Cha msingi dakitari kasema mhe. hana matatizo makubwa yeyote ya kiafya ukiondoa hilo la kuwa na damu nyingi. Nashukuru kwa huduma wanazoendelea kuzitoa kwa mkuu wa nchi yetu. Hata hivyo, inabidi wamaanishe hivyo, kwamba hana matatizo makubwa zaidi ya la damu kuwa nyingi. Vinginevyo, watanzania tutakuja kuumbuka kama mengine yatatokea kwa sababu tu ya usiri uliokuwa umekumbatiwa. Isiwe suala la longolongo na usanii mkifikiri eti kuumwa ni suala geni kwa rais. Ninachoamini ni mwanadamu kama binadamu wengine. Hivyo, kuumwa si kitu kigeni. Isipokuwa kama kundi fulani ikatokea likawa na mtazamo tofauti na huu wa rais kuwa miongoni mwa wanadamu, basi ni hatari!! Namuombea tu kwa Mwenyezi Mungu azidi kumuongezea siku zake za kuishi.