Tabora yangu Tabora

Mji wangu mkongwe wa Tabora,
Wewe ndio chimbuko la vuguvugu la uhuru wa Tanganyika,
Ndio mji mkubwa wa kwanza hapa Tanganyika enzi za ukoloni,
Leo umesahaulika mkoa wangu Tabora,
Sijui ni nani amekupoteza Tabora yangu,
Umezalisha wasomi na wazalendo wengi Tabora yangu,
Hukujipendelea kwa kujipendelea mkoa wangu Tabora,
Leo unaonekana ni mkoa ulio mwishoni kabisa,
Hata sherehe za miaka 50 hujakumbukwa na kupewa nishani kwa harakati zako Tabora,
Akina Fundikira na Kasangatumbo walikiona cha moto japo walipigania uhuru,
Tabora mji wangu wee...leo umebakiwa ni magofu,
Utalii haushamiri, japo fursa za historia zipo,
NANI KAKUPOTEZA TABORA WANGU,
Umezalisha viongozi lukuki, lakini wamekusahau Tabora,
Leo miundombinu hafifu, shauri ya kukuikomboa Tanganyika,
Nani atakukumbuka Tabora, iwapo hata nishani za uhuru hukupata,
Umejaaliwa ardhi rutuba, misitu na wanyama pori,
Wajanja wanakutafuna Tabora, na kukuachia jangwa bila maendeleo
AMKA TABORA AMKA, NAWE UONJE KEKI YA TAIFA.
Umeibeba historia ya nchi, lakini miaka 50 huthaminiwi.
Umeletewa Sanamu, na uwanja wa mpira usiokamilika,
Barabara hazipitiki, ndio leo wanaamka kukutengenezea barabara baada ya miaka 50,
Si reli wala ndege, barabara ndio tegemeo,

Maendeleo ya sehemu huchangiwa na wenyeji sasa ndugu zangu Wanyamwezi mmekalia umbea na starehe kazi hamtaki kufanya mtapataje maendeleo?
 
tabora haiwezi endelea kama wanatabora wenyewe hawtabasdili utamaduni wao, ni bahati mbaya sana kwamba wanatabora wenyewe hawatambui kama wako nyuma kumaendeleo; nimeishi tabora kwa mda mrefu sana, pamoja na ukarimu wa wenyeji lakini its not a place to stay
 
Back
Top Bottom