Tahadhari kali kwa nyote mlio na magari binafsi; chunga sana na waambie wengine!

Hapo kwenye malori nimepapenda ki ukweli kwenye safari zote nilizosafiri madereva wa malori wamekuwa na msaada sana kwangu kwa kunipa ishara ya indicator na hata nilipokuwa na wasiwasi wa ku overtake dereva wa lori alitoa ishara ya mkono kuniambia nipite mambo shwari na wakati mwingine huwa wanatoa ishara ya mkono usi overtake kama akikupa ishara ya indicator na bado ukawa una force Ku overtake big up madereva wa malori, ila kingine nilicho note wakati nasafiri na basi nimegundua kuwa madereva wa malori na wa mabasi ni kama paka na panya hawapendani wawapo barabarani hata kama basi lina overtake Lori , ni ngumu sana mtu wa lori kumpa ishara dereva wa basi sijajua tatizo ni nini .


Hahahah...Mkuu, hawa jamaa hawapendani kwa sababu madereva wa Basi huwafanyia fujo wenye maroli na wanachukia sana. kwa mfano, basi akimkuta mwenye semi- lazima ampigie honi kali na kulazimisha overtake. Mabasi ya BM ndo wanaendesha rafu sana.
 
Somo zuri sana, umenikosha pale ulipotaja matumizi ya Red Bull tena zisidizi mbili maana ndio style yangu hiyo nikiwa na safari ndefu peke yangu.
 
Nilikuwa najiuliza ni kwa nini drivers wa F1 akina Hamilton, Alonso nk wanafanya sana mazoezi ya kukimbia na kuendesha baiskeli , ni kuongeza uwezo wa uvumilivu/kutochoka haraka barabarani ,
...kabisa...endurance!
 
Hapo kwenye malori nimepapenda ki ukweli kwenye safari zote nilizosafiri madereva wa malori wamekuwa na msaada sana kwangu kwa kunipa ishara ya indicator na hata nilipokuwa na wasiwasi wa ku overtake dereva wa lori alitoa ishara ya mkono kuniambia nipite mambo shwari na wakati mwingine huwa wanatoa ishara ya mkono usi overtake kama akikupa ishara ya indicator na bado ukawa una force Ku overtake big up madereva wa malori, ila kingine nilicho note wakati nasafiri na basi nimegundua kuwa madereva wa malori na wa mabasi ni kama paka na panya hawapendani wawapo barabarani hata kama basi lina overtake Lori , ni ngumu sana mtu wa lori kumpa ishara dereva wa basi sijajua tatizo ni nini .
Ni kweli mkuu madereva wa malori kiujumla ni wastaarabu sana.
Kimsingi madereva wa malori hutumia engine power au torque na stability ya mzigo barabarani, wakati mabasi mxigo ni mfoho sana kulingana na power ya engine.
Hivyo basi madereva wa mabasi huishia kukimbiza sana magari kwani hata likijaza full capacity na power ya engine bado inadai.
Kulikuwepo na ule utaratibu wa kuweka speed governors, lakini seriksli ilishindwa kusimsmia hilo.
Hata baada ya huu mgomo wa madereva, cheki ajali xilixotokea katika siku mbili tu, mabasi yamehusika karibu ajali zote.
 
Mleta mada ubarikiwe mnoooooooo

Katika ujumbe mzito na makin niliondoka nao hapa na nawiwa kuufanyia kazi ni BE PATIENT.

huwa nina fujo na haraka zisizoisha
 
To be more and more safe....hili wengi hawajui kwa sbb za kiufundi...
👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

Jaza tairi zako na upepo wa NITROGEN....!!!!!!

FILL UR TYRES WITH NITROGEN....esp for long routes za
mikoani....utaokoa maisha yako kwa sana tu...!!!

Most tyres, 75% bust ni sbb za kuexpand saana kwa hizi hewa za kawaida tunazojaza...tairi zinapopata moto
sana barabarani hewa ya kawaida tunayojaza ina expand sana na kusababisha tyre bust....ILA NITROGEN WILL NEVER EXPAND...hivyo kuwa very safe...mm magari yote hutumia hewa hii ya NITROGEN ktk matairi ...inapatikana katika baadhi ya shell kwa bei kama ya kawaida..kwa tairi moja ni sh.400.....

Ikiwa utakosa hiyo Nitrogen...na itakubidi usafiri mkoani....basi punguza tyre pressure by 10% ...if tyre pressure ya gari yako inatakiwa 36psi...then 36 - 3.6 = 32.4psi...alafu nenda safari yako...!!! Make sure gauge ya tyre pressure inasoma vema...ni vizuri ukanunua gauge yako..ni bei rahisi sana....

Hili ni muhimu sana kwa matairi, mengine yamesemwa...

👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆

Mbuuutaaaa cjawahi skiaa hyooo. Asante mkuu. Kwa hyo cku nikienda kujaza upepo niulizie upepo wa nitrogen
 
Madereva wa mabasi ni wa hovyo sana mkuu huko mbugani, na kuthibitisha hilo fuatilisa ajali za mabasi na malori, utakuta kama si mara zote , mabasi mawili au matatu yana overtake lori , na basi lile la mwisho ndio hupata ajali ya head-on maana yeye hakuona kilicho mbele.

