Taarifa za mikopo midogo midogo ya kibiashara!

Ahsante sana Maxence Melo kwa kutembelea uzi huu.

Ni muda sasa hatujatoa updates. Ila nilitamani kama tungekuwa na database ya mikopo ambayo tunaweza kuwa tunaweka dates kila zinapopatikana taarifa mpya.

Kama mnaweza kutupa nafasi hiyo, na mie naweza kutoa mchango wangu kwa kuiwekea tarifa mpya kila ninapozipata. Kwa jinsi uzi huu ulivyo, inatia uvivu kutoa updates.
 
Last edited by a moderator:
Nilitaka kukopa saccos ni kama million 10, nilitakiwa kudiposite 20%(2m)ambazo zitarudishwa nikimaliza mkopo, then kunaghrama za mkopo,nikajikuta kimsingi nitapata 6m,nikakimbilia access bank


Huko imekuwaje na riba yao ni kiasi gani??
 
Niaje wana jf? Nina habari njema kwa wale walio ucngizin kuhusu suala la mikopo.kwa huku niliko kuna chama cha kibiashara kiitwacho BRAC.kinajihusisha zaidi na utoaji mikopo.By the way ni loans zenye masharti mepesi na riba zao ni nafuu.kwa hapa k.njaro wana branches kadhaa ila cjajua kwa huko mliko.
 
- ingine ni Opportunity microfinance nayo inatoa mikopo midogomodogo iko pale ilala karume ukishuka karume ukauliza watakuonesha ofisi zao,

- na ingine ni Tujijenge microfinance ltd nayo iko kijitonyama wanatoa mikopo midogo midogo namna ya kujiunga nenda pale kajaze fomu zao

- wengine ni Mapambazuko saccos wao wanapatikana Tabata relini ndani ya jengo la SDV TRANSAMI pale pale kituoni mbele kidogo na ofisi za mwananchi namna ya kujiunga nenda kajaze fomu zao za kujiunga wanatoa mikopo ukiwa mwanachama wao na wengine nikiwakumbuka nitakutajia pia
 
Kuna microfinance moja inaitwa Enterprise Finance Limited, iko Sinza Mapambano. Wanafaa sana kwa mikopo ya chap chap. Hiyo mikopo wao wanaiita Quick Finance. Wanapokea hata collateral za magari au barua ya mwajiri. Ukiwa na deal hata saa 12 jioni unapata mkopo. Ili kufahamu Riba na Viwango vya mkopo watembelee au twanga 'google'.
 
mkuu dark city,kama niko nje je na ninataka millioni 200,na sina kazi nategemea 'benefits' /social fund inakuwaje?

Ahsante sana imaney,

Mimi si mtaalamu wa mambo ya fedha ila nadhani kwa benk nyingi za Tanzania jambo kama hilo litakuwa gumu. Hata kwa wafanyakazi wa hapa nchini, ili benki ikupe mkopo lazima upate barua ya mwajiri na akubali kupitisha mshahara wako kwao ili wakate kilicho chao. Sasa kwa mtu ambaye yuko nje ya nchi, kwa kweli sina hakika itakuwaje.

Labda tuzidi kuwauliza wadau kama kuna mwenye taarifa zaidi...
 
Last edited by a moderator:
Ahsante sana imaney,

Mimi si mtaalamu wa mambo ya fedha ila nadhani kwa benk nyingi za Tanzania jambo kama hilo litakuwa gumu. Hata kwa wafanyakazi wa hapa nchini, ili benki ikupe mkopo lazima upate barua ya mwajiri na akubali kupitisha mshahara wako kwao ili wakate kilicho chao. Sasa kwa mtu ambaye yuko nje ya nchi, kwa kweli sina hakika itakuwaje.

Labda tuzidi kuwauliza wadau kama kuna mwenye taarifa zaidi...

thanks mkuu
 
TIB wanahitaji a good project proposal, mwenye format nzuri please can you pm me?


Kama kuna habari zaidi tunaomba utuwekee hapa.

Kwa mfano, wanahitaji security ya namna gani, amount wanayotoa, interest rates na kama wanakubali kutoa katika form ya overdraft.

Tutashukuru sana kwa kutuelimisha.
 
Babu ahsante kwa taarifa ila hizo riba..... Mmmh!
Hizo riba ndiyo zinasababisha mkopaji ashindwe kulipa mkopo na kupelekea majanga ya kuchukuliwa/kuuzwa kwa mali zake kama nyumba na mashamba na hivyo kusababisha migogoro katika familia nyingi hivi leo. Benki Kuu wasimamie hili jamani!!!!!!!!
 
Wadau mimi mshahara wagu total ni 650,000 ukiondoa makto take home ni 540,000.naitaji kampuni yetu ipitishie mishahara yetu benki ya crdb au kcb ili turuhusiwe kuchukua mikopo.hivyo naomba mwenye ufahamu anijuze kwa mshahara huo nikikopa milioni 10. Nitaweza katwa sh ngapi na nitabaki na nini take home?then ni benki gani unaweza kunishauri yenye unafuu hapa dar?hatujaanza kupitishiwa mishahara benki but tumeambiwa tuamue ni benki gani then mwajiri wetu apitishie huko mishahara yetu...ushauri plzzz wadau
 
Back
Top Bottom