Tafadhali tukumbushane ya kibohehe sekondari.

Kyachakiche

JF-Expert Member
Feb 16, 2009
983
207
Ndugu wadau,
Nawaombeni kwa wale waliopitia shule ya Sekondari Kibohehe watukumbushe yale yaliyokuwa yanajiri kipindi hicho hasa miaka ya mid and late 80's. Mnakumbuka uhasama wa Kibohehe na Kolila Sec na nini matokeo yake? Vipi ikitokea kuna trip ya kwenda kucheza muziki na Sec za akina dada au wao waje Kibohehe? Mnamkumbuka TJ Martin, Visimbo vya kwa Masawe pamoja na miziki ya raggae je? Vipi Chief cooker mzee Jack, bila kumsahau yule mpiga chapa mwanaume sikumbuki jina lake kwa sasa, Mbege ya Kirikiri na Miwa kule Kware? Mwalimu Gentleman na msemo wake 'SICHEZI NA KUKU! Vipi Mbosho parishi na Sokoni kwa Sadala siku za Jumamosi! Mwalimu Ndano wa Physics bila kumsahau Machambizi na chupa yake ya gongo mfukoni! Banda la njiwa karibu na ofisi H/ Master bila kusahau mashamba ya kahawa ya Kibo na vyoo vya kuvulia mashati nje kutokana na harufu kali. Tukumbushane majina ya Mabweni kama KNCU, NIMERI, SAADATI, MOBUTU, NYERERE, HAILE SELASIE...., Ama kweli machozi yana....., nakukaribisheni wakuu kuchangia. Nini umekumbuka au kimekugusa?
 
sisi tulikuwa tunaamini eti mzazi wako kama hakupendi ndio anakupeleka kibohehe ukasome,i guess this was not true but back in the days watu waliamini hivyo
 
Mkuu ni kweli wengi waliamini hivyo, lakini kwa wasiojua pale vimetoka vichwa vingi ambavyo vimekuwa kwenye level ya Uwaziri, Wabunge, Wakurugenzi wa Idara nyeti tu Serikalina na kwenye mashirika ya umma. Nasubiria michango ya waliowahi kupita pale ndipo wengi wataamini kwamba hizo zilikuwa hisia tu.
 
Duu, hiii shule na jina ni Kiboko. Kijana wangu mmoja alisoma hapo miaka ya 80 mwanzoni na ni kweli yeye na kundi lake wamefika mbali saana kwa sasa katika international level. Nafikiri wanafunzi huwa hawapendi shule zinazohimiza kusoma saana. Na Wachaga wako zaidi kwenye kutafuta pesa na si kusoma Newton's law.
 
Nashukuru mkuu kwa ushuhuda wa mwanao aliyewahi kupita pale. Kwa taarifa zisizo rasmi nilizo nazo, katika bunge la sasa kuna wabunge wasiopungua wanne walipita katika shule hii.
 
Duuu: Nakumbuka watu waliokuwa wakilala mabweni yaliyoangalia uwanjani wakiangalia na kusubiri kitolori cha mpishi nadhani alikuwa akiitwa kidish lina nini siku hiyo. Eee bwana wewe mimi mwaka wetu zilitokea div zero nazani kama 120 out of 280. Na div 1 ya kwanza baada ya miaka mingi.Form 1 ilikuwa ikitokea aluta(kugombea msosi)walikuwa wanakuja nyuma wanakunywa mchuzi.Mwalimu mkuu(Muhindi) TJ Martini=Teri gandi Che Martini,watu walikuwa wakigoma lazima akimbie,maana hajui yatakayomkuta. Akaja mwalimu Malya 2nd Master,huyu ilikuwa ukitoroka unakimbia umefunika kichwa, yeye anakukimbiza na piki x2 kwenye migomba,ilikuwa akiona kisogo tu,anakuita jina. Mtu aliyepita Kibohehe hawezi kushindwa maisha na akienda Jeshini au Ukonga ni kama kapelekwa Hostel. Nasikia Kiongozi wa migomo siku hizi ni mbunge. Ni kweli wako viongozi wengi serikalini na bungeni,nikiwemo mimi-ahaaahha. Mengine baadae.
 
Mkuu umenikuna sana, mpishi alikuwa anaitwa JACK. Yule 2nd Master Mallya alikuja kuwa katibu wa Bakwata Mkoa wa Kilimanjaro. Aluta kaka zilikuwa za kugombea BONDO(Ugali). Mabweni yaliyokuwa yanaangalia uwanjani ni KNCU na Nyerere.
 
Nashukuru mkuu kwa ushuhuda wa mwanao aliyewahi kupita pale. Kwa taarifa zisizo rasmi nilizo nazo, katika bunge la sasa kuna wabunge wasiopungua wanne walipita katika shule hii.

Kyachakiche,

Kijana wangu nilikuwa na maana RAFIKI YANGU na si Mtoto wangu. Tumezoana kuitana hivyo na nilipoandika nilikuwa namaanisha hivyo kiasi kwamba kama akija kusoma ataahamu ni mimi tu. Mie na yeye nafikiri tumezaliwa mwaka mmoja na wow, tunafahamiana sasa zaidi ya miaka 17. Yeye ni mwenyeji wa Mbokumo..... yes, my kijana Kambaboy.
 
Sikonge,
Hapo utakuwa umenirudisha darasani! Any way, nafurahi tuko pamoja ingawa nafikiri huyo rafiki yako ni wa MBOKOMU na sivyo kama ulivyoiweka hapo juu.
 
huyo headmaster martin nasikia wanafunzi wanamkunja wanamnyaganya ada na kuhama shule
Nilisikia Bakwata walipata msaada wa Kielimu chini ya IOC na kupelekea apelekwe H/Master mpya kutoka Ghana pamoja na waalimu kutoka Uganda. Huo ukawa mwisho wa TJ Martin na 2nd Master Mallya kuhamia Bakwata Mkoa kama Katibu.
 
Back
Top Bottom