I am saying this from experience.

Katika safari zangu nawakwepa kabisa mabasi hivyo safari zangu huanza saa 10 au 11 kabla hao wenda waximu hawajaingia barabarani.
Kwa vile wao husafiri hizo barabara wanajiona kama wana hatimiliki, wakwepe.
View attachment 242361

Dadeki hapo lazimaaa jasho na machoz yalitokaaa na kahaja kadogo kwaaa mbaaaaliiiiiiiij
 
attachment.php



Ndio maana ajali haziishi na zinazidi siku hadi siku
 
Asante Mkuu. pole na wewe pia. tulisalimika, ingawa nilikaa more than two months sijitambui. ilinichukua muda sana ku-recover na kurudi kwenye hali ya kawaida. naheshimu sana matumizi ya barabara, ndo maana nikiwa barabarani huwa sina story na mtu. wala siwezi kuweka muziki mkubwa, kwani any noise or disturbance of any nature, inapunguza umakini barabarani. nikiwa speed huwa napenda kusikiliza mlio wa engine ya gari nayoiendesha na tairi zinavyokanyaga. niliwahi kufanya pilot studies nchi fulani, na kwenye mambo ya anga, a single mistake, inagarimu maisha. hivyo hata barabarani i deploy the same principles....!! jambo jingine, udereva wa kujihami ni muhimu sana. aina hii ya udereva inaokoa maisha kwa takribani 50%.

Ila kusema ukweli, hapa Dar es salaam, asilimia 90 siyo madereva. i wish thread hii iwafikie kokote waliko.

Kuviringika na gari mara tano sio jambo dogo, hata hivyo tunafurahi tuko pamoja bado hata tunakutana umu JF.

Hili la kusema madereva wa Dar karibu asilimia 90 sio madereva, napenda kuliangalia pia upande wa pili, kwamba madereva wa Dar ni wachache sana wanaweza kuendesha gari manual.

Unajua siku hizi wengi wanachukulia kuendesha gari ni usukani, breki na accelerator. Mie nadhani ni jambo zuri kila mtu aliye dereva ajifunze au ahakikishe anaweza kuendesha gari ya manual gear pia. Nadhani kuna advantage fulani katika kujua jinsi ya ku-handle gari na kulimudu ikiwa unajua pia kuendesha gari ya manual gear. Zamani ukienda Polisi ku-test ilikuwa lazima utumie gari ya manual gear, sijui siku hizi.
 
Asante kwa somo. Ni kweli kabisa kuwa madereva wa mabasi wengi wao uendeshaji wao ni wa hatari sana. Sijui waelimisheje ili wabadilike
 
Somo zuri sana, umenikosha pale ulipotaja matumizi ya Red Bull tena zisidizi mbili maana ndio style yangu hiyo nikiwa na safari ndefu peke yangu.

Mkuu ukinywa Redbull zaidi ya mbili ni hatari sana. In fact pale niliposema sio zaidi ya mbili nilimaanisha katika safari yote au kwa siku!
 
Mkuu Synthesizer,
Nakubalina na wewe kwa yote uliyoyaandika lakini napinga ushauri ulioutoa kwa watumiaji wa Automatic Gear Box Cars kwamba wanapaswa ku-downshift from D to 2 na ku-switch off Overdrive. Siyo kweli kwamba ukishift gear selector from D to 2 na kuswitch off overdrive gari inajenga spidi ya ku-overtake.

Ukweli ni kuwa ukishift to 2 maana yake umeicomand gear box itembee na gia namba moja na namba mbili tu. Aidha, unapoweka overdrive off maana yake umezuia overdrive gears na zenyewe kuwe engaged hata kama zilipaswa kuwa engaged. Shifting to 2 gari inakuwa nzito matokeo yake dereva anakanyaga mafuta mengi huku gari ikiendelea kuishia hadi kwenye gia namba mbili hata pale ambapo ilipaswa gia namba tatu na nne ziingie ili kupata acceleration kubwa zaidia. Matokeo yake you will suffer from poor fuel consumption and even gear box damage kama dereva ataendelea kukanyaga mafuta zaidi kwa kutegema atapata acceleration kubwa wakati amelimit gear box isiingie gia zaidi ya namba moja na namba mbili.

Gear shift position 2 and D1 zinatumika kama dereva anashuka mlima mkali kwa kuwa zina-act as engine brake. Aidha, kwenye maeneo yenye matope na mchanga mwingi kwa kuwa maeneo hayo yanahitaji gari kuwa nzito ili kupata traction ya kutosha.

Kwa hiyo tunavyotaka ku-overtake with automatic gear box car you just leave your car to select the proper gear depending on the condition available at that moment. Gari haiwezi ku-hold gear namba 5 wakati tayari imeshasense spidi ya gari, RPM na throttle position vimeshuka. Itadownshift to lower gears automatically kulingana na hali ilivyo na utapata tu acceleration inayotakiwa. Ni hayo tu mkuu.

CC: Goodrich, TCleverly, etc.

Very well said, ishu ni kusafiri safari ndefu na kama you think unapenda ku-overtake ovyo basi safiri na powerful engine car sio kuovertake na vipasso na visuzuki kei
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom