Taarifa nyeti: Mbinu za wizi wa kura hizi hapa - PART 2

Rutunga M

JF-Expert Member
Mar 16, 2009
1,769
1,382
Jamani pole na majukumu.

Leo nawaletea taarifa ya pili ya namna ya kuzuia wizi na mparaganyiko wa uchaguzi wetu.Sisi watu wa mungu tunapenda atakayeshindwa awe ameshindwa haswa bila kuwepo nguvu ya ziada kutoka katika mfumo usio rasmi.

Fuatana nami.

1:UPINZANI KOMARIA ORODHA YA WALIOMO KATIKA DAFTARI LA KUDUMU

Katika suala hili wapinzani chonde chonde kama inawezekana achaneni na mikutano ya kampeini kabisa ili mshugulikie suala la daftari la kudumu-uhai wa ushindi kwa chama husika umebaki hapa tu. achaneni na hoja za mnyika za kutisha press conference eti kudai daftari,tumia njia zilizowekwa na tume.andika barua rasmi kwa tume iwe na kumb no,ipeleke kwa disparch NEC.

Au tuma mtu anayeheshimika kama mbowe,mbatia,lowassa,juma duni au mwanasheria wwenu afike NEC aombe daftari kwa njia iliyo wazi,bila kumungunya maneneo au kugombana na mtu pale lazima mpate majibu au mnapewa au hampewi na kwa nini? from there mnaweza anzisha ya kuitisha press conference kueleza kunyimwa daftari au kupata.

Mkipata daftari husika toa copy sambaza kwa mawakala wenu,lakini nawahakikishi itakuwa ngumu kidogo kupewa hilo daftari.

Kesho 12/10/2015 NEC imeandaa mkutano baina yo na vyama vya siasa kikubwa katika mkutano huo agenda kubwa iwe ni kupewa dafatari la kudumu.

Kumbuka NEC imesema wapiga kura ni milion 23+ lakini taarifa rasmi iliyoko NBS wapiga kura ni milioni 24+ bonyeza hapa http://www.nbs.go.tz/ msicheze na TAKWIMU.

2:UKAWA OMBA KUJUA ALIPO MKUU WETU WA MAJESHI

Kama kuna ambaye hawezi kuhusisha suala hili na uchaguzi huu arudi shule.(sitajadili sana kulinaga na sheria ya mitandao)

Kumbuka hivi karibuni kijana mmoja 'anadaiwa' kumzushia Mwamunyage kuwa kalishwa sumu na jeshi lilitoa taarifa ilifuatyo

"Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Luteni Kanali Juma Sipe, imeweka wazi kuwa Jeshi na Wizara kwa kushirikiana na mamlaka husika, wanachunguza watu hao na kuwataka waombe radhi mapema kabla ya hatua hizo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Jenerali Mwamunyange ni mzima wa afya na aliondoka nchini Jumanne iliyopita Septemba 22, 2015, saa 10.45 jioni kwa ndege ya Shirika la Ndege la Emirates kwenda Rome, Italia kwa ziara ya kikazi ya siku TISA (9) kwa mwaliko wa Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo, Jenerali Claudio Graziano." Soma hapa
chini ‘Waliomzushia Jenerali Davis Mwamunyange waombe radhi’

Sasa kuanzia septemba 22,2015 hadi leo october 11,2015 ni siku 20.Je alimaliza ziara yake? amerejea? yuko wapi?.ukawa pata majibu ya alipo huyu kiongozi wetu kwa mfumo ulio mzuri kabisa,amabo hauingilii mamlaka ya jeshi letu.

Maswali haya wala hayavunji sheria yoyote bali kutka kujua alipo.Suala hili lina impact sana katika huu uchaguzi.

Mungu awabariki .
Nitarejea tena
 
**HAKI,UWAZI NA UKWELI,UTADUMISHA AMANI YA TAIFA LETU**
**AMANI HAILETWI KWA MABAVU**
**USTAARABU NA MARIDHIANI SAFI HURU NA HAKI==="AMANI""
ii
 
Kuna watu sijui wanawaza kwa kufikiri viungo gani vya mwili. Daftari lipo wazi na kila chama cha siasa kina haki ya kulipata. Sasa eti waache mikutano ya kampeni kuhangaikia daftari huu si ufedhuli kabisa?
 
