Taarifa ya Mhe.Joseph Selasini, Aanzisha M4C leo huko Rombo

Ni Mimi Msiogope

JF-Expert Member
May 28, 2012
352
200
Taarifa kwa Umma:

Jimbo la Rombo limekuwa na wawekezaji wa ndani na nje pamoja na wafanyabiashara wakubwa na wadogo lakini wamekuwa wakiwekeza nje ya Jimbo na hivyo tatizo la Ajira kwa vijana wa Rombo limeendelea kukua kila siku. Kama nilivyoahidi mwaka 2010 kwenye kampeni tayari wawekezaji wameanza kurudi kuwekeza Rombo na wengine watarudi kuwekeza Rombo.

Mfano ni kiwanda cha Juice na Maji Safi cha SEQUA ambacho kimeanza na uzalishaji wa Maji ya kunywa na Juice zitaanza kutengenezwa hivi karibuni. Lengo ni kuwapa vijana Ajira pamoja na kukuza pato la wakulima wa Matunda. Nitoe Wito kwa wana-Rombo kuanza kulima matunda ya aina mbalimbali kwa wingi ili waweze kukidhi makitaji ya kiwanda hicho ambapo kila siku yatahitajika matunda kati ya tani 5-10.
Pili jana nimezindua kiwanda cha mikate kinachomilikiwa na Tumaini Center ambapo kina uwezo wa kuzalisha mikate 250 kwa saa moja. Tumaini Center ni kituo cha kuwasaidia watoto Yatima kupata Elimu na kwa sasa kina watoto zaidi ya 350 ambapo wapo kwenye level mbalimbali za Elimu kuanzia Primary hadi Chuo kikuu. Nimewaahidi 5million kutoka kwenye CDCF ili ziweze kuwasaidia japo wanafunzi kadhaa kupata elimu hiyo kwa kuwa kituo hiki kimekuwa kikijiendesha kwa miradi yao midogo midogo. Natoa wito kwa Wana-Rombo popote walipo kukisaidia kituo hiki kwa hali na mali ili kiweze kuendelea kutekeleza majukumu yake mazuri kwa ustawi wa Jamii yetu. Kwa wale wasiojua namna ya kukichangia naomba tuwasiliane kwa maelekezo zaidi.

Haya yote nitayasisitiza kwenye Mikutano yangu ya M4C nitakayoianzisha leo tarehe 20-09-2012 hapa Rombo na kumalizika tarehe 2-10-2012.
Leo nitaanzia kata ya Nainjara Reha ambapo pamoja na mambo mengine nitazindua matawi na ofisi kadhaa za Chama wilayani hapa.

Ahsanteni, M4C.
Joseph R. Selasini
Mb.Rombo (CHADEMA)

Source:Facebook Page.. www.facebook.com/Joseph Selasini
 
Höngera mbunge wangu. Nafarijika kwa machache uliyoanza kuyafanyia kazi. Usiache kupita pale kwetu Mahida. Tunahitaji M4C iliyoshiba, watu wetu pale wamelala sana, wanahitaji kuamshwa.
 
M4C inahitaji kusambazwa kila nyumba nchi nzima hadi kufikia 2015.. Kila mmoja kwa nafasi yake aisambaze elimu ya mabadiliko kadri iwezekanavyo.
 
Höngera mbunge wangu. Nafarijika kwa machache uliyoanza kuyafanyia kazi. Usiache kupita pale kwetu Mahida. Tunahitaji M4C iliyoshiba, watu wetu pale wamelala sana, wanahitaji kuamshwa.

mheshimiwa Selasini, Mahida kuna tatizo kubwa sana katika shule ya sekondari ya Mahida. Shule hii imekua ikifelisha tangu kwa zaidi ya Miaka mitano mfululizo. Headmaster amekua ni chanzo kikuu cha haya yote,wananchi wamelalamika vya kutosha kwa mkurugenzi na kwa mkuu wa wilaya. bila shaka malalamiko yako pia kwa naibu waziri wa elimu. Bila watoto kusoma pale mahida hakuna maendeleo, miaka ya mwanzoni shule ilipeleka hadi chuo kikuu vijana wengi wa mahida, na sasa ni chachu ya maendeleo pale mahida, ila kufeli huku kwa sasa kumekatisha matumaini kabisa ya maendeleo pale mahida. Vijana waishiyo Dar es salaam na mikoa mingine wako tayari kusaidia kwa hali na mali ili kufanikisha maendeleo ya elimu mahida ila wanakwamishwa na uongozi mbovu wa shule. Kulikua na mpango wa kuanzisha high school tangu miaka mitatu/minne iliyopita. Madarasa yalijengwa kwa kiwango cha chini sana utandani ni banda la ng'ombe. Nakuomba ufanye utafiti wa kutosha, fuatilia shule hii, na hatma ya High school. Pia usisahau swala la maji na swala la Tembo kutoka kenya wanaharibu mazao ya wakulima alafu eti serikali inawafidia shs.100,000/= kwa ekari moja, ambocho ni fedheha kubwa sana kwa wakulima. Bila shaka unajua kilimo kilivyo cha mateso kule Rombo.Naomba uangalie matokeo hapo chini.
Matokeo ya Mtihani -Mahida Secondary School
Mwaka
DIV 1
DIV 2
DIV 3
DIV 4
DIV 0
2006
2
6
30
50
3
2007
7
9
48
121
12
2008
2
8
27
28
0
2009
0
11
30
89
23
2010
0
0
8
82
94
2011
0
0
2
69
54
 
Mh. Selesini kata ya kirongo samanga hamna hata kiongoz wa CHADEMA kawaamshe mkuu pia ufisad uliokithiri kwa kata nzima michango ni mingi ambayo matumizi yake hayapo wazi.SHULE YA MSINGI MAMBA ambayo mkuu wke wa shule ni FOCUS TESHA anawafisid sana wazaz wa kata hii mapato na matumizi hayajulikan nenda uongee na wanachi wa kawaida wakupe matatizo yao ucje ukapoteza jimbo
 
Taarifa kwa Umma:......
Ahsanteni, M4C.
Joseph R. Selasini
Mb.Rombo (CHADEMA)
Yaani badala ya kuungana na kamanda Lissu kumfariji hata kwa siku ya leo anayotegemea kumuaga baba yake wengine bado wanaendelea na M4C simamisha hiyo kuonyesha heshima kwa Kamanda Lissu.
 
