Taja jimbo unaloona linakwenda upinzani 2025 endapo Tume ya Uchaguzi itakuwa ya haki

Vunjo, Moshi Vijijini, Moshi Mjini, Rombo, Hai na Siha mkoani K'Njaro lazima yatarudi upinzani kwani watu wa kule wanajielewa vyema. Sina uhakika sana na Same Mashariki/Magharibi na Mwanga kwani kule ni species ingine na bado kidogo u-zuzu upo.
Hivi kwanini watu hudhani Kilimanjaro ni ya wapinzani?... Hapo labda vunjo, hai, na siha ila huko kwengine wapinzani hawawezi chukua
 
Kuna majimbo lazima yatakwenda upinzani, nani kushinda wapi hiyo kwangu hata sioni kama ina maana tena, siamini kama itabadilisha chochote kwenye scape ya siasa zetu.

Mambo yataendelea kuwa vile vile tu business as usual, wapinzani wapige kelele, CCM wasikilize kelele zao, mwisho wa siku wote wale mishahara minono na posho, but nothing else will change.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
2025 ni fursa nzuri sana ya kuingia bungeni, maana CCM wameshaona wanawahitaji wapinzani bungeni, kwahiyo dizaini fulani tutegemee baadhi ya viti kwenda upinzani... tena haswa haswa wale CCM ambao wapo against mama Samia nahisi wanaenda kupotea
 
Back
Top Bottom