Taji Liundi avunja ukimya kuhusu COVID-19

Changamoto Kama hizi zinapokuja ndio mwanzo pia wa innovation... Inakuwaje mtu WA catering au mpika keki unalalamika... Inamaa wewe mpishi WA keki unashindwa kujiongeza hata kutengenezea keki ndogo ndogo au other bites Au Mikate ...wanaotengeneza hizo bidhaa zingine still they making money kama kawaida... Elewa watu wanakupunguza spending ,bidhaa zikiwa bei nafuu utauza tu.
Nani atoke kwenye home quarantine aje kununua keki ndogo ndogo? Sasa hivi mtu anaenda kununua bidhaa muhimu; Unga, mchele, sukari, maharage, dawa na nishati
 
Ahaha labda nikose bando Mkuu Ndio nitaacha kutupia

Ukiona kitoto kimekblock ujue hakina hoja ten, options ni kukimbia tu

Waambie wakue kisiasa wawe na vifua, siasa sio kunywa mbege
Sio Mimi tuu, umeona kuna watu mpaka wame kublock kwa kuchoka ujinga. Jitathmini kijana!
 
Wazee wa riziki miguuni hii kitu imetukalia vibaya, kukaa ndani na kutoka vyote ni hatari kwa uhai wako. Tunabaki na option 2 tu zote za kikatili ni aidha njaa au korona
 
Mkuu hata uendelee miaka miwili as long kwamba nafanya kazi na naingiza mapato nakosaje mshahara?? sio kwamba natamani ugonjwa uendelee, HAPANA! Ila Dharau zao kwetu watumishi wa Umma zikome kabisa
Unadhani ma biashara yakifungwa/shughuli zikasimama nyie watumishi wa umma mtakua mnalipwa mishahara kutoka wapi,kama hujaanza kusikia story za nyie watumishi kupigwa 'ridandasi',likizo za bila malipo etc
 
Usipaniki Mkuu, elewa maana yangu. Watu wengi wanaolia sasa ndio waoubeza sana utumishi wa Umma. Maana yangu ipo hapo, usijibu kwa Jazba
 
Anaandika Taji Liundi

AKIBA INAISHA.
Tunaingia mwezi wa pili sasa baadhi yetu kwenye sekta binafsi/wajasiriamali hatujafanya kazi.
Mimi ni Mshereheshaji.
Djs wangu hawajafanya kazi
Kumbi zimefungwa zote
Watengeneza cake
Wapambaji wengi wanalalamika sana.
Event Planners wanakosa kazi.
Hadi caterers wakubwa wanalia.

Nikipima mbele, napatwa hofu kwamba May na June pia zitapita tupu. Labda July na August pia. Kiufupi 2020 imeharibika kabisa.
Sikujiandaa.
Nisingeweza kujiandaa kabisa na janga hili.

*Mahitaji ya maisha hayakomi, yanaendelea. Kodi. Chakula. Matibabu.
*Najitahidi sana, mpaka sio kawaida kubana matumizi. Lakini bidhaa nyingi zimeongezeka sana bei.

Najiuliza nitafanya nini nikibaki na tuseme 300.000/ May katikati.
Nitamkopa nani?
Nitakopa wapi?

Na marafiki wengi ambao tayari wananiomba hata 30.000/ wadundulize?
Natoaje ikiwa na mimi sina mfuko mrefu?

Wewe ungefanya nini?
Nasoma nje kuhusu stimulus package ya $400/600 kwa mwezi kwa miezi 6 na jinsi waMarekani wanahaha kuipata!

Tunaona kote duniani watu wanapinga kufungwa kwa biashara. Watu wanakaidi. Wanaasi.
Hapa Dar, ukipanda Boda na Bajaj na Uber ndo utasikia malalamiko.
Ukienda sokoni au dukani. Ukienda Mlimani na kujikuta peke yako corridor nzima.

Tufanyeje?
Tutoke turisk?
Tukae bila ajira tufilisike?

Ndio maana nataka kuona takwimu za kweli.
Kila siku.

Ni namna moja ya kupima tulipo. Mafanikio ya kupunguza maambukizi. Inajenga moyo wa kwamba kuna siku maisha yatarejea kama kawaida.

