TAHADHARI: Wizi kwa unaempa lift

Sasa kama Wababa wanafanyiwa hivi, wamama itakuwaje? hii ni moja ya sababu wanawake wengi hawatoi lift kwa yeyote njiani, potelea mbali acha tuonekane tuna roho mbaya tumechoka kuibiwa mapochi na vipodozi vyetu kila siku!

hivi happiness win ndio Miss Tanzania 2013 from Dodoma?
Gari hujakabidhiwa ushakula kiapo hutupi lift kwenda Chako ni Chako?
 
Last edited by a moderator:
Wadau.. Mfanyakazi mwenzangu, ameibiwa LAPTOP baada ya kuwapa lift watu watatu, mmoja akiwa ni mwanafunzi FAKE. Alikuwa anatoka maeneo ya MAJOHE asubuhi kuelekea maeneo ya Gongolamboto halafu kibaruani. Alipofika Relini, Watu wawili na mwanafunzi FAKE wakaomba lift. Jamaa alipoona na mwanafunzi yupo. akasimama na kuwapa lift.

Wale watu, walilaza kiti cha nyuma na kupata ACCESS kwenye buti ambako alikuwa ameweka Laptop. Wakaitoa kwenye BAG lake, na kuupitisha chini ya kiti cha abiria aliyeko upande wa kushoto wa gari mbele, (Mwanafunzi fake) kwani alipoingia garini, aliweka madaftari yake chini. Hivyo basi, alipofika Pugu Sec, akatelemka, na kuchukua madaftari (Counters) yake na kuunganisha na laptop ya jamaa.

Jamaa alikuja kushtuka baada ya kufika kibaruani na kuona hana laptop na alijua kaibiwa kwani zile shughuli aliziona zikifanyika, lakini hakuhisi kama ni wizi ulikuwa unaendelea. Wale wezi wawili wakatelemkia Gongo la Mboto..

Hivyo hata nyuma ya BUTI la gari sio salama tena. Dawa ni kutompa mtu yeyote lift.
Hii kitu mbaya sana, yaani unaingia kwenye gari la mtu kwa kusudi la kudokoa, kuiba au kufanya madude yako mengine unayoyajua mwenyewe,...., hii kitu mbaya sana and I hate it to the bottom of my heart. Halafu naomba siku moja nije nifanikiwe kukamata mtu kama hii, siku hiyo itanitambua hiyo mtu!
 
nampa lift ninae mfahamu tu, njia hiyo kuanzia kisarawe, chanika, pugu, majohe wizi kama huo ni mwingi sana!
 
Mi huwa napita sana Kinyerezi mwisho au Goba na huwa naota lift kwa wanafuzi sana tu, lakini kabla sijatoa lifti nahakikisha kila kitu nimeweka vizuri na kama siku hiyo gari yangu iko na vitu vingi sitoi lift.Usafiri ni wa shida sana jamani tusaidiane na Mungua atatulinda. Naumia sana especially ninapoona STK/STG zinakatisha na mtu mmoja hata hazitoi lift gari za serikali madereva na ma boss wao wanaroho mbaya sana jamani.
 
Toa tu.. Ipo siku watakutengeneza.. Siku hizi bora umpe lift SIMBA JIKE, na si Binadamu.
 
Wale watu, walilaza kiti cha nyuma na kupata ACCESS kwenye buti ambako alikuwa ameweka Laptop. Wakaitoa kwenye BAG lake, na kuupitisha chini ya kiti cha abiria aliyeko upande wa kushoto wa gari mbele, (Mwanafunzi fake) kwani alipoingia garini, aliweka madaftari yake chini. Hivyo basi, alipofika Pugu Sec, akatelemka, na kuchukua madaftari (Counters) yake na kuunganisha na laptop ya jamaa.

Duuh...drama utadhani limetokea ndani ya nyumba ya vyumba viwili...kumbe ni gari..hapo kwenye red ingekuwa mm washakoga matusi na kupgwa chini,hata maongezi unnecessary sitakagi,ndio sembuse uanze kukorokochoa vitu
 
Wapeni lift ila waambieni kwamba nitakushusha kituo cha police alafu uone
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom