Tadea yaridhishwa na Utawala Bora Tanzania

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Mwenyekiti wa Chama cha Ada Tadea ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania Mhe. Juma Ali Khatib amesema kuwa Tanzania imefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika kuimarisha suala la demokrasia na siasa hali ambayo imepelekea Tanzania kuwa katika hali nzuri ya Utawala Bora ukilinganisha na nchi nyengine za Afrika.

Hayo ameyasema mapema leo hii wakati alipokutana na uongozi wa Taasisi ya Mpango wa hiyari wa nchi za umoja wa Afrika kujipima katika vigezo vya utawala Bora (APRM Tanzania) katika Ofisi za Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.

Mhe Juma amesema kuwa katika uso wa dunia Tanzania ina taswira nzuri na kubwa kuhusu masuala ya Utawala Bora na hilo linatokana usimamizi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuonesha ukomavu wa hali ya juu katika suala la siasa kwa kufungua milango ya demokrasia na kuruhusu mikutano ya hadhara na kutoa mwanya mkubwa katika suala la ushirikishwaji wa wananchi.

Aidha ameahidi uongozi wa APRM Tanzania kuwa yeye binafsi pamoja na wafuasi wake wa Chama cha Ada Tadea wapo tayari kutoa ushirikiano mkubwa kwa APRM wakati ambapo wataalamu wa kukusanya maoni wakifika katika maeneo yao.

Kwa upande wake Katibu mtendaji wa APRM Tanzania Lamau Mpolo amesema kuwa vyama vya Siasa ni wadau muhimu sana kwa APRM na watahakikisha kuwa maoni na michango yao inachukuliwa kwa uzito mkubwa katika uandishi wa Ripoti ya Pili ya Tathmini ya masuala ya Utawala Bora Tanzania.

Lamau ameongeza kuwa kwa vile dhumuni la APRM Tanzania ni kukuza dhana ya Utawala Bora kwa kuzingatia vigezo vinavyokubalika kimataifa hivyo itahakikisha inafuata msingi wa kuwashirikisha wananchi bila kutumika kisiasa ili iweze kuandaa Ripoti ambayo itakubalika Kimataifa na kuweza kuharakisha shughuli za kimaendeleo pamoja na kuimarisha muungano wa kikanda na Bara zima la Afrika.

Katika ziara hiyo, uongozi wa APRM Tanzania umeambatana na Katibu Mtendaji Lamau Mpolo, Mratibu wa eneo la Uchumi Jamii Balozi Hemedi Mgaza na Meneja wa Habari na Mawasiliano Badria Masoud.
_A017544.jpg
_A017607.jpg
_A017605.jpg
_A017562.jpg
_A017602.jpg
_A017557.jpg
_A017586.jpg
_A017617.jpg
 
Back
Top Bottom