TAKUKURU: Askofu na Viongozi Wakuu wa Kanisa la Avengelical assembless of God (EAGT) wachungunzwa kwa rushwa

Hawa ndio walitoa tuzo na sifa kemkem kumbe nyuma yao mafisadi..walidhani wako salama .....
Nilipowaona wakisifia nilijua wazi kuwa kuna kitu 'kimeoza nyuma ya pazia' na kweli, kumbe kusifia kwao ni sehemu ya kuficha ujinga uharamia wao. Hawa ngosha hawa!
 
Shetani yuko kazini.Anajaribi kila awezalo kuudhalilisha wokovu na Kanisa la Mungu.Ni wakati sasa wa kila anaye-amini kwamba kaokoka kujisimimamia mwenyewe.

Mfumo wa madhehebu yanayoitwa ya kilokole uko under violent attack.We see this in many areas.Hata wanaoitwa Wachungaji sasa wanajinyonga!Ni aibu kubwa.
 
Mkuu kwa kiasi kikubwa makanisa yanayoitwa ya kiroho yote yana matatizo,hakuna lililo salama,kwa hivyo hili LA EAGT wala halishangazi.Ukienda kwa mfano kwenye kanisa la Askofu Mtokambali Muembe Songo, utagundua mambo ya ajabu sana.Nalizungumzia hili specifically kwa kuwa Askofu wa TAG ndilo Kanisa lake,so I expect it to be best.Ila kinyume chake kanisa limejazwa taratibu za kidunia ambazo ni foreign kwa watu wa kiroho!

Zoe FM ambayo nilitegemea kusikia mahubiri mazuri,vipindi vya nyimbo za Injili safi na tenzi za rohoni,nayo ina air vipindi vya kawaida za dunia kama mipira.Katika hali ya kushangaza,eti nao wanapiga sebene la Yesu,Yesu ana Sebene!Aibu tupu.Ni kumdhalilisha tu Yesu wangu.Yaani wameshindwa kabisa kujua kwamba Shetani ana rythym zake na Mungu ana rythym zake.The funny thing is,Askofu yupo hapo hapo,sijui haoni Radio yake inavyo-dilute spirituality!

Frankly niwe mkweli,yanayojiita makanisa ya kiroho it is over,Roho Mtakatifu ameshaondoka,imebaki mazoea ya kuigiza kuongea kwa lugha ya Roho Mtakatifu tu.Ni dini tu sasa.Hata hivyo naamini katika kiza hiki kinene cha kiroho,Mungu hatanyamaza,atafanya jambo jipya.
 
Chabusalu:
Tatizo ni la kiuongozi na kukosa transparency.
1. Katika mikutano mikuu yote ndiko ambapo maswali na hoja zozote hujibiwa. Jambo hilo halifanyiki. Mara nyingi ikitokea hoja yoyote ambayo inagusa uongozi haijibiwi na unaamulishwa kukaa chini.
2. Kuhusu magari tupeane mawasiliano njoo nikuonyeshe ushahidi.
3. Taasisi yoyote huwa ina TIN namba moja njoo nikuonyeshe Tin namba 5 za dhehebu hili ambazo zimetumika.
4. Kuhusu majengo tangu yamenunuliwa na kukodishwa hakuna taarifa yoyote ya mapato wala matumizi. Na mengine mengi.
Kwa taarifa yako siongei hadithi ya kusimuliwa, mimi ninajua nina chokisema
Ndo maana nimekwambia kama kweli unataka ukweli na ushahidi wa jambo hili nitafute.
 
Kanisa limeharibika sasa kuna biashara kanisani watu wanauziwa mafuta, chunvi, keki, vitambaa eti vina upako
nimekuwa nasikia zamani watu walikuwa wanaponywa, viwete wanatembea, viziwi kusikia na vipopofu kuona tena hadharani. Kanisa limeingilia na wabinafsi tena jaama lingine lilikuwa Calvary Assemblies of God CAG pale Majengo Moshi baadae likachomoka likaenda sijui wapi liliporudi nikafikia Dar es Salaam linakanyagisha watu mafuta. Ushetani mkubwa kabisa Mungu atusaidia kanisa lirudi katika hadhi yake ya awali
 
Kutokuwa na transparency unakuchukuliaje na issue ya maadili.

Nimesema wewe unaye taka kujiridhisha na ninacho sema nitafute nikupe ushahidi na vielelezo. Sipo kushabikia issue yoyote hapa.
 
Chabusalu:
Tatizo ni la kiuongozi na kukosa transparency.
1. Katika mikutano mikuu yote ndiko ambapo maswali na hoja zozote hujibiwa. Jambo hilo halifanyiki. Mara nyingi ikitokea hoja yoyote ambayo inagusa uongozi haijibiwi na unaamulishwa kukaa chini.
2. Kuhusu magari tupeane mawasiliano njoo nikuonyeshe ushahidi.
3. Taasisi yoyote huwa ina TIN namba moja njoo nikuonyeshe Tin namba 5 za dhehebu hili ambazo zimetumika.
4. Kuhusu majengo tangu yamenunuliwa na kukodishwa hakuna taarifa yoyote ya mapato wala matumizi. Na mengine mengi.
Kwa taarifa yako siongei hadithi ya kusimuliwa, mimi ninajua nina chokisema
Ndo maana nimekwambia kama kweli unataka ukweli na ushahidi wa jambo hili nitafute.
Mkuu kama una ushahidi kwann usiweke tuonee
 
Mkuu, kwa haya unayo yaongea it sound like unayajua mengi; ungeeleza ni kwanini hasa mgogoro hu ulianza hasa baada ya askofu msaidizi kutemwa uongozi? Taja hasa sababu ya yeye kuondolewa kwenye hiyo nafasi, huyu askofu msaidizi hasa ndio man of the match. Anachokisema huyo jamaa uliye m quote kipo sahihi, shida ni UKABILA, Wasukuma wanaamini ni lazima awepo msukuma mwenzao pale kwenye kiti; Mwakipesile nae amekaza, kashikiria msimamo wa misingi ya Kibiblia
Mkuu
Makamu askofu Mkuu Mahene yeye ndiye alikuwa wa kwanza kuibua hoja ya ubadhilifu. Katika kuhoji mambo kadhaa akazuliwa kuwa yeye ni mnzinzi hivyo afukunzwe na Mwakipesile akafanya hivyo.
1. Tulimwuliza Mwakipesile adhibitishe tuhuma hizo akadai kuwa kuna nabii ameonyeshwa na Mungu. Na siyo tu kuonyeshwa na Mungu nabii huyo akadai kuwa amemrekodi Mungu wakati akisisitiza kuwa Mahene hafai kuwa makamu. Katika minutes alizo andika katibu mkuu Mwizarubi ameandika hivyo. ( ushahidi ninao wa minutes hizo).
2. Kuhusu issue ya ukabila, dhehebu hilo limekuwa kama makabila mawili ndo yenye hati miliki (i) Wasukuma ( ¡¡) Wanyakyusa, Tangia mwanzo. Nguvu ya wazee wa kinyakyusa ilianza kutokana na mchango mkubwa waliokuwa nao kwa Askofu Kulola hasa wakati wa mgogoro wa kwanza.
1.Askofu M.Kulola- msukuma
Makamu M.Mwamwenda- nyakyusa
Katibu: Ngobito - mgogo.
2. Awamu nyingine:
Askofu M.Kulola - sukuma
Makamu M. Mwamwenda
Katibu M.Mhina- Tanga
M/Hazina E. Andrew- Msukuma.
3.Awamu nyingine tena:
Askofu M Kulola- sukuma
MakamuA. Mwaisabila- nyakyusa
Katibu B. Mwakipesile- nyakyusa
Unaweza kupata picha ya uongozi huo.
Kwenye uongozi huu wa mwisho
4.Askofu B. Mwakipesile- Nyakyusa
Makamu J.Mahene- Sukuma
Katibu L.Mwizarubi- kerewe.
Hivyo ukiacha awamu tatu za mwanzo hii ya nne imepunguza ukabila kwa sehemu.
Hivyo tukizungumzia ukabila upoupo lakini issue ilikuwa baada ya kuhoji ubadhilifu ambao umefanyika wakati wote askofu Mwakipesile akiwa ni kiongozi wajuu. Inasemekana ili kukata mzizi wa fitina askofu alicante mbinu za kumwengua/ kutemwa makamu wake kama ulivyo sema, jambo hilo lilipingwa na mahakama ilitengua maamuzi hayo.
Hii ni stori ndefu:
Lakini kwa kifupi, Mgogoro huu ni wa kiuongozi na mbinu za kuficha baadhi ya matendo hasa yale yasiyo na maadili.
Watu wenye mapenzi mema walishauri uongozi wote ukae pembeni na tupate viongozi wa muda walinusuru dhehebu lakini always ukubwa ni mtamu.
Nimejitahidi kueleza kwa kirefu ili kwa wale wasiojua angalau wawe na mwanga.
 
Kumbuka kanisa Lilikuwa TAG, baada ya ule mgogoro hayati Moses kulola na kundi lake waliamua kujitoa TAG na kuanzisha EAGT. Uporaji uaozungumziwa ni wa mali za TAG kwani viwanja na makanisa yaliyokuwa yanatambulika TAG yalibadilishwa na kuwa EAGT
Usilolijua ni kama usiku wa giza. Hadi sasa hakuna mali yoyote ya TAG iliyoporwa ndugu zangu tusiwe tunasikiliza propaganda za watu, hadi sasa ni viwanja na makanisa yaliyo jengwa na wamissionary wa Assemblie of God toka Springfield Missouri USA ambazo zilibakia kwa kanisa la mahali pamoja.
Hivyo propaganda za kuporwa nadhani huo ni upotovu na uzushi. Tuepuke kusema tusilolijua.
 
