Tahadhari: wizi wa ATM nimeibiwa laki 4

Hawa wafanyakazi wa mabenki fulu of Fraud nimesikia kuna kikundi cha wafanyakazi BANK M ni matapeli. wanatumia mtandao ya e mail ya BANK M kutapeli na
kujipatia pesa za wizi? tujuzeni majina yao isijekuwa ni boyfriend au girlfriend zetu.
 
zipo bank komavu kama CRDB na NBC wewe unaweka hela saccos unadhani ni bank?
Mkuu hapo umepatia, hizi "advanced saccos" tunazo zichukulia kama benki zitaliza watu wengi sana, kwa nini ATMs zao ndio ziwe na BUGS masaa yote au wananunua ATM mtumba nini?
 
Aisee kama policy zenu zimekaa namna hii, kua hakuna kulipa once kuna default imetokea kwenye ATM card, basi hakuna haja ya kuweka pesa kwenye benki zenu...whatever happened to the insurance ambayo bank inaku anayo, au haijacover losses za namna hii, maana hii pia inaweza kuwa mojawapo ya loss ambayo benki anapata, kwakua ATM imetolewa na Bank, pesa ipo bank, so kukitokea matatizo ambayo hayapo ndani ya uwezo wa mteja kuyatatua inakua ni jukumu la benki?? hamuoni kufanya hivyo ni kujivua majukumu yenu?? so likitokea tatizo nakua tena si mteja wenu??

mkuu kama hali unataka iwe hivi utakavyo si wateja wanawapa watu wasiojulikana kadi zao then wanatoa hafu wanaenda ku claim benk ili alipwe
 
ndani hawataki sasa, wanasema wanaruhusu kutoa kuanzia milioni, na sisi wenzangu na mie tumetoa pesa nyingi ni kilo

NMB mwisho kwa ATM ni laki 4,kwa siku,mimi leo imenigomea nilitaka kutoa zaidi,nilipotoa 4 ya kwanza,ya pili ikagoma,nikaenda ndani
 
Noamba ni declare interest,mim nimefanya benk kazaa na ktk idara mbalimbali.subject to this matter kuna uwezekano mkuu hapa alicommand hiyo pesa na ikahesabu haikutoka pesa hii hubaki kwenye pujbin(kifaa maalumu cha rejected notes)sasa hapa inategemea na ATM custodians wasipokuwa waaminifu hela hii wanaipiga maana vinginevyo muda kwa kureplenish ATM ambao ni kila saa kumi na mbili jion basi ATM isinge balance na over hiyo ingeonekana.kwa case kama hii wakikupa statement tu utashindwa maana inaonesha cash imekuwa debted suluhisho hapa ni ku play PVR ambapo itaonesha nani kachukua kama ni ww ama mteja aliyefuatia maana kitaalamu kama kuna jam cash inaweza chelewa paka dk 5.kwa msaada zaidi unaweza nicheck lakin punguza hasira kwa style hiyo utapoteza vyote mkuu.ikumbukwe tu benk haina dhamana ya matunzo ya kadi yako wizi wowote utakao fanyika ktk atm kwa kadi ambayo umekabidhiwa wewe benk hailipi sana sana utasaidiwa kumtafuta mtuhumiwa tu

kama kesi ni hiyo mteja inabidi adai hata kitunguu aone km kweli cash ilitoka maana kama pesa inarudi kwene pujbin lazima ile leja ioneshe kwamba cash haijachukuliwa. ila km custodian ni mpigaji bas atakuwa kabalance mfukoni mwake.
 
Nikweli mkuu me nimeibiwa 40 elf, bank NMB Tawi nzega, baada ya kutaka kutoa elfu hamsin ikatoka elfu kumi, af kufatilia transaction ndan ikaonekana 50 imetoka nisha andika barua lakin had leo wapo kimya. kueni makin jaman
 
Back
Top Bottom