Tabora: Yaliyojiri kutoka viwanja vya Ali Hassan Mwinyi, Rais Magufuli ahutubia Wananchi

''Na kwa ombi la viwanda, niwaombe wabunge walete wawekezaji waje wajenge viwanda na serikali itawapa support. Na tutampunguzia hata ushuru, tutampa hata eneo."

Alituahidi viwanda, sasa hivi anawaomba wabunge walete wawekezaji waje wajenge viwanda!

Hapa Malaika kaniacha mbali, nisaidieni kufafanua hiyo kauli.
 
hakuna tatizo kutokana na kauli ya Rais na wala hakuna tatizo kwa mtu wa kawaida kutamka kwamba kuna vilaza au mtu fulani ni kilaza hayo ni maoni binafsi hasa ukizingatia kwamba,anaemsema sio wa chama chako maana ni tofauti na sera zako hivyo una haki ya kumuita kilaza au mjinga ili mradi usimpige kibao kwa ujinga wake
 
Yeye dikteta uchwara ndiye mwenye RUKHSA ya kutumia maneno ya kuudhi lakini wakitumia wengine ni UCHOCHEZI!

Watanzania wenzangu. Kuna mambo ambayo yanashangaza sana nchini mwetu, vituko haviishi!

Naangalia taarifa ya habari Azam Tv. Wame-cover ziara ya Rais Kigoma/Tabora. Akihutubia umati wa watu, rais amempongeza Prof. Kitila Mkumbo kuwa ni mwerevu na mwenye akili kutoka chama cha upinzani tofauti na wale vilaza wa vyama vingine vya upinzani na ndio maana amemteua.

Sioni tatizo hapa kwa rais kuwata wapinzani vilaza, hayo ni maoni yake na kwa ufahamu wake ni sawa.

Tatizo langu ni taabu na polisi kuwakamata wapinzani wanapodai kuwa rais ni dikteta uchwara! Nikilichunguza neno uchwara maana yake ni kitu kisicho halisi na sioni tatizo kwa wapinzani kumwita hivyo.

Tatizo naloona hapa ni jinsi watawala na vyombo vya dola na hata wanaharakati watakaa kimya.

Kama Tume ya Utawala bora na haki za binadamu walimkemea Mkapa kwa kuwaita wapinzani wake wapumbavu, je wataweza kufanya hivyo kwa rais?

Vv
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli amefunguka na kuahidi kuwa bado ataendelea kuchomoa baadhi ya watu katika vyama vya siasa nchini huku akisema ataacha vilaza tu kwenye vyama hivyo Ameyasema hayo mapema hii leo alipokuwa kwenye ziara mkoani Tabora katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi, ambapo amesema kuwa maendeleo ya nchi hayana vyama ndiyo maana ameweza kuchangua baadhi ya viongozi kutokea upinzani na kudai kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu. [ 142 more words ]

JPM: Nitachomoa mwingine mwenye akili kutoka upinzani
 
Watanzania wenzangu. Kuna mambo ambayo yanashangaza sana nchini mwetu, vituko haviishi!

Naangalia taarifa ya habari Azam Tv. Wame-cover ziara ya Rais Kigoma/Tabora. Akihutubia umati wa watu, rais amempongeza Prof. Kitila Mkumbo kuwa ni mwerevu na mwenye akili kutoka chama cha upinzani tofauti na wale vilaza wa vyama vingine vya upinzani na ndio maana amemteua.

Sioni tatizo hapa kwa rais kuwata wapinzani vilaza, hayo ni maoni yake na kwa ufahamu wake ni sawa.

Tatizo langu ni taabu na polisi kuwakamata wapinzani wanapodai kuwa rais ni dikteta uchwara! Nikilichunguza neno uchwara maana yake ni kitu kisicho halisi na sioni tatizo kwa wapinzani kumwita hivyo.

Tatizo naloona hapa ni jinsi watawala na vyombo vya dola na hata wanaharakati watakaa kimya.

Kama Tume ya Utawala bora na haki za binadamu walimkemea Mkapa kwa kuwaita wapinzani wake wapumbavu, je wataweza kufanya hivyo kwa rais?