Mkuu, kuna watu wajinga sana sijapata kuona. UKAWA ni mkusanyiko wa wajinga na wapumbavu

Tulieni mnapanic nini kama sio uwoga wa kusombwa na mafuriko!
 
Kuna watu sijui wanawaza kwa kufikiri viungo gani vya mwili. Daftari lipo wazi na kila chama cha siasa kina haki ya kulipata. Sasa eti waache mikutano ya kampeni kuhangaikia daftari huu si ufedhuli kabisa?
Japo hatupo kada moja ila nakuunga kidole hata mimi sijaelewa watu waache kampeni kutafuta daftari kwani chama hakina viongozi wengine au anamaanisha sasa hivi ofisi zinefungwa?Hata mimi hapo hapana.
 
Daftari la kudumu la wapiga kura ni muhimu kuliko kila kitu. Usikute kuna watu milion 10 wameingizwa kinyemela. Ukawa washughulikie hilo kwa nguvu zote.
 
Kuna watu sijui wanawaza kwa kufikiri viungo gani vya mwili. Daftari lipo wazi na kila chama cha siasa kina haki ya kulipata. Sasa eti waache mikutano ya kampeni kuhangaikia daftari huu si ufedhuli kabisa?

Povu la nini wakati haya ni mambo ya ukawa? Hahaha kweli ww mwanamke una shida
 
Mtoa hoja amenena hivi kama mtu unataka haki si tu indendeke na ionekane imetendeka basi ni busara daftari la wapiga kura na vinginevyo vikawekwa wazi. Hii itaondoa malalamiko kwa yeyote atakeyeshindwa awe CCM au Chadema. Ndio maana hata wakati wa kupiga kura sanduku la kura linashuhudiwa na mawakala wote kuwa lipo tupu. Kwa analogy hiyo hiyo hakuna kigumu hapo Tume weka wazi daftari tulijue na tuwajue wapiga kura kabla ya kupiga. Kwanini vitu vidogo na vya msingi tunavifanya kuwa hoja hii nikuchochea malumbano yasiyokuwa ya lazima.!
 
LIWEKWE WAZI kwa nani tarifa za mtu binafsi siyo za wanasiasa wakome kutaka tarifa zetu mie zangu sitaki wapewe wanasiasa hata kidogo myika akapewe zake na mkewe siyo zetu.
 
Mkuu, kuna watu wajinga sana sijapata kuona. UKAWA ni mkusanyiko wa wajinga na wapumbavu

Na ninyi ni genge la wahuni tu, mafisadi wakubwa na majangili, mkifuatiliwa na issues zenu kutibuliwa mnaanza kulia lia tulieni tu dawa iingie vizuri........
 
We mhamiaji haramu bado uhamiaji hawajakudaka tu?

Hivi ni wapi mleta mada ameongea vibaya au kuvunja sheria? mbona mnaangaika hivyo fisiem? kupanic kwenu ndio kunatupa maswali kuwa mnatumia mbinu chafu kuwin huu uchaguzi na kamwe haitawezekana LOWASSA KIMBIZA HAWA BATA
VIVA UKAWA!!!!!
 
LIWEKWE WAZI kwa nani tarifa za mtu binafsi siyo za wanasiasa wakome kutaka tarifa zetu mie zangu sitaki wapewe wanasiasa hata kidogo myika akapewe zake na mkewe siyo zetu.

Hivi ata unajua hapa kinaongelewa nini au ni uzezeta unakuendesha utapike vile unatapika hapa? vitu kama hivyo lazima viwekwe wazi ili kusizue maswali yatakayosababisha uvunjifu wa amani NA NI LAZIMA VIONGOZI WETU WAVIJUE.
VIVA UKAWA!!!!
 
Kuna watu sijui wanawaza kwa kufikiri viungo gani vya mwili. Daftari lipo wazi na kila chama cha siasa kina haki ya kulipata. Sasa eti waache mikutano ya kampeni kuhangaikia daftari huu si ufedhuli kabisa?

Kwa nini wasiwape hilo daftari?Nyie MACCM tumieni akili hapo ugomvi ni nini?Kama tume ina daftari shida ni nini kutokuwapa nakala kwa kila vyama vinavyogombea? Mnawaza uwizi tu na acheni kujitoa ufahamu
na nawaambieni mnacheza na amani ya nchi hii.NEC wapeni hiyo nakala maana muda umeisha kabisa.
 
Back
Top Bottom