TAAZIA: Sheikh Ahmed Zubeir Mwalimu na mlezi wa vijana

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,924
30,272
SHEIKH AHMED ZUBEIR MWANAFUNZI WA SHEIKH ABDALLAH FARSY NA MWALIMU NA MLEZI WA VIJANA WENGI DODOMA
Namkumbuka Sheikh Ahmed Zubeir katika miaka ya mwanzoni 1980s ndiyo karejea Tanzania akitokea Mombasa Kenya alipokuwa akisoma kwa Al Marhum Sheikh Abdallah Saleh Farsy.na pia Sheikh Ally Seneda Gunda (Baba yake Dr. Janja Gunda wa UDOM).

Sheikh Ahmed Zubeir alikuwa amerudi Tanzania katika wakati ndiwo khasa.

Waislam wa Tanganyika walikuwa wanafungua ukurasa mpya wa kutaka kubadili mengi yaliyokuwa yanawaelemea kwa miaka mingi.

Sheikh Ahmed Zubeir alichagua kwenda Dodoma kusomesha.

Kwa hakika alipokelewa vyema na vijana wa Kiislam wa Dodoma kama Faiz Mafungo, Abdulkadir Faya maarufu kwa jina la Moto, Ahmed Mnyanga, Jaffar Mjasir, Colonel Mohamed (Wambung’o) Hamisi Ambari, Mahmud Abdurahmani Dachi kwa kuwataja wachache.

Sheikh Ahmed Zubeir alikuwa kijana umri sawa na vijana aliowakuta Dodoma waliompokea kwa mikono miwili.

Haukupita muda Sheikh Zubeir akishirikiana na vijana wenzake wakaweka darsa Msikiti Nunge ambako ndiko alipowakuta vijana wenzake.

Darsa likashamiri kupita kiasi pamoja na darsa la Tafsir ya Qur’an Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na tarweh yake na baada ya Ramadhani.

Mwaka 2002/2003 Sheikh alikwenda Makkah – Chuo Kikuu cha Ummu al Qura - kuhudhuria Mafunzo ya Maimamu na Wahubiri inayokuwa chini ya Muslim World League (MWL) na ambayo huchukuwa kiasi cha mwaka mmoja.

Sifa za kujiunga na mafunzo haya ilikuwa mtu kwa kiwango cha chini awe na shahada ya kwanza ya Chuo Kikuu, lakini yeye alikuwa kasoma majamvini.
Vipi kuwaje kupata fursa hii?

Ni hivi.

Uongozi wa WML (akiwemo Katibu Mkuu) mnamo mwishoni mwa miaka ya 1990, ulipata kuzuru Tanzania, walipofika Dodoma, walikutana na Sheikh Ahmad na wakazunguka naye katika miradi na taasisi mbalimbali.

WML walivutika sana na kushangazwa na maalumati yake na umahiri wake wa lugha ya Kiarabu na hawakuamini kwamba yote haya ameyapata majamvini tu.

Basi aliahidiwa fursa ya masomo ya ziada.

Sasa walipokuja watendaji kuwasaili walioomba nafasi hizo, walipofika kwa Sheikh wakamshangaa, ni vipi kaomba na kupendekezwa kwa usaili naye cheti hana?

Akawaomba hivyo hivyo wamfanyie usaili.
Allahu Akbar!

Aling’ara hata zaidi ya wengi wenye vyeti vyao, wakawa hawana budi kumchukua.

Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya Sheikh Shaaban Musa ambaye alikuwa masomoni Saudia katika kipindi hicho akisomea shahada yake ya kwanza, anasema hivi:

“Wakati wa Msimu wa Hijja, tukiwa Minna, alikuja kwenye hema letu la Haji Trust na akakutana na Sharifu Mwenyebaba wa Mambrui, Kenya, na nilichokiona baina yao ni kwamba Sheikh Ahmad alikuwa akimhariria makala yake (Sharifu) ambayo ilikuja kutoka kwenye gazeti la Rabita (MWL) akizungumzia hali ya Da'wah na Maduat wa Afrika.”

Sasa turejee Dodoma.

Dodoma ni Mji Mkuu wa Tanzania na Bunge lilipohamia Dodoma na Msikiti Nunge kuwa msikiti ulioko katikati ya mji na Waislam wengi waliokuwa serikalini pamoja na wabunge Waislam na wapita njia wakauchukua Msikiti Nunge kuwa msikiti wao, akiwemo swahibu yake mkubwa Al Marhum Meja Jenerali Mstaafu) Muhiyidin Kimario, aliyewahi kuwa Murugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Makao Makuu Dodoma (CDA).

Nunge ukawa msikiti ambao wakubwa wote wakiwa Dodoma watasali hapo na vilevile kuhudhuria darsa za Sheikh Ahmed Zubeir.

Ikawa hata kama una lako unamtafuta muheshimiwa ambae huwezi kumfikia ofisini kwake kwa vizingiti vya urasimu wa maofisa wa serikali ukimvizia Msikiti Nunge utamtia mkononi.

Shida zako zitakuwa zimemalizika.

Kama ilivyo kawaida ya neema yeyote haikosi kuhusudika.
Ghafla ikatokea fitna kuwa wenye msikiti wao wanaudai.

Hiki kikawa kipindi kigumu kwa Sheikh Ahmed Zubeir kwa kiasi polisi walihusishwa katika mgogoro ule na baadhi ya Waislam kukamatwa na kuwekwa korokoroni.

Lakini hili likapita na Waislam wakaibuka na nguvu kubwa haba jana.
Kipindi hiki baada ya kupita ndipo mimi nikajuana na Sheikh Ahmed Zubeir na vijana wa Kiislam waliokuwa Dodoma.

Vijana wa Msikiti Nunge kwa ushirikiano na Muslim Students Association of the University of Dar es Salaam (MSAUD) walikuwa wakiendesha programu kadhaa pamoja.

Katika programu hizi moja ilikuwa kuwatafuta na kuwasomesha watoto hodari katika masomo ambao hali zao ni za dhiki.

Sheikh Ahmed Zubeir kwa ajili ya programu hii alikuwa mara kwa mara akija MSAUD na hivi ndivyo tukaja kufahamiana.

Wakati ule nilikuwa katibu MSAUD.

Hawa wanafunzi walikuwa chini yake na wengi wao walikuwa sekondari na yeye ndiye aliyekuwa mlezi na mwalimu wao wa Qur'an.

Iko siku mwaka jana nikiwa na mgeni wangu katika moja ya migahawa maarufu tunakula chakula cha usiku mbele ya meza yetu alikuwa amekaa kijana na binti amejitanda vizuri na watoto wadogo wawili.

Picha niliyopata ni kuwa wale ni mtu na mkewe na hao ni watoto wao.
Lakini kilichonivutia ni ule mwonekano wao kijana kavaa kanzu na kofia kapendeza na mkewe yuko kwenye hijab.

Hakika walikuwa wamependeza kuwatazama.

Si siku zote mtu unakutana na vijana kama hawa mtu na mkewe na watoto katika migahawa kama hii.

Kila nikigeuza shingo naona yule kijana jicho lake halibanduki kwangu.
Ukapita muda tunaibiana kushangaana.

Mara yule kijana akanyanyuka ghafla akaja kwenye meza yetu akatutolea salamu.

"Sheikh Mohamed Said," kijana kaushika mkono wangu tabasamu kubwa usoni mwake.

"Naona umenisahau."
Sikuweza kumkumbuka.

Mimi fulani.
Subhanallah!

Lile jina lilikuwa maarufu ofisini kwetu MSAUD.

Mwanafunzi hodari mtoto mwema katika orodha ya wanafunzi wa Sheikh Ahmed Zubeir.

Mwanafunzi akiongoza shuleni kwake katika masomo na tabia.
Imepita miaka yapata 30 tumepotezana.

Sikuyaamini macho yangu.

Nimemwacha mtoto mdogo leo tunakutana mtu mzima ana mke na watoto.

"Alhamdulilah."
Nilishukuru.

"Haya bwana sasa unafanya nini?"
Aliponitajia kazi anayofanya serkalini sote tulicheka.

Mwanafunzi wa Sheikh Ahmef Zubeir leo kawa kijana wa kutegemewa na taifa lake.

Kubwa ni kuwa hakubadilika kwa mafanikio yake.
Ni mtoto yule yule niliyekuwa nikimjua miaka 30 iliyopita akiwa sekondari.

Naamini kifo hiki cha mwalimu na mlezi wake kimempiga sana.

Naamini Sheikh Ahmed Zubeir kawaacha vijana wengi kama huyu.

Kwa mfano hapo msikitini Nunge kaacha vijana mahiri na makini wanaodarasisha na kuhutubu kama vivuli vya Al Marhum Shekhe wao.

Hao ni akina Ustadh Abdallah Sadiki na Ustadh Abdi Musa na Sheikh Mustafa Rajab, Imam mkuu wa Masjid Gaddafi wa Dodoma, ambaye ndiye Sheikh wa Mkoa wa Dodoma ni kwanafunzi wake.

Hawa wakisimama mimbarini, utakubali kuwa ni wanafunzi wake kwa jinsi walivyo mnakili shekhe wao kwa naghma na midundo, Allah Awazidishie wao nasi pamoja ari ya elimu kwa manufaa ya Umma wa Kiislamu.

Mwenyezi Mungu amtie peponi ndugu yetu na mwalimu wetu Sheikh Ahmed Zubeir.
Amin.

image_2022-07-03_211559298.png
 
SHEIKH AHMED ZUBEIR MWANAFUNZI WA SHEIKH ABDALLAH FARSY NA MWALIMU NA MLEZI WA VIJANA WENGI DODOMA

Namkumbuka Sheikh Ahmed Zubeir katika miaka ya mwanzoni 1980s ndiyo karejea Tanzania akitokea Mombasa Kenya alipokuwa akisoma kwa Sheikh Abdallah Saleh Farsy.

Sheikh Ahmed Zubeir alikuwa amerudi Tanzania katika wakati ndiyo khasa.

Waislam wa Tanganyika walikuwa wanafungua ukurasa mpya wa kutaka kubadili mengi yaliyokuwa yanawaelemea kwa miaka mingi.

Sheikh Ahmed Zubeir alichagua kwenda Dodoma kusomesha.

Kwa hakika alipokelewa vyema na vijana wa Kiislam wa Dodoma kama Faiz Mafungo, Abdulkadir Moto maarufu kwa jina la Faya, Ahmed Mnyanga, Jaffar Mjasir kwa kuwataja wachache.

Sheikh Ahmed Zubeir alikuwa kijana umri sawa na vijana aliowakuta Dodoma waliompokea kwa mikono miwili.

Haukupita muda Sheikh Zubeir akishirikiana na vijana wenzake wakaweka darsa Msikiti Nunge ambako ndiko alipowakuta vijana wenzake.

Darsa likashamiri kupita kiasi pamoja na darsa la Tafsir ya Qur’an Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na tarweh yake.

Dodoma ni Mji Mkuu wa Tanzania na Bunge lilipohamia Dodoma na Msikiti Nunge kuwa msikit ulioko katikati ya mji Waislam wengi waliokuwa serikalini pamoja na wabunge Waislam na wapita njia wakauchukua Msikiti Nunge kuwa msikiti wao.

Nunge ukawa msikiti ambao wakubwa wote wakiwa Dodoma watasali hapo na vilevile kuhudhuria darsa za Sheikh Ahmed Zubeir.

Ikawa hata kama una lako unamtafuta muheshimiwa ambae huwezi kumfikia ofisini kwake kwa vizingiti vya urasimu wa maofisa wa serikali ukimvizia Msikiti Nunge utamtia mkononi.

Shida zako zitakuwa zimemalizika.

Kama ilivyo kawaida ya neema yeyote haikosi kuusudika.

Ghafla ikatokea fitna kuwa wenye msikiti wao wanaudai.

Hiki kikawa kipindi kigumu kwa Sheikh Ahmed Zubeir kwa kiasi polisi walihusishwa katika mgogoro ule na baadhi ya Waislam kukamatwa na kuwekwa korokoroni.

Lakini hili likapita na Waislam wakaibuka na nguvu kubwa haba jana.

Kipindi hiki baada ya kupita ndipo mimi nikajuana na Sheikh Ahmed Zubeir na vijana wa Kiislam waliokuwa Dodoma.

Vijana wa Msikiti Nunge kwa ushirikiano na Muslim Students Association of the University of Dar es Salaam (MSAUD) walikuwa wakiendesha programu kadhaa pamoja.

Katika programu hizi moja ilikuwa kuwatafuta na kuwasomesha watoto hodari katika masomo ambao hali zao ni za dhiki.

Sheikh Ahmed Zubeir kwa ajili ya programu hii alikuwa mara kwa mara akija MSAUD na hivi ndivyo tukaja kufahamiana.

Wakati ule nilikuwa katibu MSAUD.

Hawa wanafunzi walikuwa chini yake na wengi wao walikuwa sekondari na yeye ndiye aliyekuwa mlezi na mwalimu wao wa Qur'an.

Iko siku mwaka jana niko na mgeni wangu katika moja ya restaurant maarufu tunakula chakula cha jioni.

Mbele ya meza yetu alikuwa amekaa kijana na binti amejitanda vizuri na watoto wadogo wawili.

Picha niliyopata ni kuwa wale ni mtu na mkewe na hao ni watoto wao.

Lakini kilichonivutia ni ule mwonekano wao kijana kavaa kanzu na kofia kapendeza na mkewe yuko kwenye hijab.

Hakika walikuwa wamependeza kuwatazama.

Si siku zote mtu unakutana na vijana kama hawa mtu na mkewe na watoto katika restaurant kama hizi.

Kila nikigeuza shingo naona yule kijana jicho lake halibanduki kwangu.

Ukapita muda tunaibana kushangaana.

Mara yule kijana akanyanyuka ghafla akaja kwenye meza yetu akatutolea salamu.

"Sheikh Mohamed Said," kijana kaushika mkono wangu tabasamu kubwa usoni kwake.

"Naona umenisahau."
Sikuweza kumkumbuka.

Mimi fulani.
Subhanallah!

Lile jina lilikuwa maarufu ofisini kwetu MSAUD.

Mwanafunzi hodari mtoto mwema katika orodha ya wanafunzi wa Sheikh Ahmed Zubeir.

Mwanafunzi akiongoza shuleni kwake katika masomo na tabia.

Imepita miaka yapata 30 tumepotezana.
Sikuyaamini macho yangu.

Nimemwacha mtoto mdogo leo tunakutana mtu mzima ana mke na watoto.

"Alhamdulilah."
Nilishukuru.

"Haya bwana sasa unafanya nini?"

Aliponitajia kazi anayofanya serkalini sote tulicheka.

Mwanafunzi wa Sheikh Ahmef Zubeir leo kawa kijana wa kutegemewa na taifa lake.

Kubwa ni kuwa hakubadilika kwa mafanikio yake.

Ni mtoto yule yule niliyekuwa nikimjua miaka 30 iliyopita akiwa sekondari.

Naamini kifo hiki cha mwalimu na mlezi wake kimempiga sana.

Nampa mkono wa rambirambi.

Naamini Sheikh Ahmed Zubeir kawaacha nyuma vijana wengi kama huyu.

Mwenyezi Mungu amtie peponi ndugu yetu na mwalimu wetu Sheikh Ahmed Zubeir.

Amin.View attachment 2279578
Poleni sana mzee Mohamed Said

Yesu anaokoa
 
Sheikh Zuberi ni miongoni mwa watu maarufu Dodoma, sikuwahi kumfahamu kwa sura ila kwa kukaa kwangu Dodoma utotoni ukiniuliza Sheikh Zuberi anaswalisha wapi nitakuambia msikiti wa Nunge japo mie si wa dini yake. Kwa umaarufu wake Dodoma nilidhani ndio huyu Sheikh Mkuu ameteuliwa nikaambiwa sio yeye
 
اينا ليله وينا اليه راجيون

Allah amuweke mahala pema wanapostahili waja walio wema, Ameen.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom