BIF
Member
- Aug 2, 2012
- 47
- 10
Ebana mi naomba mnipe mawazo juu ya ili swala la interview kufanyika kwa lugha ya kigeni(English) Wote tunajua fika Watanzania walio wengi icho kizungu ni cha kubabaisha babaisha na hii ni kutokana na mfumo wetu wa Elimu ulivyo, wengi wetu tumepitia kwenye izi shule za wakina "kayumba" na Sec vilevile tulikua tunaongoza kuvaa lile bango la Swahili speaker.Uwa nalitafakali hili alafu nashindwa pata jibu ina maana kigezo hasa cha kujua kua uyu mtu yupo sawa kwenye hii fani flan ni icho kizungu?.Twende kwenye ivi vyuo vyetu vikuu, wanafunzi walio wengi iicho kimombo hawakijui ipasavyo kama wabisha nenda kafanye Analysis chuo chochote kile utakuja kubaliana na mimi, sasa kama ni ivi kuna aja gani hasa ya kuwafanyia watu interview kwa lugha ya kigeni? na kama kuna ulazima basi huu mfumo tulionao sasa ubadilishwe watu wawe wanatumia kizungu toka vidudu(chekechea) na kuendelea sio mara shule ya msingi kiswahili tupu Sec kingereza.Kwa matazamo wangu wapo watu wazuri wenye sifa na uwezo wa kufanya makubwa katika Nchi hii lakini walishindwa shule (kufaulu)huko masekondari kwasababu ya Lugha, unajua swala la kuklemu si la mchezo nakumbuka wakati nipo "O level" mambo yalikua mazito mtu unashinda ukiimba definition ya History na masomo mengine, ebana huku ni kama kutesa wanafunzi wa kitanzania na ndo matokeo yake tunapata makanjanja kwenye kila kona kwasababu wengine waliibia ibia tu kwenye mitihani.Wengi wanashindwa majalibio kwasababu ya lugha kujieleza kwa kizungu shida tupu ila mwambie kwa kiswahili atajieleza mpaka kesho.Sijui wenzangu mnalionaje ili?