Tahadhari kuelekea christmas na mwaka mpya

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Nov 30, 2008
1,518
22
Shamrashamra za SIKU KUU ZA Christmas na mwaka mpya zimeanza.

TAHADHARI INAHITAJIKA,

1. Vibaka sasa wamejiweka tayari kuwakwapua watu simu zao za

mikonomni na vitu vinginevyo.

2. Matapeli nao wakijua kuwa watu wanahitaji pesa za matumizi,

wametunga mbinu nyingi kuwahadaa watu kwa kisingizio cha

kuwajaza mapesa.

3. Madereva wengi wasiorasmi sasa wanaendesha vyombo vya

usafiri kwa lengo la kupata pesa za chapchap.Hawa ni rahisi

kusababisha ajal.

4. Kumbi zinazoitwa za Starehe zinaandaliwa kufanya

maonyesho kama walivyofanya kule Tabora na kusababisha vifo

lukuki vya watoto.Wanastarehe hao husema ''KUTAKUWA NA

DISCO LA KUFA MTU '' na kweli watu hufa eidha kwa

kuambukizwa virusi au kwa tukio kama lile la Tabora.

Je hizi ni kumbi za starehe au ni kumbi za vifo?

NASHAURI,

1. Watu tuwe makini kwa kila tukifanyacho.

2. Vyombo vya usalama viwe makini katika wajibu wao.

3. Waumini tumwombe Mungu atuepushe na athari mbaya zozote.

4. Sikukuu zitumiwe kwa kusudi halisi na siyo makusudi bandia.

5. Watoto walindwe wasiingie katika uharibifu unaoitwa starehe.

EXAUD JOHN MAKIYAO
+255784347001
makyaoexaud@yahoo.com
 
Back
Top Bottom