Tafakuri: Nahodha huyu anaungwa mkono na nani?

Wanasema huyu nahodha haendeshi meli, ila meli inaendeshwa kutokea kule kunako mkataba wa mchina.....
Lkn yule wa kwa mchina mbona alikuwa kipenzi cha watu na demokrasia? Itakuwa huyu nahodha katengeneza "utawala mchanyato"
 
Anaungwa mkono na Vasco dagama na mtandao wake!!Na vasco keshaanza harakati za kupenyeza ikulu vijana wake na turufu kaianzia yanga kama platiform !!Tusubiri tuone!!!
 
Atakuwa anajaribu kukonga nyoyo za kila abiria waliomo ndani ya meli.....
Approach hii ya kutaka kufurahisha watu wote huwa inapelekea watu wengi kununa.

Lazima achague upande ambao ataufanya unune ili wengi wafurahi.
 
Approach hii ya kutaka kufurahisha watu wote huwa inapelekea watu wengi kununa.

Lazima achague upande ambao ataufanya unune ili wengi wafurahi.
Boli posesheni inaonyesha wapiga dili wanamiliki mpira kwa asilimia 80, wanyonge wana 20 percent...
 
Unaidanganya nafsi, haya bhana
Mimi sina ushabiki wa vyama.
Mwanzoni JPM nilimwona yuko ok. Lakini nikaja kushuhudia anavyowaonea wa vyama vingine nikasema hii hapana. Wale ni watanzania kama alivyo yeye, asijipe yeye haki zaidi ya mtanzania mwingine kisa anamiliki vyombo vya dola. Halafu ikawa tabia ya kutishwa ujinga mitandaoni. Watu wamefungwa sana kwa kukosoa utendaji wake. Huu ni uonevu.
Mimi sipendi uonevu hata kidogo.
Siwezi kukushabikia ukiwa mwonevu.

Hivyo sijidanganyi ,nimezaliwa hivyo, mke wangu ,wafanya kazi wenzangu na ndugu zangu wananijua kwa hilo.
Najijua pia.
Popote penye uonevu siungi mkono. Nifuatilie vizuri.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Nahodha ananikumbusha nesi mmoja utotoni pale ocean road anakupiga sindano na wakati unasikilizia dawa inaingia kwa uchungu yeye anakwambia poleeeee kwa sauti moja laini.

Muda huo huo vidudu vya malaria vinakufa vyote, mama ana sauti fulani tamu na ya kiungwana.
 
Nahodha Wa sasa wengi tunampenda sana!
Mimi namheshimu sana kwa open mind yake na ustaarabu ambao naona ni kipaji,...Kwenye utendaji bado sina muda wa kutosha kutoa comment

Weakness moja naiona ni kutoamini kama sisi tunaweza....Maneno haya ya wawekezaji wa nje "tunawahitaji" kuliko sisi kisiasa ni hatari sana maana watamtumia kwa faida yao....wao tunawahitaji kama ambavyo wanatuhitaji...Tunahitajiana ila ili sisi tufaidike lazima watu wetu walindwe na mlinzi namba moja ni yeye...Akiachia mlango wazi na kuwaalika pasipo kuchuja who is for us and who is against kwakua tu tunawahitaji zaidi anatuweka sisi hatari kupokwa na tusio wajua...Huu ni ushauri wangu kwake!
 
Yule wa kipindi kilee, aliyependa kusafiri kama Vasco da Gama aliungwa mkono na walioitwa wanamtandao.

Na yule aliyekuwa akipenda kazi na kuongea kwa kujiamini sana aliungwa mkono na abiria waliouchukia ufisadi. Japo baadaye huyu nahodha alibadilika na kuwa katili asiyeelezeka. Akachukiwa na watu wote wakiwemo wa boti yake mwenyewe.

Lakini huyu wa sasa anaungwa mkono na nani? Kwanza kaingia kwa bahati mbaya. Na siyo siri tena kwamba kundi kubwa ndani ya boti yake mwenyewe halikumtaka awe nahodha. Sababu zilizotolewa na kundi hili ni mbili...1. Udhaifu wa kijinsia 2. Anatoka upande wa wachache.

Salama yake ilikuwa ni kuungana na wale wengi waliokuwa wakikwazwa na ukatili na majivuno ya yule nahodha aliyetwaliwa. Lkn pia angepatana na manahodha wa boti shindani.

Haya yangemsaidi kuzima figisu za ndani ya boti yake. Na kumpa uimara ktk unahodha wake

Lakini kwa kuwa kaingia kwa bahati mbaya, hapendwi hata na wale wa boti yake mwenyewe na anarudia makosa ya nahodha aliyetwaliwa basi anajiweka kwenye hatari ya kushindwa kazi mapema sana.
Ajihuzulu basi
 
Back
Top Bottom