Tafadhali naomba tafsiri ya sentenzi hii katika lugha ya kiingereza!

Hapa panakaribia na ukweli... nafikiri karika utamaduni wao hakuna maneno yanayofanania na haya. anyway huwa tunapenda kutumia ''hope u had a nice journey'' kuwaambia wazungu wakitutembelea... sasa hapa kwetu tutatumia kiswahili gani???
 
kwa kawaida ukitaka kutafsiri lugha ni vizuri kujua utamadui wa lugha ya kutafsiria. waingereza hawana utamaduni wa kusema pole kwa namana ileile ya waswahili mfano pole kwa kazi pole kwa kuumwa n.k. wao wanaashiria kwa ku simpathise hivyo kama una maumivu watasema sorry kuonyesha wanasikitika kwa hivo kama umetoka safari watakusifia tu yaani watasema congratulation ... ikiwa utasimulia matatizo katika safari yako watasema sorry. kwa hivo kusema kweli mtu akikuambia pole kwa safari hana maana hasa kusikitika bali anakupongeza basi tafsiri hasa ya pole kwa safari ni congratulation for arriving safely (now you can have a rest) au kwa kifupi hongera congratulation. usiangalie hasa maneno angalia kusudio la msemaji
 
sina hakika kama wazungu wana utamaduni wa kupeana pole kwa safari kwa maana kwa wao safari ni ku-enjoy, kuburudika, kustarehe na kujifunza sio kama sisi wabantu unampa mtu pole ya safari bila kujali kuwa alifurahia safari au la! kama nimesafiri kuzuru mbuga za wanyama sasa pole ya nini wakati nilienda kuburudika!?

Kweli kabisa, wazungu hawana sababu ya kupeana pole kwa safari kwani barabara zao ni nzuri. Hazina mashimo kwa hiyo hawatingishwi na kuchoka. Pia magari hayakwami ovyo wakati wa mvua na kusukumwa kwa hiyo hawachoki kwa safari. Vilevile hawana traffic jam kama Dsm kwa hiyo gari linakwenda kasi hawasimami saana njiani na kuchoka. isitoshe wanasafiri kwa ndege umbali ulio mrefu kwa hiyo hawachoki kwa safari. Sio akina sisi tunasafiri kwa siku mbili toka Dsm kupitia Kenya kwenda Mwanza utaacha kuchoka upewe pole? Kwa hiyo kwa kiingereza neno hilo halipo bali liko Tz katika lugha zote.
Poleni kwa safari jamani.
Napita tu.
 
Yap hapo nimekusomeni... kuna wakati nataka kumwambia bosi wangu pole na safari... kwa lugha ya ki-english.... nakosa msamiati... najikuta nabadili lugha ili kufikisha ujumbe.
 
mmejaribu ila tuwe tunamaanisha nini hasa tunataka kujua na kwa manufaa (joke sana) itatupoteza
 
''pole na safari'' tunasemaje hapo kwa ki-english?

Hapa naona shida ni neno 'pole' kama linavyotumika kiswahili halipo katika kiingereza. nafikiri pia kuana mahusiano na tamaduni, mfano ukiwa unatembea na mtu akijikwaa kwa kiswahili unamwambia 'Pole' kwa kidhungu unajua wanakuambiaje 'be careful' ambayo kikwetu ingetafisiriwa kuwa umekuwa katili sana kwake.
Inabidi tukubali lugha zina mapungufu pia mfano mwingine ni maneno maarufu ya kifaransa wakati wa kula mnatakiana hamu ya kula 'Bon appetit' hakuana msemo wa kizungu wa moja kwa moja ila kutokana na umaarufu wa kutakiana hamu ya kula unaweza kulazimisha ukasema 'have a good appetite' wengine wansema énjoy your food'ambayo naikubali zaidi
 
mi kama ndo katoka safari namwambiai hope you enjoyed your journey well. welcome back, whats up? naye anasema thank you very much we enjoyed much.
 
kwa kawaida ukitaka kutafsiri lugha ni vizuri kujua utamadui wa lugha ya kutafsiria. waingereza hawana utamaduni wa kusema pole kwa namana ileile ya waswahili mfano pole kwa kazi pole kwa kuumwa n.k. wao wanaashiria kwa ku simpathise hivyo kama una maumivu watasema sorry kuonyesha wanasikitika kwa hivo kama umetoka safari watakusifia tu yaani watasema congratulation ... ikiwa utasimulia matatizo katika safari yako watasema sorry. kwa hivo kusema kweli mtu akikuambia pole kwa safari hana maana hasa kusikitika bali anakupongeza basi tafsiri hasa ya pole kwa safari ni congratulation for arriving safely (now you can have a rest) au kwa kifupi hongera congratulation. usiangalie hasa maneno angalia kusudio la msemaji

Muuliza swali azingatie sana uzi wa chumachakavu na mzamifu. Hawa waliweka kando mzaha wa kivulana na kudadavua suala lililosailiwa. Unapotafuta tafsiri ya neno au tungo yoyote kutoka lugha yoyote ni lazima kwanza utangulie kufikiria utamaduni wa lugha lengwa ikiwa unawiana na utamaduni wa lugha chanzi juu ya suala mnalolijadili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom