TAHADHARI ya Mvua Kubwa Tanzania

Asubuhi imefika, mbona hakuna mvua? Ni bora TMA ikavunjwa, then tutegemee utabiri kutoka kwa maruhani wa ikulu.
 
Kwa wale wandugu mlioko mkoa wa Dar es salaam pamoja na Mtwara chukuen tahadhari kwani picha za satelite zinaonyesha kwa tar 02May hali ya hewa ni mvua asubuh mpaka usiku .

Asubuhi ya saa ngapi? hawa si walisema mvua masaa 24 kuanzia Tar 30 April. mbona sijaona?
 
kupata mvua nyingi sio hali mbaya ya hewa! ni hali nzuri sana tunatakiwa kwanza tuweke miundo mbinu vizuri kuzuia mafuriko lakini pia maji haya ya mvua yavunwe ili yatumike kwenye kilimo cha umwagiliaji! kwa matumizi ya nyumbani na hata kuzalisha umeme! inashangaza leo kuna mvua nyingi hata mpaka mafuriko kesho ukame na njaa na mgao wa umeme hivi viongozi wetu na watunga sera wanafikiri kwa kutumia nini??Leo unaachia yanenda baharini kesho unalia ukame?halafu upo kifua mbele majukwaani unatangaza kilimo kwanza???
 
Sasa kaka ulitegemea taarifa zao ziwe sahihi wakati wote ni kamlete

i said this hawa jamaa taarifa zao haziaminiki kabisa leo ni tarehe 2 hamna cha mvua kubwa wala dalili ya mvua. itafika kipindi watanzania wataanza kuwapuuza hawa jamaa
 
Tahadhari

Kuanzia: Tarehe 30 Aprili 2012 Mpaka: Tarehe 04 Mei 2012

Aina ya Tukio Linalotarajiwa: Mvua Kubwa (zaidi ya milimita 50 katika kipindi cha saa 24 kila siku)

Kiwango cha Uhakika: 80%

Eneo: Mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi, Tanga, Morogoro, Pwani na visiwa vya Unguja na Pemba

Maelezo: Kuimarika kwa mgandamizo mdogo wa hali ya hewa katika maneo ya Bahari ya Hindi yanayopakana na Pwani ya kaskazini.

Angalizo: Wakazi wa maeneo hatarishi, watumiaji wa Bahari na nchi kavu wanashauriwa kuchukua Tahadhari. Aidha Taasisi zinazohusika na Maafa zinashauriwa kuchukua hatua stahiki.

Maelezo ya Ziada: Mamlaka inaendelea kufuatilia mifumo ya hali ya hewa na kutoa taarifa kila itakapobidi.

IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Max,

Mimi hawa TMA siwaamini kabisa
 
Hao wanakopy na ku paste taarifa za cctv wanabadilisha majina ya mikoa tu! Wakikwambia kutakuwa na mvua kubwa jiandae kuanika mahindi,wakikwambia jua kali jiandae kulima au kuzibua mifereji ya maji machafu!
 
Nasindwa kuelewa mamlaka hii! siku mvua ikinyesha tu DAR ndo mkurugenzi wao anatoka kwenye TV, redio n.k kutabiri hali ya mvua hapa nchini! kwa nini asitabiri kabla mvua haijanyesha!!!!!!!!! utabiri wenyewe huwa ni uongo mtupu!, mara sunami hiyo inakuja mara mvua kubwa siku kadhaa n.k! Hivi mikoa ya TZ ni DAR tu! mbona huko Mara mvua inapiga kichizi siku nyingi mbona hasemi chochote!!!!!!!!!! Nahisi huu ni utabiri wa kiasiasa ama wa kutojiamini........kwa vile mabosi wake wako hapa DAR!!!!!!!!!1
 
Tatizo la utabiri bwana.... yaani ni kama kupiga ramli tu
Tahadhari

Kuanzia: Tarehe 30 Aprili 2012 Mpaka: Tarehe 04 Mei 2012

Aina ya Tukio Linalotarajiwa: Mvua Kubwa (zaidi ya milimita 50 katika kipindi cha saa 24 kila siku)

Kiwango cha Uhakika: 80%

Eneo: Mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi, Tanga, Morogoro, Pwani na visiwa vya Unguja na Pemba

Maelezo: Kuimarika kwa mgandamizo mdogo wa hali ya hewa katika maneo ya Bahari ya Hindi yanayopakana na Pwani ya kaskazini.

Angalizo: Wakazi wa maeneo hatarishi, watumiaji wa Bahari na nchi kavu wanashauriwa kuchukua Tahadhari. Aidha Taasisi zinazohusika na Maafa zinashauriwa kuchukua hatua stahiki.

Maelezo ya Ziada: Mamlaka inaendelea kufuatilia mifumo ya hali ya hewa na kutoa taarifa kila itakapobidi.

IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
 
Kama hiyo tahadhali imetolewa na Mamlaka ya hali ya hewa ya Tanzania then watu wala wasiogope.
Mnaweza kunikumbusha ni lini hii mamlaka ilitabiri hali fulani ya hewa na ikatokea kweli?

Mkuu hata BBC wameonyesha ukanda wote wa pwani utakuwa na mvua kubwa zikiambatana na radi. "Prevention is better than cure".
 
Back
Top Bottom