Kiranja, asante sana kwa mnyumbulisho wako uliosimama wima. Mimi nipo hapo nilipo paonyeshaKiranja: Huu ni sehemu ya ushahidi mkubwa kuwa Spika wa Bunge huwa hafuati kanuni katika kufanya maamuzi yake , na hivyo anapaswa na yeye kufanyiwa kazi kwa mujibu wa kanuni za bunge kifungu cha 134 ambacho hakihitaji hata saini za wabunge ila ni mbunge mmoja kuwasilisha taarifa hiyo na hatimaye atapigiwa kura na theluthi mbili ya wabunge.
Nafikiri, kuna haja sasa kwa wananchi wetu kila mmoja akawa anawaelewesha kuhusiana na kanuni na sheria mbalimbali ili pindi wanapopotosha basi wakutane na wananchi ambao wanaelewa