Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
Nape unadai Kikwete na familia yake wanachafuliwa kwa kuhusishwa na hao watu kwani nyoka anajivua magamba. Kijana hizi picha zinadanganya ? Kumbuka Wapemba hutambuana kwa vilemba na ndege wa rangi moja huruka pamoja.
Hapa anaonekana Kikwete akimnadi Rostamu Igunga kwa kudai ni mtu safi ila anasingiziwa!
Hapa Kikwete anaonekana akimnadi Lowasaa huko Monduli na kudai hana doa na ni mchapakazi ila anasingiziwa tu !
Hayo yakiendelea Salma Kikwete naye akajitosa uwanjani kumnadi Chenge huko Bariadi kwa kudai ni mtu safi ila anaonewa wivu !
Na katika hali ya kuongezea chumvi kwenye kidonda cha Watanzania, Kikwete akamnadi hadi Mramba Rombo akisema, "Huyu kwa maneno ya mjini, ni Mzee Kijana, kwani ni mwenye mawazo mapya yenye manufaa wakati wote…siyo wale wazee ambao wakichoka la mbele linawekwa nyuma, la nyuma linawekwa mbele. Huyu ubongo wake unajadidika (renewal), ni chimbuko la maarifa mapya".
Wakati JK anamnadi, Mramba alikuwa akikabiliwa na kesi ya ufisadi mahakamani iliyofunguliwa na serikali.
Huo msitari unaowatenganisha Kikwete na hao washikaji wake umechorwa lini na nani na kwa misingi ipi ? Hapana, labda mtafanikiwa kuwazuga hao hao mliozoea kuwazuga, lakini mjue wengi wanaanza kuzinduka.