Nimeshabana mkanda mpaka sipumui.
Tupeane ushauri.
usiwaze sana Taji Liundi kuna kitu kinaitwa Mifuko ya hifadhi ya jamii. soon itaanza kuihifadhi hii jamii naamini wewe na familia yako ni wanajamii pia basi MTAHIFADHIWA
 
Anaandika Taji Liundi

AKIBA INAISHA.
Tunaingia mwezi wa pili sasa baadhi yetu kwenye sekta binafsi/wajasiriamali hatujafanya kazi.
Mimi ni Mshereheshaji.
Djs wangu hawajafanya kazi
Kumbi zimefungwa zote
Watengeneza cake
Wapambaji wengi wanalalamika sana.
Event Planners wanakosa kazi.
Hadi caterers wakubwa wanalia.

Nikipima mbele, napatwa hofu kwamba May na June pia zitapita tupu. Labda July na August pia. Kiufupi 2020 imeharibika kabisa.
Sikujiandaa.
Nisingeweza kujiandaa kabisa na janga hili.

*Mahitaji ya maisha hayakomi, yanaendelea. Kodi. Chakula. Matibabu.
*Najitahidi sana, mpaka sio kawaida kubana matumizi. Lakini bidhaa nyingi zimeongezeka sana bei.

Najiuliza nitafanya nini nikibaki na tuseme 300.000/ May katikati.
Nitamkopa nani?
Nitakopa wapi?

Na marafiki wengi ambao tayari wananiomba hata 30.000/ wadundulize?
Natoaje ikiwa na mimi sina mfuko mrefu?

Wewe ungefanya nini?
Nasoma nje kuhusu stimulus package ya $400/600 kwa mwezi kwa miezi 6 na jinsi waMarekani wanahaha kuipata!

Tunaona kote duniani watu wanapinga kufungwa kwa biashara. Watu wanakaidi. Wanaasi.
Hapa Dar, ukipanda Boda na Bajaj na Uber ndo utasikia malalamiko.
Ukienda sokoni au dukani. Ukienda Mlimani na kujikuta peke yako corridor nzima.

Tufanyeje?
Tutoke turisk?
Tukae bila ajira tufilisike?

Ndio maana nataka kuona takwimu za kweli.
Kila siku.

Ni namna moja ya kupima tulipo. Mafanikio ya kupunguza maambukizi. Inajenga moyo wa kwamba kuna siku maisha yatarejea kama kawaida.

Nimeshabana mkanda mpaka sipumui.
Tupeane ushauri.
Hakuna Mpare mwenye hajui kusave japo kwa kula ugari na harufu ya dagaa..naamini una akiba lakini la msingi kuliko yote,tutoke tuendelee na kazi kama kawaida maana tunatishika sana na maneno mengi ilihali uhalisia ni mwingine. Sema tu swala la wageni kutokuingia nchini ndo inayumbisha uchumi lakini binafsi nashauli Serikali ingerudisha kazi zote ziendelee kama kawaida isipokua shule tu lakini mashirika na kazi zingine nyingi zisonge mbele tusikae watu watapata shida ya njaa

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
Hahahahaha Mpwa unajua wewe ndio unaacha bangi isiheshimiwe?? Dah umeniangushà sana
 
Usipaniki Mkuu, elewa maana yangu. Watu wengi wanaolia sasa ndio waoubeza sana utumishi wa Umma. Maana yangu ipo hapo, usijibu kwa Jazba
Jazba ipi sasa umeiona hapo?Naona wewe ndio umejibu kwa Jazba.

Hebu ngoja nikuulize ndg. Mtumishi wa Umma,hivi mshahara unaolipwa wewe na serikali unadhani hua unatoka wapi?
 
Duh! Afadhali watu wenye uthubutu, watusemee maana sisi wengine, kulia njaa hadharani ni aibu!.
P

Mkuu usijisikie aibu kulia njaa hadharani maana siku ile pale Ikulu, tuliambiwa kupitia luninga ya kwamba jina lako la Mayalla lina maanisha njaa!! Na bahati nzuri wewe ni muimini wa "Karma" hivyo huna budi kuikubali tu 'njaa' hasa wakati huu wote wa Corona.
 
Back
Top Bottom