Tajiri Bakhresa Kujenga kiwanda Cha Kusindika Mafuta ya Alizetia Kwa Bilioni 255 Malawi. Kwa Nini Hawa Matajiri Wanakimbia nyumbani Tanzania?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,109
49,811
Uwekezaji wa kigeni yaani FDI Huwa na faida Kwa Nchi inayopokea na hasara Kwa Nchi wanakotoka hasa hapa Tanzania ambapo Matajiri ni ngumu sana kuvuna pesa huko Nje na kuzileta Nchini Kwa sababu siasa zetu haziaminiki.

Inanisikitisha sana kuona Tanzania inapambana kuacha Kuagiza mafuta ya kula Nje ya Nchi ambapo Kwa mwaka tunatumia takribani Bilioni 400(uhakika wa soko) kuingiza mafuta ya kula.Matajiri ambao wangepiga jeki Kwa kuanzisha viwanda na kusaidia wakulima Wetu wanakimbia na kwenda Nchi za jirani kuwatengenezea fursa.Inasikitisha sana.

Kuna haja ya Serikali kujitathmini Kwa sera zake na siasa zetu kama zinatabirika vinginevyo watu watachuma mtaji Tzn na kwenda Kupeleka Ajira Nchi jirani huku Tanznaia ikiachwa na shida zake.

Na uhakika ukimuuliza Mzee Barkharessa atakwambia ukiritimba na sera za siasa na Utawala ambazo hazitaniriki ndio chanzo Cha kukimbia Tanzania.

Rostam aliwahi sema kwamba hata kukiwa na kesi ,Watawala wanampigia hakimu simu na anaamua Serikali inavyotaka.Hasara yake ndio hii.

My Take
Nimesikitika sana Kwa hili.

=====

Bakhresa Group has invested $100 million (Sh255 billion) to establish a vegetable oil refinery factory in Malawi’s commercial city of Blantyre that is set to employ over 500 people.

The soybean oil refinery plant, which is 70% complete, is an addition to other business interests already established by the Tanzanian conglomerate in Malawi, which includes the popular Azam wheat flour, Azam pay services, and the production of Azam washing soap, which is among the most popular products in Malawi.

The Bakhresa Group is Tanzania’s largest family-owned business, owning 30 subsidiaries and factories in nine African countries, such as Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Mozambique, Malawi, South Africa, and Tanzania, where the group’s headquarters are located.

Chanzo: The Citizen
 
Uwekezaji wa kigeni yaani FDI Huwa na faida Kwa Nchi inayopokea na hasara Kwa Nchi wanakotoka hasa hapa Tanzania ambapo Matajiri ni ngumu sana kuvuna pesa huko Nje na kuzileta Nchini Kwa sababu siasa zetu haziaminiki.

Inanisikitisha sana kuona Tanzania inapambana kuacha Kuagiza mafuta ya kula Nje ya Nchi ambapo Kwa mwaka tunatumia takribani Bilioni 400 kuingiza mafuta yet Matajiri ambao wangepiga jeki Kwa kuanzisha viwanda na kusaidia
Nimesikitika sana Kwa hili.
Wanakimbia watu aina ya Gekul
 
Nchi hii haina mfumo thabiti wa kuaminika kwa wawekezaji.
Kila rais akija ana sera zake tofauti na aliyepita.

Taifa linapaswa kuwa na sera zisizo badilikabadilika

CCM wanatukosea sana, just imagine harassment ya Mwendazake Kwa wawekezaji na wafanyabiashara, unategemea Mwekezaji yupi wa ndani ataweka pesa? Wataendelea kuja Wazungu kwenye Madini na kusema nayo.

Wawekezaji Wetu wa ndani kwenye sekta za Kilimo ni muhimu sana.
 
ccm wanatukosea sana,just imagine harassment ya Mwendazake Kwa wawekezaji na wafanyabiashara,unategemea Mwekezaji yupi wa ndani ataweka pesa? Wataendelea kuja Wazungu kwenye Madini na kusema nayo.

Wawekezaji Wetu wa ndani kwenye sekta za Kilimo ni muhimu sana.
Utawekezaje kwenye kilimo wakati wa kuuza mazao mipaka inafungwa?

Tanzania bado sio nchi bali iko katika majaribio kuwa nchi baadae
 
Mkuu moja ya kuwa Nchi tajiri ni kwenda kuwekeza kwenye Nchi masikini. Hilo ni jambo zuri sana na ni hatua kwa wafanya biashara na wafanyakazi wa Tanzania. Hapo lazima management itatoka Tanzania na cheap labour itatoka malawi.

Pia bei ya mafuta itapungua. Ingekuwa ni benki ya crdb imefungua tawi usinge sikitika kwakuwa ni mfanya biashara unaona Tanzania tumepoteza nafasi ila kiukweli ni dalili nzuri ya mafanikio. Tanzania itaanza kuheshimika. Hata ukiwa nje ya Nchi umetembelea Nchi maskini utasikia huyu ni mtanzania.
 
Mkuu moja ya kuwa Nchi tajiri ni kwenda kuwekeza kwenye Nchi masikini. Hilo ni jambo zuri sana na ni hatua kwa wafanya biashara na wafanyakazi wa Tanzania. Hapo lazima management itatoka Tanzania na cheap labour itatoka malawi.

Pia bei ya mafuta itapungua. Ingekuwa ni benki ya crdb imefungua tawi usinge sikitika kwakuwa ni mfanya biashara unaona Tanzania tumepoteza nafasi ila kiukweli ni dalili nzuri ya mafanikio. Tanzania itaanza kuheshimika. Hata ukiwa nje ya Nchi umetembelea Nchi maskini utasikia huyu ni mtanzania.
Tanzania ni Nchi Tajiri? Uwekezaji wake huo unasaidia nini Tanzania? Hukuwahi kuona Trump Alikuwa ameweka sera za kuwarudisha Wamarekani China?

Ni hasara Kwa Nchi yetu na faida Kwa Nchi Yao.
 
Hajaamua kwenda Malawi.kqa bahati mbaya,.
Bakheresa lengo lake kuwekeza bidhaa za kilimo na chakula nchi zote za Africa Mashariki na SADC kawekeza Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Kongo, Namibia na Afrika kusini ambako ana kiwanda kikubwa cha juice kuliko kiwanda chochote Afrika kwa Malawi.

Kule kawekeza miaka mingi toka enzi za Mwinyi na kwa Malawi ndie mfanyabiashara mkubwa kule hata kukiwa na maonyesho ya kimataifa nje ya nchi kampuni ya Bakheresa ndio huwakilisha Malawi.

Hakimbii Tanzania yeye mfanyabiashara wa kimataifa mtanzania kama walivyo makampuni mengi ya mafuta ya watanzania akina Lake oil, Taifa gas, Mo Dewji nk

Tofautisha kampuni za kimataifa na local companies
 
Back
Top Bottom