Taarifa ya habari TBC..Vichekesho vitupu!!!

Yaani nakwambia tangu wamfukuze TIDO MHANDO mambo vululu vululu.Mi siku hizi hata siiangalii kabisa.
 
Kumbuka boss aliyepo TBC ndo aliandika barua kufungia (soma kutishia) gazeti la Mwanahalis na Mwananchi ETI yanaisakama serikali akiwa maelezo. Nilidhan yuko makini kumbe naye makajanja wa management. We are after professionalism pale TBC si UCCM
:shock:
 
Nashauri kwa vile wanashindwa kusoma taarifa habari live, basi wawe wanafanya recording then editing. Kweli wanatia aibu!!!
 
sasa utakuta wanamuweka yule jamaa wa habari za biashara Joseph Msami yani wanazuga yuko live wakati anaonekana kabisa karekodiwa,saa zingine utakuta anaongea alafu cd inakwamakwama mpaka aibu.
 
hamjawakuta kazini nyie mtawahurumia. wengi wameajiriwa kwa kujuana na wanaqfanya kazi sio kwa kuelewa bali kwa kuriri. unajua ufundi mitambo sio kusomea tu bali ni sanaa. sasa utakuta mtu ameenda kusomea sababu anaona kuna dili sasa inapokuja hutakiwi kufikiria kwa kutumia masaburi hapo ndo ngoma inachaha!
 
Mi waliniudhi,walishindwa hata kuttuonesha soccer michuano ya club bingwa africa kule eq.Guinnea na Gabon.Private TV oyeeeeeeh!!!
 
mbona hio kwa tbc imekuwa ni tabia yako-
kila siku ni hivyo-jaribu kufatilia utaona-hawapo makini kabisa
 
Yaani TBC sasa inatia kichefuchefu, huwa naangalia kila siku siku asubuhi lakini hamna siku ambayo wanapatia.

Kuna wakati mtangazaji wao wa michezo anakuwa anawaambia studio wazime sauti za ajabu ajabu ambazo zinamuingilia na kumfanya ashindwe kuendelea kutangaza.

Kuna tatizo sana kwenye wataalam wao wa kubadilisha matukio, sijui jamaa saa zote wanakuwaga mitungi??

Kichekesho juzi mgeni wao wa asubuhi kaingia na mobile phone yake pale ikaanza kuita, Marine akamwambia aizime yaani duh!
 
kwa hili limenigusa live,Tbc hamna kitu imekuwa ya wahuni,mafundi mitambo hovyo,vipindi hovyo,tunashindwa hata kupaste kwa KBC NA UBC?kwa kweli km kuna uwezekano wa TIDO kurudi arudishwe tu kunusuru televishen ya taifa ama laa! Atafutwe mwingine mwenye uwezo wa kuiendesha na kulinda heshima.inasikitisha sana kuona hali inayoendelea.I HATE TBC
 
Pia chunguzeni yale maneno yanayopita chini wakati wa taarifa ya habari mtagundua mara nyingi kuna makosa typo.
 
hivi nahisi wana mitambo ya kichina hawa jamaa,maana ni muda sasa makosa haya anatokea.ina maana wameshindwa kabisa kurekebisha hilo?
Aibu kweli asee ningekua mtangazaji pale ngejiuzuru
 
Back
Top Bottom