Tafakari ya mwaka tuisome wote

Edson

JF-Expert Member
Mar 7, 2009
9,846
5,076
Natumai wote hamjambo wanajamii wenzangu!

mwaka 2009 ndo unaeleka ukingoni, ni siku chache zimebaki kabla mwaka huu haujaisha na kuukaribisha mwaka mpya 2010. Kuna baadhi ya watu wanasema mwaka unaisha mwezi huu wa 12 lakini mwaka ulianza kuisha januari mosi na sasa mwaka unakamilisha safri yake ya miezi kumi na mbili.

kuna mengi miongoni mwetu tumefanya mengya mwaka huu, kuna changa moto nyingi tumekutana nazo. lakini kuna wengi mpaka sasa hatuoni tulichofanya yaani tangu mwaka uanze mpaka leo au pengine tumefanya kiasi kidogo na kupata mafaniko kidogo.

Nawaomba wana jf wenzangu mwaka ujao uwe mwaka wa mafanikio kwa kila mmoja wetu, tufanye kazi kwa maarifa, tujitume na tuthubutu kufanya kile ambacho kiko ndani ya uwezo wetu. tuweke akiba kwa kile tunachopata, naomba tusiwe kama wawindaji.

Muwindaji ana tabia moja, anaweza kwenda porini kuwinda, anashinda siku nzima porini anawinda , anafukuza pengine swala.siku nzima inaisha akiwa porini na jioni ikifika anarudi nyumbani na swala mmoja begani. sasakinachoshangaza sana au kibaya zaidi ni kwamba swala huyu huuawa na kuliwa,then kesho asubuhi tena muwindaji hurudi porini kuwinda. hali kama hii ikiendelea sikiu moja atarudi nyumba mikono mitupu maana aliwawinda na kuwauwa wote. Nawaomba tusiwe kama wawindaji.

Kuna baadhi yetu hatuna tabia ya kutunza faida au kile tunachokipata mwisho wa mwezi,hatauna utaratibu huo, yaani wapo baadhi yetu mishahara huwa haikutani toa mwezi mmoja kwenda kwenda mwezi mwingine.na ukiangalia hakuna kitu cha maana kilichofanyika, hakuna balance yoyote iliyohifadhiwa mahali, kwa hiyo mwezi ukiisha na mfuko unakuwa tupu. kwa hali hii maendeleo hayawezi kuja.t utakuwa tunalalamika tu lakini wakati mwingine tunajitakia matatizo.Fanya kazi, save pesa then wekeza kwenye kile unachoona kina tija kwako.

Kitu cha msingi ndugu zangu wana jf katika maisha ya mwanadamu ni KUJITAMBUA kuwa wewe ni nani, kama hujitambui maisha yako yote utakuwa ni mtu wa kushangaa tu juu ya kile wenzio wanafanya, '' dah jamaa kajenga nyumba?! duh amenunua gari?! dah jamaa ameoa? kaolewa? amenunu kiwanja?! nk nk. Yaani upo upo tu wakati wenzio hao wanafanya hayo na wewe una nafasi kabisa ya kufanya hayo,na uwezo unao, lakini tatizo ni kuwa hujitambui, huna malengo, hakuna saving yoyote, mishahara haikutani. hali kama hii ikiendelea utakuwa mtu wa kulalamika na kuwasingizia wenzio kuwa ni wezi, haiwezekani huyu akafanya hivi wakati kipato namzidi!.

mwaka 2010 kuna uchaguzi hapa nchini, kama nafsi yako inakutuma kumchagua mtu flani kwenye nafasi flani, fanya hivyo. kama huoni mtu anaefaa ni bora ukakaa kimya huku ukiendela na shughuli zako za kila siku. usiilazimishe nafsi ukampa mtu dhamana ya miaka mitanoambayo unajua kabisa kuwa huyo unaemchangua aidha hana uwezo, au kwa jinsi tabia yake ilivyo atalihilikisha taifa.

Mwisho kabisa nawatakia kheri ya x-mass na mwaka mpya kwenu nyote na famila zenu, Mungu awabariki sana.
 
jamani kwanini mabandiko yenu yanakuwa marefu hivi kama magazeti ya MZALENDO!jaribuni kuweka summariiz zinazovutia pia kuzisoma
 
jamani kwanini mabandiko yenu yanakuwa marefu hivi kama magazeti ya MZALENDO!jaribuni kuweka summariiz zinazovutia pia kuzisoma

Kwani hii haijakuvutia kuisoma ? Pengine mambo aliyobainisha mwandishi yamekugusa pabaya; kama ni hivyo utafaidika ukifuata ushauri wake la sivyo waache wengine wanufaike!!
 
Back
Top Bottom