Vv
Wapinzani wengi ni punguani wa akili. Yaani wana mtindio wa ubongo. Yaani siyo binaadamu ni nusu binaadamu
 
Mikutano mingi ya raisi magufuli ni viwanja vikubwa vya michezo
Sasa huwa najiuliza anaenda kuzindua miradi huko viwanjani au au ni mikutano ya ccm

Na huu utakuwa ni upumbavu kama rais anafanya kazi ya kuzindua mikutano ya ccm
Mwenzio yupo kwenye kampeni hana uhakika Kitengo kitamuweke tena ajabu a nakumbuka na mabango wanamwambia haja fanya kitu a naanza kutukana wananchi jamaa kaloa hajui hata aseme nini anajiapiza hadi u namuona huruma
 
''Na kwa ombi la viwanda, niwaombe wabunge walete wawekezaji waje wajenge viwanda na serikali itawapa support. Na tutampunguzia hata ushuru, tutampa hata eneo."

Alituahidi viwanda, sasa hivi anawaomba wabunge walete wawekezaji waje wajenge viwanda!

Hapa Malaika kaniacha mbali, nisaidieni kufafanua hiyo kauli.
Kwa lugha chafu na anavyokandamiza demokrasia hakika atabaki na cherehani nne kama viwanda
 
Msikilize huyo kisebengo wako hapa:

Maskini vyeti hamna mumepewa madaraka muna hofu kuu vichwa vya panzi shule ziliwashinda muna nene pa makalio kwa kodi za wananchi mumeshupaaza shingo hamtaki muambiwe ukweli madictator wakifa wamekuwa wakashindwa kuzikwa wengi mizigo yao I kali wa na fisi sasa kwa taarifa yako hii ni nchi ya wote
 
Mh Hussein Bashe (Mbunge wa Nzega Mjini)

=>Hawa watu wanatakiwa kufungiwa leo hakuna
Nakuomba mh raisi utakapomteua mtendaji mkuu wa kamisheni ya madini, waanzishe masoko kwenye sehemu yenye wachimbaji wadogo.

=>Naona mtendaji mkuu wa ACACIA amesema wanahisa hawatapata divident kwasababu ya mchanga uliozuiwa, wao walikuwa wanasema ni makapi na sasa hawatoi divident, tuendelee kuchukua hatua kulinda rasilimali zetu.

=>Tunakushukuru mh rais kwa kutuletea maji Tabora

======

Sasa Rais Magufuli anaanza kuhutubia;

Rais Magufuli: Tabora Hoyee....

=>Mh mkuu wa mkoa wa Tabora, waziri wa ujenzi, waziri wa maji, naibu waziri wa afya Dr Kigwangala, wabunge wa Tabora, MaDC, viongozi wa dini, waheshimiwa madiwani, wakurugenzi, waandishi wa habari, wanachuo, viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

=>Kwanza ninawashukuru sana kwa heshima kubwa mliyonipa na kwa kumtanguliza Mungu na kwa kunichagua. Asanteni sana kwa kura nyingi mlizonipa. Mungu awabariki sana.

=> Niseme kwa dhati kwa jinsi mlivyonipa kura nyingi na wabunge na madiwani, napenda niseme nina deni kubwa.

=>Tabora ina heshima kubwa katika kutetea ukombozi wa taifa letu.

=>Ndugu zangu wa Tabora, nimesema mkoa wa Tabora una heshima ya pekee. na ndiyo maana wananchi wa Tabora niliwaomba kwa heshima kubwa.

=>Nilipochaguliwa na ndiyo maana nimekuja hapa kuwashukuru na kuzindua miradi ya maedeleo.

=>Namshukuru sana rais wa awamu ya nne. Miradi ninayowezindua leo ilianza awamu ya nne. Mimi nilikuwa waziri wake. Tutakuwa tumekosa shukrani bila kushukuru Kikwete.

=>Ninafahamu, miradi ya ujenzi iliyopo katika manispaa ya Tabora. Ukiangalia fedha zilizotumika pale fedha zote zilitolewa na serikali.

