KIDUNDULIMA
JF-Expert Member
- Aug 18, 2010
- 966
- 537
nawashauri vijana kote nchini hasa kwenye majimbo ambako CCM hawapui, waviache vitambulisho vya kupigia kura majumbani badala ya kutembea navyo. Hii ni kwa sababu katika maeneo hayo vijana wanakamatwa kamatwa ovyo na kuswekwa ndani. Na ukiwa ndani vifaa huachwa counter na kama kuna kitambulisho ni rahisi kwa polisi kukificha ili upoteze haki yako ya kupiga kura. Kijana kama huna kitambulisho zaidi ya cha mpiga kura bora ukachukue barua toka serikali ya mtaa ndo utembee nayo kama kitambulisho la sivyo tutapoteza wapiga kura wengi vijana kutokana na kamata kamata ya polisi. Si mmeshasikia Arusha na Mwanza jinsi vijana wanavyoswekwa ndani? Huo ni mwanzo majimbo mengine yatafuata.