A big up Kamanda Selasini, thats the way to go; tunakuombea salama katika vuguvugu lako la M4C huko Rombo kwani bado matukio ya Nyororo Mufindi bado ni fresh kwenye akili na mioyo yetu. RIP David Mwangosi
 
Avoid single track mindedness kama unataka wana JF wakuchukulie kama mchangiaji mwenye fikira yakinifu!!!

Katika dunia halisi isiyo ya kusadikika ya zama za Hayati Shaaban Robert RIP, watu lazima wagawanye majukumu ili maisha yaweze kuendelea. Kikosi kilichopo singida mashariki na kile kilichoshiriki Dar vinatosheleza kuwaliwaza wafiwa wote akiwamo kamanda Lissu.

Naamini hata Mzee Antipasi Lissu angependa kuona vuguvugu la M4C linaendelea kama njia bora ya kuienzi kazi iliyotukuka ya kijana wake kamanda Tundu Lissu. RIP Mzee Lissu
 
Avoid single track mindedness kama unataka wana JF wakuchukulie kama mchangiaji mwenye fikira yakinifu!!!

Katika dunia halisi isiyo ya kusadikika ya zama za Hayati Shaaban Robert RIP, watu lazima wagawanye majukumu ili maisha yaweze kuendelea. Kikosi kilichopo singida mashariki na kile kilichoshiriki Dar vinatosheleza kuwaliwaza wafiwa wote akiwamo kamanda Lissu.

Naamini hata Mzee Antipasi Lissu angependa kuona vuguvugu la M4C linaendelea kama njia bora ya kuienzi kazi iliyotukuka ya kijana wake kamanda Tundu Lissu. RIP Mzee Lissu
 
Yaani badala ya kuungana na kamanda Lissu kumfariji hata kwa siku ya leo anayotegemea kumuaga baba yake wengine bado wanaendelea na M4C simamisha hiyo kuonyesha heshima kwa Kamanda Lissu.

Makamanda wote wakihudhuria msiba utakuwaje?.. Ina maana wewe upo msibani? Jaribu kufikiria kabla ya matumizi ya vidole
 
Makamanda wote wakihuria msiba utakuwaje?.. Ina maana wewe upo msibani? Jaribu kufikiria kabla ya matumizi ya vidole
Tatizo lenu makamanda wengine huwa mnatumia vichwa kuoteshea nywele na wala si kufikilia. sijasema wote waende kwenye msiba bali ni kusimamisha M4C angarau kwa siku moja kwa ajili ya maombolezo.
 
Nimekuona mh Selasini ukiongea na vijana naeneo ya soko la mrere nilipokuwa napita kuelekea rongai kikazi.ajitahd kuwaletea maendeleo wana rombo na watz kwa ujumla.go futher mh.!
 
Yaani badala ya kuungana na kamanda Lissu kumfariji hata kwa siku ya leo anayotegemea kumuaga baba yake wengine bado wanaendelea na M4C simamisha hiyo kuonyesha heshima kwa Kamanda Lissu.

wewe unaeweka misiba mbele kuliko mambo ya maendeleo unapaswa kuogopwa kama ukoma!m4c ni pamoja na kutambua fursa na vikwazo vinavyowakumba wananchi ili kuvifanyia kazi!unategemea kwny msiba wa babake kamanda Lisu chdm wote waende?PAMBAFU YAKO!haya mambo ya kukumbatia misiba ni vikwazo ktk maendeleo,ndo maana wawekezaji toka nje hawaajiri watz kwa sababy ya misiba icyoisha!
 
Yaani badala ya kuungana na kamanda Lissu kumfariji hata kwa siku ya leo anayotegemea kumuaga baba yake wengine bado wanaendelea na M4C simamisha hiyo kuonyesha heshima kwa Kamanda Lissu.

Akamwambia, "Bwana, kama ungalikuwapo, ndugu yangu hangalikufa". Vision ya mabadiliko ni, pamoja na mambo mengine, kuondoa vifo visivyo vya lazima vilivyosababishwa na mfumo mbovu wa CCM uliotawala nchi hii kwa zaidi ya miaka 50 bila majibu ya matatizo yetu kama taifa; huenda hata Mzee wetu Antipas Lissu (RIP) kaangukia katika kundi hili la "kuuwawa na mfumo mbovu".

Huenda chama kingine kingelikuwepo madarakani wengi waliokufa wasingelikufa! The best way ya kumuenzi mzee wetu ni kwa kufanya ambayo yataondoa sababu za vifo visivyo vya lazima and M4C is one of them. Je, walijua hili?
 
Tatizo lenu makamanda wengine huwa mnatumia vichwa kuoteshea nywele na wala si kufikilia. sijasema wote waende kwenye msiba bali ni kusimamisha M4C angarau kwa siku moja kwa ajili ya maombolezo.

Like father Like Son.
Sishangai kwenu matusi na kejeli ipo kwenye Ilani yenu.
 
Back
Top Bottom