Tumefungwa 1-0 na kutolewa kwa jumla ya bao 2-0. Bao la Rwanda limefungwa dk. Ya 36 na kiungo Albert haya tena tusubiri mechi ya Brazil
Mechi imeisha hivi punde tumefungwa 1-0 baada ya bao lililofungwa na kiungo wa Rwanda Albert dakika ya 36 alipopiga shuti lililombabatiza beki wa Stars na kujaa wavuni. Kwa hiyo Rwanda imefuzu CHAN 2011 kule Sudan
Watu wakisema TFF bado haijapata viongozi, hatuamini. Wewe fikiria, kwa wiki kadhaa sasa watu wanaiongelea mechi ya brazil tu badala ya kuongelea mechi hii muhimu. Sitashangaa nikisikia wachezaji hawakuwa ma morali yoyote, wao wanawaza kucheza na brazil.
Hivi kwa nini tunacheza na Brazil? Au ni biashara tu?