Nimepokea simu na email ambazo zinanipa wasiwasi na hofu

professional ethics

Senior Member
Dec 24, 2023
108
352
Wakuu mdogo wenu nipo njia panda, Jana usiku sasa tatu kamili nime pigiwa simu na mwanamke aliejitambulisha kuwa ni mkurugenzi wa shule moja binafsi hapo jijini Arusha (jina nimelitunza O level hadi A level), lengo la simu yake amenambia kuwa wananihitaji katika shule yao mara baada ya kumaliza masomo mwaka huu (nipo mwaka wa tatu hapa DUCe, nachukua Bachelor of Science with Education, Biology na Chemistry).

Baada ya kumuuliza namba zangu kapatia wapi alikata simu. Cha ajabu zaidi leo asubuhi nimekuta email yao kwenye simu yangu ikisisitiza nilicho ambiwa jana na mwanamke aliejitambulisha kuwa ni mkurugenzi.

Kwa kweli baada ya simu hiyo nimekuwa na wasiwasi sana kwani nahofuia usalama wangu, mana nimejiuliza Mimi ni nani hadi wanipigie simu.
 
Saa tatu usiku kwa ishu za kazi ni ishu kidogo

Ila

Angalia domain ya email yao.

Mfano

castr@gmail.com

Hapa domain ni gmail.com

Kwao domain ni ipi?
Wahuni wanaweza kutengeneza domain ambayo itakuwa inafanana kabisa na jina la shule husika.

Fact check afanye yafuatayo;
1. Google search shule husika na mahali ilipo.
2. Tafuta mawasiliano ya wahusika.
3. Asubiri amalize chuo
4. Asitoe ushirikiano wowote kwa sasa
 
😁nimecheka kidogo nife.Mi ni kadhani wewe ni CEo flani wa kampuni kubwa Africa,au ni gavana wa benki kuu Africa kumbe ni mwanachuo ambaye hujahitimu na unayesomea Ualimu.
Mkuu Kuna konection ambazo ww mwenyewe huzijui ila wanaokufahamu wanakutengenezea,so uliza nenda nae taratibu maana unaweza ukapoteza au ukapigwa
 
Wahuni wanaweza kutengeneza domain ambayo itakuwa inafanana kabisa na jina la shule husika.

Fact check afanye yafuatayo;
1. Google search shule husika na mahali ilipo.
2. Tafuta mawasiliano ya wahusika.
3. Asubiri amalize chuo
4. Asitoe ushirikiano wowoye kwa sasa
Even a domain ili kumtapeli third year is a big step tho
 
Wakuu mdogo wenu nipo njia panda, Jana usiku sasa tatu kamili nime pigiwa simu na mwanamke aliejitambulisha kuwa ni mkurugenzi wa shule moja binafsi hapo jijini Arusha (jina nimelitunza O level hadi A level), lengo la simu yake amenambia kuwa wananihitaji katika shule yao mara baada ya kumaliza masomo mwaka huu (nipo mwaka wa tatu hapa DUCe, nachukua Bachelor of Science with Education, Biology na Chemistry).

Baada ya kumuuliza namba zangu kapatia wapi alikata simu. Cha ajabu zaidi leo asubuhi nimekuta email yao kwenye simu yangu ikisisitiza nilicho ambiwa jana na mwanamke aliejitambulisha kuwa ni mkurugenzi.

Kwa kweli baada ya simu hiyo nimekuwa na wasiwasi sana kwani nahofuia usalama wangu, mana nimejiuliza Mimi ni nani hadi wanipigie simu.
Kwani mkuu ww una issue gani mpaka uwe na wasi wasi au unatembea na mke wa mtu? Huwezi kuwa na wasi wasi kwa kitu kama hicho unless labda uwe most wanted
 
Graduates wa siku hizi ni bure kabisa. Sisi enzi zetu tulikua tunaenda hadi maporini na vibahasha vyetu kisa kuna kibao kinaonesha uhai huko wa kupeleka CV na hatukuogopia kitu, afu we unakuja kuogopa email na call? Hopeless kabisa
 
Nipe jina la shule nifanye cross check.
Ikiwa matapeli utakuja kuwatambua wakiwa uchi..
Sina utani na matapeli mm.
Karibu kijana nipe details zao.
 
Saa tatu usiku kwa ishu za kazi ni ishu kidogo

Ila

Angalia domain ya email yao.

Mfano

castr@gmail.com

Hapa domain ni gmail.com

Kwao domain ni ipi?
Mnabagua sana na hii itawacost ipo siku nilipotoa kuwa nimetumiwa email ya ajabu kama hizo ya mtu kuniinclude kuwa wanataka kutuua hamkutoa ushirikiano kwa maana mie ni malaya sindio nyie sio miungu Mungu ndio ananilinda. Kabisa mkae mkijua . Najingine maisha mungu anapanga ipo siku hata nyie mtakuwa na shida tu na mtakutana na watu wa liokama niliokutana nao.
 
Back
Top Bottom