongwe

Mzalendo120

JF-Expert Member
Jul 2, 2022
1,601
2,091
Nimejiuliza kwanini hao TAKUKURU ofisi yao haikaguliwi na CAG. Hii nikwasababu ndani ya ofisi hiyo kuna walarushwa na wabadhirifu.

Kuna kesi wamezikaliatu wala hawapepesi macho kuzipitia.

Huu ufujaji unaotokea TAKUKURU wanamahali wamepwaya. Nchi nzima inanuka ubadhirifu, mikataba hewa, mawaziri wahovyo lakini taasisi ipo mpaka watu wanaambiwa wajitafakari

Kuhusu adhabu ya kunyonga wapo waliopendekeza ifutwe akiwemo mzee Pinda.

Ninapendekeza watu kama hao waliofanya ubadhirifu kwenye ununuzi wa ndege wanyongwetu. Hii nikwasababu kitendo cha kufuja hela zote hizo nisawa na kuwaua watanzania waliokosa matibabu hospitalini,madaktari wachache maana hawajaajiriwa wengi,wanafunzi hawana walimu shuleni,maji safi na salama hakuna vijijini wala mjini. Wengi wanakufa kwa uzembe wawachache. Wachache wanyongwe ili wengi waishi. Hapo tuone huyo mtetezi wa wezi atajenga hoja gani.

Nchi imekua ya kutuhumiana wizi na wanaotakiwa kuchukua hatua wanalalamika
Imefikia hatua hata Rais anawaambia wezi wajitafakari? Wanajipanga kuiba tena. Wanyongwe tu ili kuokoa walio wengi
 
Back
Top Bottom