=>Kwa juhudi hizi kubwa zinazofanywa na serikali, Kuna fedha zilizotolewa na benki ya dunia kwa ajili ya kujenga barabara. Na leo nimetoa maagizo, uwanja wa ndege upanuliwe.

=>Tunafanya yote haya ili wananchi wachague wenyewe, watatumia usafiri gani wanapotaka kusafiri.

=>Ndugu zangu wanatabora tutembee kifua mbele. Na leo mmeshuhudia Prof Mkumbo

=>Na mimi nitaendelea kuchomoa wale wenye akili waliopo kwenye vyama vingine, wale vilaza wataendelea kubakia kwenye vyama vingine.

=>Maana mimi ni rais wa wote, hata ukiwa chadema mimi kwangu sawa tuu, ukitaka ninyooshe vidole; si vidole tuu..

=>Reli tuliyonayo ilijengwa mwaka wa 1905 na kuja kumaliziwa na wajerumani.

=>Kwahiyo tunajenga reli ya umeme, na itakuwa inachukua muda mchache tuu.

=>Niwaombe wana Tabora.

=> Sisi wanasiasa tuache siasa katika maendeleo.
=>Nimekuwa nabomoa nyumba ili zipite barabara wakati nikiwa waziri lakini bado mlinichagua.

=>Watu walio katika hifadhi ya reli tutabomoa ili wasitucheleweshe, na waanze kujiandaa kutafuta maeneo.

=>Kwa mujibu wa sheria namba ya 4 na 5 kifungu cha tatu, watu watakaobomolewa watalipwa.

=>Tunataka hiyo njia ya reli iwe nyeupe, haya ndiyo maendeleo tunayotaka.

=>Nimesikia kilio cha mbunge wa hapa, najua lazima aseme hivyo maana mmemtuma awasemee.

=>Tabora ni miongoni mwa mikoa yenye matatizo ya maji.

=>Tuliahidi kwenye ilani ya uchaguzi kwamba maji vijijini 85% na mijini 95%

=>Waziri mkuu wa India alipokuja kututembelea, nilimuonyesha Tabora kuwa ndiyo kipaumbele katika mradi wa maji ambao utauhusisha vijiji 89.

=>Leo nimeweka jiwe la msingi na ndani ya miaka 2, mradi ule utakuwa umekamilika.

=>Wananchi wa Tabora mmependelewa, ninawaomba sana tushirikiane na tuvumiliane. Mambo yote hayawezi kufanyika siku moja.

=>Tumemaliza barabara zote. Na huo ndio utanzania. Ipo mikoa ambayo haijapata barabara. Umeme nao utaletwa, mtuvumilie.

=>Wananchi tulipe kodi, kwa wananchi wa kawaida mnalipa kodi. Watu wanaokwepa kodi ni wale matajiri wakubwa.

=>Na ninyi wananchi wa Tabora muendelee kuwaelimisha wananchi wengine umuhimu wa kulipa kodi.

=>Tumechukua hatua ya kukusanya mapato kutoka bilion 800 hadi trilioni 1.3.

=>Mwaka jana tuliongeza wanafunzi waliopata mikopo kutoka 98,000 hadi 125,000

=>Tumetangaza ajira kwa madaktari na manesi.

=>Tulikuwa tumejaza wafanyakazi hewa kila sehemu.

=>Ni Tanzania tuu kila sehemu unakuta kila kitu hewa, kuna mpaka wakimbizi hewa.

=>Kumekuwa na wanafunzi hewa 65,000. Kumekuwa na mikopo hewa ya zaidi ya bilioni 3. mikopo hewa ya zaidi bilioni 38. Kulikuwa na kaya hewa.

=>Hizi fedha zilitakiwa ziende kwenye hospitali, zinunue ndege na kwa wafanyakzi tutaanza kutoa promotion.

=>Kwa Tumbaku, tutaanza kuchukua hatua.

=>Na kwa ombi la viwanda niwaombe wabunge walete wawekezaji waje wajenge viwanda na serikali itawapa support. Na tutampunguzia hata ushuru, tutampa hata eneo.

=>Tushikamane wote wabunge wa Tabora, na kukiwa na kiwanda Tabora hata hili tatizo la Tumbaku tutalimaliza.

=>Nimekuja hapa kuwashukuru, nawashukuru sana wabunge wa Tabora, wana ushirikiano sana.

=>Tumepunguza tozo za mazao kwa mzigo usiozidi tani moja.

=>Kwenye mifugo tumefuta tozo saba na uvuvi tozo 5.

=>Kwa wafanyabiashara wadogo, watapata utambulisho maalumu na wapewe maeneo.

=>Mh Bashe amezungumza kuhusu wizi uliokuwa unafanywa katika dhahabu.

=>Na kutumbua nitaendele kutumbua na wala siogopi.

=>Na ndiyo maana nilipoingia nilifuta safari zote, semina semina zote nilifuta. kama unataka kufanya semina, fanya hata chini ya mwembe.

=>Kwa hiyo nimebinya hiyo mianya ya wakubwa, nikawapa wananchi.

=>Wafanyakazi wamekuwa hawalipwi, wamekuwa wanacheleweshewa na tumeamua madai ya watumishi lazima yalipwe mara moja.

=>Tunafanya hivi kwa maslahi ya wananchi hasa wananyonge, hii ndiyo Tanzania ninayoitaka.

=>Maendeleo hayawezi kupatikana bila ya kuwepo amani.

=>Katika mikoa hii ya Tanzania, nimeteua viongozi wengi, hawa wote wapo kwa ajili ya kutatua matatizo ya wananchi.

=>Niwaombe viongozi wa mkoa wa Tabora mshughulikie kero za wananchi.

=>Inawezekana viongozi mnakaa sana ofisini bila kutatua kero za wananchi.

=>Niwaombe viongozi wakuu wa mkoa, wakuu wa wilaya msikilize kero za wananchi na kuyatatua.

=>Sasa nitakuwa natembea mikoani, nikiona kero ambazo wakuu wa mikoa na wilaya wangeweza kutatua, nitalala nao mbele.

=>Najua hapa mkoa wa Tabora, kuna tatizo kubwa la ardhi. Ninaomba mkuu wa mkoa kila mwenye tatizo, uelekeze litatuliwe na nani. Yale ambayo yamekushinda ukiona kwangu ni mbali sana mpelee waziri mkuu wangu.

=>Nipende kuwaomba mshirikiane na wabunge wenu na madiwani.

=>Mimi nipo pamoja na ninyi na mapokezi niliyoyapa hapa Tabora yananifanya niwe na deni kubwa.

=>Ninawashukuru sana walioniombea hapa, niwashukuru sana wana Tabora.

Niwashukuru sana na Mungu awabariki

Close linkage with other dictatorships will increase possibilities for survival of a dictatorship.
 
Maskini vyeti hamna mumepewa madaraka muna hofu kuu vichwa vya panzi shule ziliwashinda muna nene pa makalio kwa kodi za wananchi mumeshupaaza shingo hamtaki muambiwe ukweli madictator wamekuwa wakashindwa kuzibwa wengi mizigo yao I kali wa na fisi sasa kwa taarifa yako hii ni nchi ya wote
Umemsikiliza huyo kibwengo akisema "takataka" lakini?
 
Aruhusu na wapinzani wake wafanye kama yeye anavyofanya basi! Yote anaongea peke yake, huku akizuia wenzake kufanya mikutano! Majimbo yenye wapinzani na ambako wabunge wake wanafanya vizuri haendi maana hawezi kuwasifia wapinzani maana kwake ni dhambi. Ila kule walipo CCM na ambapo umaskin umepiga kambi ndo mremko na tambo za kufa mtu.
 
bandiko la hotuba ya rais lina saa zaidi ya 7 lakini comments zinalingana comments za bandiko la kuhusu lipumba

huyo mzee apelekwe kwa mkemia mkuu akapimwe kiwango cha umaarufu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom