Mwalimu Nyerere na Sheikh Thabit Kombo

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,918
30,259
MWALIMU NYERERE NA SHEIKH THABIT KOMBO

Rais Ali Hassan Mwinyi anaeleza katika kitabu chake kuwa Sheikh Thabit Kombo ndiye aliyependekeza jina lake kwa Mwalimu Nyerere awe Rais wa Zanzibar.

Sikuwa nakumbuka kuwa ninayo picha hii hadi nilipoingia Maktaba asubuhi na kuikuta.

Mlamali Adam aliandika taazia ya Sheikh Thabit Kombo.

Katika maisha yangu sijapata kusoma taazia kama ile.

Mlamali kalamu yake inazungumza.

Kamweleza Sheikh Thabit Kondo akiwa kijana na usafiri wake ukiwa baiskeli.

Wakati mwingine kaipanda.
Wakati mwingine anaikokota.

Mlamali huyo.

Anakutaka wewe msomaji utembee katikati ya mistari uhangaishe bongo lako.

Anamweleza Thabit Kombo watu wanamkimbilia kutafuta nusra za ndugu zao wanaoteseka jela.

Wananchi wa kawaida wanashughulishwa na mapinduzi.

Hapa kalamu ya Mlamali inabadili mapigo.

Anatanguliza neno, "Ami," kisha ndipo linafata jina la Thabit Kombo.

Huyu si Thabit Kombo yule aliyekuwa anakokota baiskeli.

Siwezi kuendelea kueleza.

Mlamali Adam ni sheikh, alim wa kutajika.

Nimewahi kuhudhuria darsa yake London, High Bennett nyumbani kwa Sheikh Mohamed Abubakar, Mzanzibari mwanasayansi wa nuclear.

Naam.
Utastarehe.

Hadi leo sijapata jibu kwa nini Sheikh Mlamali alimwandika vile Sheikh Thabit Kombo.

Miezi michache iliyopita kuna kijana kutoka mbali kawasiliana nami.

Huyu kijana anatafiti maandishi ya Mohamed Mlamali Adam.

Tuvute subra.
 
Back
Top Bottom