Tahadhari: Kuwa makini na wachumba unaowapata mitandaoni

julius caesar

Member
Mar 20, 2015
94
27
Habari wana jamii forum,

Ngoja niende direct to the point, kuna kipindi niliwahi kuweka bandiko hapa la kutafuta msichana ambaye Mungu angependa tungeweza kuoana,bahati nzuri wasichana wengi walijitokeza wakani pm,ila mmi nikaamua kumchagua mmoja kwa sababu yeye alikuwa mdogo kuliko wote walionitafuta na pia nilitokea kuvutiwa nae.

Baada ya kuwasillana nae kwenye simu na kunitumia Picha zake,ila changamoto kubwa yeye alikuwa anaishi mkoa mwingine tofauti na mimi,nkwa hiyo hatukuweza kuonana kirahisi ila tulikubaliana mda wa kuja kuonana live,nbaada ya kupita wiki mmoja yule dada akaanza kuniomba hela ya matumizi,ila mmi nikamjibu sina.

Nlijibu hivyo maksudi kwa sababu kwanza hatujawahi kuonana live bado hatujasomana vizuri anaanza kunipiga mizinga,pesa nilikuwa nayo ya kumpa ila mwenendo wake ulinitia wasiwasi,nikaamua kuleta uzi humu kuwauliza wana jf,je ni haki kumhudumia msichana ambaye hujawahi kumuona live amekutumia tu picha na hamjasomana vizuri?

Wengi walinipa ushauri tofauti nikachukua uamuzi wa mbayu wayu "akili za kuambiwa changanya na zako",nikaweka msimamo wangu nikasema huyu dada simpi hela yangu mpaka tuonane live,siku zikaenda yule dada aliendelea kunisumbua kuniomba hela ila mimi nikawa namjibu sina na mambo majukumu mengi yamenibana.

Baada ya wiki mbili yule dada kuniomba pesa bila mafanikio ya kumpatia,siku moja nipo kazini akanitumia sms kwenye simu,akasema mimi na yeye kuanzia siku ile mahusiano basi na pia akaniambia kama nataka sababu nimpigie,nikampigia kumuuliza kwani tatizo nini nimekukosea wapi?

Akanijibu unajua mwenyewe sababu ndio nimeshaamua hivyo,mmi na wwe basi,nikamwambia mapenzi hayalazimishwi kama umeamua hivyo sawa na kutakia kila kheri,tangu siku hiyo nikafuta namba zake na sina habari nae kabisa!.

My take: Ndani ya mitandao ya kijamii kwa mfano jf,kuna utapeli mkubwa sana wa kila aina,kuna baadhi ya wasichana ukiweka bandiko humu la kutafuta mchumba wanafikiri wwe ni domo zege kwa hiyo wanaiona hiyo ni fursa pekee yakujipatia kipato,kwa sababu atakumbeleleza kimahaba kwenye simu.

Ilimradi upagawe akikupiga mzinga utoe fasta halafu ndio humuoni tena,ushauri wangu kwa wanaume wenzagu ukikutana na hali kama hiyo kuwa kama mmi usitoe pesa bila kukutana live na msichana,usiwelimbukeni wa mapenzi na kwa wadada wenye tabia hiyo mauache "no shortcut to progress" mtakuja kuishia pabaya,wengine tukitangaza nia humu tuna jielewa sio ma zombi,mjaribu kuwa seriously ni hayo tu!
 
Alie invent internet angejua visa na vimbwanga vya mitandao .....acha tu
 
kila mtua atavuna alicho kipanda hayo ndio mavuno ya mazao yakooo... wewe ulitaka asikuombe hela maisha magumu mjiniii.. ukija kichwa kichwa unapigwa abdacadabra pah pah... tafuta binti live not behind the network..
 
Pole sana mkuu.

Ila mimi huwa natoa hela kama nikiombwa na nwanamke wa mtandaoni.

Sina kesi nyingi za kuombwa pesa lakini ila wachache walio omba pesa kabla hatujaonana niliwapa na tulionana nao na mission ikakamilika.

Kwa mfano mimi wanawake wengi naokutana nao kutoka badoo na fb sana na, binafsi huwa sioni hoja ya kuwakatalia maana wanapiga vimizinga vya kitoto kama twenty au thirty, mtu akiomba hiyo najua ana njaa namtumia, sio wengi wameniomba kabla ya kuonana ila wote nilikutana nao na tukafanya mambo mengine.

Pole sana, unatakiwa kua makini sana mkuu, hongera kwa kumshtukia huyo changu.
 
Pole sana .. Dear usife moyo .. There is still innocent women in here Jf. Thanks..

ha ha ha ha. wengi wao huwa wanaichukulia kiutani sana jf ndio maana wanaanzaga kuwapiga mizinga washkaji.
lakini demu akiwa wa mizinga hata ukifahamiana nae atakupiga mzinga tu. cha muhimu ni kujitambua tu nini unataka na nini unaweza.
 
ha ha ha ha. wengi wao huwa wanaichukulia kiutani sana jf ndio maana wanaanzaga kuwapiga mizinga washkaji.
lakini demu akiwa wa mizinga hata ukifahamiana nae atakupiga mzinga tu. cha muhimu ni kujitambua tu nini unataka na nini unaweza.

Lakini dear what I don't get it is how can a woman be more interesting in money at first than anything else? This is really not good .. There are some other things to try guys (men) at first time but not to ask for the money kwa MTU hata haujaonana nae .. Ni kujishusha hadhi ati .. agghhrrr . Some women hata siwaelewi kwa kweli . Kumpima mwanamme Mara ya kwanza sio kumpiga vibomu . Kuna other ways.. Jamani .. Thanks..
 
Lakini dear what I don't get it is how can a woman be more interesting in money at first than anything else? This is really not good .. There are some other things to try guys (men) at first time but not to ask for the money kwa MTU hata haujaonana nae .. Ni kujishusha hadhi ati .. agghhrrr . Some women hata siwaelewi kwa kweli . Kumpima mwanamme Mara ya kwanza sio kumpiga vibomu . Kuna other ways.. Jamani .. Thanks..

Embu nipime mie basi
manake jina lako limenivutia
 
ulius caesar

Uliacha nazi nzuri ukachagua koroma, kilichokuzuzua ni udogo wake ambao hata hivyo hukuuthibitisha na hata hizo habari za kuwa yuko mkoani bado ni ngumu kujua ukweli wake
Kuna mabandiko humu ndani watu wamepata wake/waume wema kabisa humuhumu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom