Tahadhari: ijumaa kesho si ajabu ikawa na vurugu kubwa.

Status
Not open for further replies.

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Kwa mtazamo wangu, kufuatia kukamatwa na kufikishwa mahakama leo kwa Ponda na wenzake na kukosa dhamana, si ajabu, kesho baada ya swala ya Ijumaa, yakazuka maandamano makubwa kushinikiza Ponda na wenzake waaachiwe huru.

Mtazamo huu, unaenda sambamba na kauli ya kamanda Kova, kuwa hawataruhusu watu kuvunja sheria za nchi.Kitakachotokea bila shaka ni mvutano kati ya waislamu na jeshi la polisi na hatima yake kila mtu anaijua kwani tumeshashuhudia ktk majukwaa ya kisiasa matokeo ya kupimana ubavu kati ya polisi na raia.

Kwa hali ilivyo hivi sasa, ni vigumu kuamini kama waislamu wataridhika Ponda na wenzake kunyimwa dhamana.Haya ni matokeo ya kulea uovu kwa muda mrefu kwani hatua zilipaswa kuchukuliwa mapema kabla hali haijawa kama ilivyo sasa.
 
Wengine tuntaka amani bwana. Weekend yote tuanze kupigana bila sababu tumekosa nini?
 
Kwakweli TZ tumekosa mambo muhimu ya kufanya. Huu naamini ndo mwezi ya HIJA...sasa inakuwaje?
 
Thubutu!!! hatari itoke wapi ilhali nchi imeshakabidhiwa kwa Malaika Walinzi, kwa usimamizi wa Bikira Maria, Mama wa Huruma!
ni MALKIA WA AMANI! atatupigania mpaka mwisho! HATAKUBALI KUONA NCHI INAINGIA VITANI, kwa wakatoliki, tusali rosary yake, ni mwezi wa rosary huu!
 
kuna taarifa nimezipata kuwa kesho baada ya sala ya Ijumaa kutakuwa na maandamano ya siku 7 mfululizo hadi ponda na wenzake waachiwe huru
 
Kwakweli TZ tumekosa mambo muhimu ya kufanya. Huu naamini ndo mwezi ya HIJA...sasa inakuwaje?

Hv ww unaweza kwenda harusini na mkeo then jamaa wakamchukua mkeo utanyamaza kwa kusema ni siku ya harusi?
 
naona vijana wa kova wanapiga jaramba!!!!!, wanaandaa flying objects, na vitu vizito vyenye ncha kali,

tuone nani kidume hiyo kesho atakae vuka utepe mwekundu.
 
Ni kweli mkuu,kesho njini kunaweza kusiwe salama sana.Shule za mjini kama St.Joseph wamefunga shule kwa siku ya kesho.Tahadhari ni bora kuliko kusubiri litokee baya.Hawa watu walipoandamana kushinikiza waliokataa kuhesabiwa waachiwe na wakaachiwa ndipo jeshi la polisi lilipokosea,sasa wanajua kuwa wanaogopwa so wakiandama tu wanaweza kutoa shinikizo.Ila kwa mkwara wa Kova aliotoa jana,nina wasiwasi kesho PATACHIMBIKA so stay mbali na city centre.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom