TAHADHARI ya Mvua Kubwa Tanzania

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,230
13,415
Tahadhari

Kuanzia: Tarehe 30 Aprili 2012 Mpaka: Tarehe 04 Mei 2012

Aina ya Tukio Linalotarajiwa: Mvua Kubwa (zaidi ya milimita 50 katika kipindi cha saa 24 kila siku)

Kiwango cha Uhakika: 80%

Eneo: Mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi, Tanga, Morogoro, Pwani na visiwa vya Unguja na Pemba

Maelezo: Kuimarika kwa mgandamizo mdogo wa hali ya hewa katika maneo ya Bahari ya Hindi yanayopakana na Pwani ya kaskazini.

Angalizo: Wakazi wa maeneo hatarishi, watumiaji wa Bahari na nchi kavu wanashauriwa kuchukua Tahadhari. Aidha Taasisi zinazohusika na Maafa zinashauriwa kuchukua hatua stahiki.

Maelezo ya Ziada: Mamlaka inaendelea kufuatilia mifumo ya hali ya hewa na kutoa taarifa kila itakapobidi.

IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
 
hawa jamaa taarifa zao haziaminiki kabisa. wakitangaza mvua kubwa hainyeshi hata kidogo wasipo sema inanyeesha balaa anyway tuchukue tahadhari
 
Kama hiyo tahadhali imetolewa na Mamlaka ya hali ya hewa ya Tanzania then watu wala wasiogope.
Mnaweza kunikumbusha ni lini hii mamlaka ilitabiri hali fulani ya hewa na ikatokea kweli?
 
Asante kwa taarifa na si vibaya kuchukua tahadhari. Na si vibaya vitengo vya maafa kama kile cha waziri mkuu kutoa elimu kwa umma hatua za kuchukua panapotokea maafa, maana hata hiyo taarifa inasema wananchi wachukue tahadhari....zipi?
 
skukrani kwenu jamani.xaxa ndugu zangu wa mabondeni tujihadhari basi kabla ya hatari.
Tuutumie utandawazi huu kujihadhari kama taarifa tushapewa.
LAKINI AJALI HUBEBA HADI MWENYE TAHADHARI.
 
hawa jamaa uwa wanakwenda OP, sijui vipimo vyao vinakanusha, yaani hapo ujue wanamaanisha ni jua kali
 
Mweh! Sirudi Dar, ngoja niendelee kujichimbia Mkuranga.
Asante kwa taarifa.

Inasikitisha sana mtoto mzuri kama wewe hujui kuwa Mkuranga iko mkoa wa Pwani na Max kaweka wazi hapo juu kuwa Pwani nayo imo katika huu utabiri wa hali ya hewa.
 
sasa wakazi wa mbezi watakua wakitoka kazini wanarudi saa sita usiku majumbani mwao...jamani only in bongo...
 
Asante kwa taarifa na tahadhari. Lakini tahadhari ya mvua ni siasa?

Hilo nalo neno!

Haya moderators, hamisheni hii pelekeni kwenye jukwaa stahiki au mnamuogopa founder atawafukuza kazi?
 
Inasikitisha sana mtoto mzuri kama wewe hujui kuwa Mkuranga iko mkoa wa Pwani na Max kaweka wazi hapo juu kuwa Pwani nayo imo katika huu utabiri wa hali ya hewa.

I know iko Pwani lakini huku hamna mafuriko si kama Dar, apa pananyesha lakini mswano.
 
Back
Top Bottom