Kwanza ieleweke kwamba mimi wala sio muumini wala EAGT, ila jambo ambalo kama Mkristo Mpentekoste nalifuatilia muda mrefu. Naweza kukubaliana na wewe katika hili la "roho ya matengano.' lakini hili kanisa kwa maoni yangu limekusanya hata wasio na hadhi za kuwa wachungaji, wakawa wachungaji. Nahisi, huko nyuma na hata sasa mfumo wa kupata wachungaji uko hovyo!
 
Mkuu uko sahihi sana.
Mimi ni muumini wa dhehebu hili, hatukuwa na roho ya matengano kabisa hasa kipindi cha askofu Kulola. Msisitizo ulikuwa injili ndiyo maana kanisa hili likakua kwa kasi sana.
2. Lakini tulikuwa na ombre la uongozi mzee alikuwa busy na injili tu, hivyo kukaingia wajanja wajanja. Hivi sasa wachungaji walio wengi hawajaitwa wamekuja kupiga deal tu ndo kwa maana haya yote yanajitokeza.
 
1. Kadri ya ufahamu wangu, mikutano mikuu huwa ina ajenda zake. Na inafahamika kwamba kimfumo, taratibu zinaelekeza kwamba mambo yaanzie kwenye majimbo. Je, hawa wachungaji wanaodaiwa kuwa 540 wanashiriki vikao kwenye majimbo?

2. Hili la magari hebu weka hizo evidence hapa hapa. Nilikuliza pia kama unafahamu utaratibu wa kuingiza magari kwa jina la EAGT hujanijibu. Na kuongezea na jingine, nani anayepaswa kujua na kulalamika kama magari haya yamekwepa kodi? Nilikuliza pia position ya TRA katika suala hili, hujanijibu!

3. Kuna tatizo gani kisheria kwa kanisa la mahali pamoja kuwa na TIN namba yake kwa masuala yanayohusiana na mambo ya hapo kanisani kwa kuwa kanisa la EAGT mfumo wake ni kujieneza lenyewe na hayategemei kuhudumiwa kutoka makao makuu?
4. Kwanini hamkuwahi kumuinukia Askofu Kulola kumdai mapato na matumizi kwa kuwa mkataba huo uliingiwa chini yake? Na kama ulivyoulizwa na mchangiaji mmoja kabla, ni kwani mlisubiri Mahene aanze kushughulikiwa kutokana na uzinzi wake ndipo mnaanza kuhangaika kihuni tofauti kabisa na watumishi wa Mungu?

Sasa mimi siwezi kukutafuta kwa ajili ya ushahidi unaodai kuwa nao, uweke hapa hapa kila mtu aone tuujadili!
 
Mkuu uko sahihi sana.
Mimi ni muumini wa dhehebu hili, hatukuwa na roho ya matengano kabisa hasa kipindi cha askofu Kulola. Msisitizo ulikuwa injili ndiyo maana kanisa hili likakua kwa kasi sana.
2. Lakini tulikuwa na ombre la uongozi mzee alikuwa busy na injili tu, hivyo kukaingia wajanja wajanja. Hivi sasa wachungaji walio wengi hawajaitwa wamekuja kupiga deal tu ndo kwa maana haya yote yanajitokeza.
Unataka kutuambia nini hapa? Kwamba walioenda Takukuru ndio wachungaji wenye sifa, siyo?
 
Unataka kutuambia nini hapa? Kwamba walioenda Takukuru ndio wachungaji wenye sifa, siyo?
Walioenda Takukuru qao pia wana matatizo yao. Walichofanya ni kufumua mambo yanayoendelea ndani ya dhehebu hili.
Kama nilivyosema hivi sasa wachungaji wachache sana ambao wako committed walio wengi ni masilahi. Hata baadhi ya walioenda Takukuru siyo wote wenye nia ya kujenga kuna wengine wapo kimasilahi.
 
Lakini umeshindwa kusaidia kuunyosha huu mjadala. Na nina uhakika sitakuwa nimekosea nikiandika hapa kuwa wewe huyafahamu vizuri haya mambo!
 
Unajua mkuu haya mambo yote yanatupa picha moja tu,the Church is no more.Yaani watakatifu wanashindwa kumaliza matatizo yao wanapelekana kwa watu wasio mjua Mungu! It's a shame.
 
Kulola alijua kuwanyonya wote. Toka afe kila mmoja anataka ALE keki. Kulola alikula peke yake na akajua kuwatawala kisawa sawa.
 
...Yaani watakatifu wanashindwa kumaliza matatizo yao wanapelekana kwa watu wasio mjua Mungu! It's a shame.
Umeambiwa kuna wahuni huko wanalihujumu taifa kwa mgongo wa EAGT, wewe unasema watakatifu! Ulitaka wapelekwe wapi tofauti na huko walikopelekwa?
 
Back
Top Bottom